Tinted za kimarekani kwenye gari tunazipenda lakini zinahitaji uvumilivu tu kwakweli

Tinted za kimarekani kwenye gari tunazipenda lakini zinahitaji uvumilivu tu kwakweli

American tinted ikifika usiku unaweza ukajikuta unatembea na gari huku umeshusha vioo🤣
kilo.jpg
 
Tuseme tu ukweli! Ka tinted! ni kaugonjwa ketu wengi!

Sina maana huu uzi niwakuwatambia hapana; siyo lazima niwe na kagari ili kuifurahia tinted, bali hata napopewa lift tu madhila, kero na utamu wa tinted huwa unaonekana!
vioo vyeusi ama tinted hizi zilizoeleka sana kwa magari ya VIP nchi za wenzetu lakini pia mbali na kufanya aliyepo ndani ya gari watu wa nje wasimuone inasaidia pia kupunguza mionzi au mwanga wa jua ndani ya gari.

Kama nilivyosema faida zake 2 nazozifahamu ni hizo ila hii ya kuweka kioo cha mbele wind screen kiukweli ni hatari maana kama ulivyosema kuona ni shida.Ila pia kuweka tinted sana nayo ni hatari maana wajamaa wakikuvizia ndani ya gari umekwisha.Hakuna atayekuona japo muda mwingine pia huondoa usumbufu wa aliyeko nje kuweza jua nani yupo ndani ya gari hasa hawa dada zetu kuonewa na vibaka maana wakijua ni wadada huwaibia.
 
Faida ni nyingi lakini swali mbona huko tunakoyanunua wao hawaweki tinted inamaana hakuna vibaka?
 
Faida ni nyingi lakini swali mbona huko tunakoyanunua wao hawaweki tinted inamaana hakuna vibaka?
Kuna baadhi huwa yanakuja kioo chake tayari ni tinted na huwa ni vioo vya nyuma hasa nakumbukia Nissan Patrol model ya 1996 na hata harrier za 2010 vioo vya nyuma zinakuja ni tinted ndani ya kioo kabisa.

Gari kuja bila tinted siyo shida sababu siyo kila mtu anapenda tinted ndiyo maana rollers zimetengenezwa kwa atayependa kuweka .Kumbuka kuna nchi jua siyo kali kihivo sasa ukitengeneza gari na tinted unakuwa hujamsaidia mnunuzi au nchi nyingine sheria zinakataza au nchi nyingine kiwango cha uhalifu ni kidogo au hakuna kabisa hivo watu kujiachia ndani ya gari waonekane hakuna shida.
 
harrier.jpg
 
Kwhy huu uzi ni wa wenye magari tu??

Hv wenzetu mnafanya kazi gani had mnamiliki magari??

Maan mie kila nikipambana napigwa nockout tu,sina hat uwezo wa kumiliki hiko kioo cha tinted.

Mungu anijalie na mm nipate rizki ya kumiliki mkoko wangu km nyinyi[emoji120]
 
Kule wana self respect na hawafatilian , ila bongo nyoso umbea mwing umeweka tuu Tinted mtu anakazan kuptsha macho ndan ya Gari [emoji1783][emoji1783]
Tunaongez privacy ZETU
Mheshimiwa umemaliza kabisa sababu maana hii ndiyo yenyewe hasa hata nguo nyeupe wakati mwingine nao wanatusumbua akikuona mfupi tu kasimamisha gari ila ikiwa tinted anajiuliza nisimamishe au, upo kwenye foleni mwenzako yupo kwenye daladala lazima maneno yatatoka huyu gari zima yupo peke yake atakuwa fisadi halafu angalia shati lake ndiyo maana bongo watu wanapenda tinted
 
Kwhy huu uzi ni wa wenye magari tu??

Hv wenzetu mnafanya kazi gani had mnamiliki magari??

Maan mie kila nikipambana napigwa nockout tu,sina hat uwezo wa kumiliki hiko kioo cha tinted.

Mungu anijalie na mm nipate rizki ya kumiliki mkoko wangu km nyinyi[emoji120]
Kuwa na amani mi mwanzisha Uzi pia sina gari lakini naona magari ya watu navyopewa lifti!
 
Unaona fresh au unavumilia
Naona vizuri sana.

Yaani nilitaka nipige zile American Tinted zinazouzwa kwenye viboksi muuzaji akaniambia hapana, hizo piga kwenye vioo vya milango sababu ukipiga na kwenye kioo cha mbele usiku utapata shida, ya kwenye kioo cha mbele piga (alitaja jina) hizi ziko kwenye roller na alikuwa anauza elfu 40 kwa kioo kimoja cha mbele nikanunua na hiyo ya kwenye vioo vya mbele.
 
Naona vizuri sana.

Yaani nilitaka nipige zile American Tinted zinazouzwa kwenye viboksi muuzaji akaniambia hapana, hzo piga kwenye vioo vya milango sababu ukipiga na kwenye kioo cha mbele usiku utapata shida, ya kwenye kioo cha mbele piga (alitaja jina) hizi ziko kwenye roller na alikuwa anauza elfu 40 kwa kioo kimoja cha mbele nikanunua na hiyo ya kwenye vioo vya mbele.
Inaitwaje
 
Inaitwaje
Jina sikumbuki ila linakuwa kwwnye roller dizaini kama rollers za kwenye vitambaa vya nguo kwahiyo wanakukatia.

Yaani ningetaka kupiga pamoja na vioo vya milangoni ingenigharimu kama 160,000. Nilinunua hicho cha kioo cha mbele kwa elfu 40 na nikanunua zile za viboksi American Tinted nadhani bei yake ni kati ya 25,000 hadi 40,000 bei yake sikumbuki vizuri ambazo niliweka kwenye vioo vya milangoni.
 
Inabandikwa kwa ndani au inje
Kushoto ni kioo cha mbele chenye hiyo tinted na kulia mlango wa gari nimeufungua kwahyoi hapo hakuna kizuizi cha kioo, ni wazi.

ukiangalia tofauti ya sehemu ya kioo chenye tinted na hiyo sehemu isiyo na kizuzi tofauti ni ndogo sana ila ukiwa nje kioo ni cheusi ila waliomo kwenye gari utawaona kwa mbali.

Ni tinted nzuri sana.

IMG-20230409-WA0013.jpg
 
Back
Top Bottom