Tinted za kimarekani kwenye gari tunazipenda lakini zinahitaji uvumilivu tu kwakweli

Tinted za kimarekani kwenye gari tunazipenda lakini zinahitaji uvumilivu tu kwakweli

Wanaoweka tint vioo vya mbele hawaweki huo uchafu unaitwa american tinted, kuna special tint za kuweka kioo cha mbele gharama yake kwa kioo cha mbele siyo chini ya 80,000 tzs, mimi nimeweka na ninaona vizuri tuu usiku
Zinaitwaje hizo?
 
Tuseme tu ukweli! Ka tinted! ni kaugonjwa ketu wengi!

Sina maana huu uzi niwakuwatambia hapana; siyo lazima niwe na kagari ili kuifurahia tinted, bali hata napopewa lift tu madhila, kero na utamu wa tinted huwa unaonekana!

Tinted ni kilevi kama vilevi vingine visivyolewesha!
Kupenda kunywa Pepsi baridi ni kilevi lakini hakileweshi, kunywa energy drink ni kilevi lakini hakileweshi, kungalia tamthilia ni kilevi lakini hakileweshi, kuangalia mizigo ni kilevi lakini hakileweshi n.k

Kupenda kutumia tinted ni kilevi pia! Ukizoea huwezi kufurahia gari isiyo kuwa na tinted kwani utajiona kama umekaa kibarazani!

Zamani tulizoea kuweka tinted za vioo vya pembeni lakini sasa teknolojia inazidi kukua!
Hivi sasa kuna ingizo jipya almaarufu American tinted!

American tinted wamekuja na tinted ya kioo cha mbele ambacho inadaiwa ukiwa ndani ya gari unaona fresh kabisa!

Mimi ni miongoni mwa watu waliovutiwa kujaribu kuishuhudia American tinted ya kioo cha mbele aina ya 4M!

Ukweli ni kwamba haya ndiyo niliyogundua baada ya kuitumia.
  • American tinted ya kioo cha mbele mchana unaona vizuri kama kawaida lakini usiku inafifia
  • Usiku inahitaji umakini mkubwa kuona vitu ambavyo havina taa au non reflecting object
  • Usiku ukiona mtu anakwenda mbio na tinted ya mbele tambua anatumia uzoefu wa njia (kaikariri njia la sivyo kukiwa na mabadiliko ya njia either ya tuta jipya mbele lazima aliparamie kwa surprise)
  • Kukiwa na mvua au ukungu ni mwendo wa kunyata tu kwaweli
  • Usiku tunazuga hatuna haraka lakini ukweli ni kwamba hatuoni vizuri
  • Kuhama njia kwenye two way traffic boda boda wanatukana sana maana sometimes siyo rahisi kuwaona!
KIUFUPI AMERICAN TINTED YA MBELE IMETAWALIWA NA UVUMILIVU!

Ni nzuri lakini moyoni tunateseka kimya kimya lakini tunavumilia hivyo hivyo!
Tinted ya mbele ni kuvumilia tu!

Siyo kwamba naiponda tinted ya mbele hapana, naipenda lakini starehe yake inahitaji uvumilivu tu katika majira na nyakati!
View attachment 2582037View attachment 2582038

Window tinting serves several purposes. Here are a few common uses of window tint:

1. Heat and UV Ray Reduction: Tinted windows can help reduce the amount of heat and harmful ultraviolet (UV) rays entering a vehicle making the interior more comfortable and protecting against sun damage.

2. Glare Reduction: Window tinting can minimize glare from sunlight, headlights, and other bright sources, improving visibility and reducing eyestrain.

3. Privacy and Security: Tinted windows provide increased privacy by limiting the view into a vehicle or building. They also make it more difficult for potential thieves to see valuable items inside.

4. Energy Efficiency: By reducing heat transfer through windows, tinting can help lower cooling costs in buildings and decrease the workload on air conditioning systems.

5. Aesthetics and Style: Window tinting can enhance the appearance of vehicles and buildings, giving them a sleek and sophisticated look.

It's worth noting that regulations regarding window tinting vary by jurisdiction, so it's essential to comply with local laws and regulations when considering window tinting for your vehicle or property.
 
Kifupi mimi bianfsi Tinted ni kwa kioo cha nyuma na vioo vya milango ya nyuma tu,kwa dereva siweki wala mbele,maana mara nyingi huwa nasafiri usiku,usijidanganye kuwa kuwa tinted ni salama,usiku hata ukiwa hujaweka tinted uonaji unakuwa sio mzuri,mfano kukiwa na ukungu,mvua au kutembea barabara ambayo haina mistari ya katikati au pembeni,kupata ajali na gari ya full Tinted ni rahisi sana,au vingenevyo kama mleta mada anavyosema labda uwe una nyata...
 
Window tinting serves several purposes. Here are a few common uses of window tint:

1. Heat and UV Ray Reduction: Tinted windows can help reduce the amount of heat and harmful ultraviolet (UV) rays entering a vehicle making the interior more comfortable and protecting against sun damage.

2. Glare Reduction: Window tinting can minimize glare from sunlight, headlights, and other bright sources, improving visibility and reducing eyestrain.

3. Privacy and Security: Tinted windows provide increased privacy by limiting the view into a vehicle or building. They also make it more difficult for potential thieves to see valuable items inside.

4. Energy Efficiency: By reducing heat transfer through windows, tinting can help lower cooling costs in buildings and decrease the workload on air conditioning systems.

5. Aesthetics and Style: Window tinting can enhance the appearance of vehicles and buildings, giving them a sleek and sophisticated look.

It's worth noting that regulations regarding window tinting vary by jurisdiction, so it's essential to comply with local laws and regulations when considering window tinting for your vehicle or property.
But can lower the visibility!
 
vioo vyeusi ama tinted hizi zilizoeleka sana kwa magari ya VIP nchi za wenzetu lakini pia mbali na kufanya aliyepo ndani ya gari watu wa nje wasimuone inasaidia pia kupunguza mionzi au mwanga wa jua ndani ya gari.

Kama nilivyosema faida zake 2 nazozifahamu ni hizo ila hii ya kuweka kioo cha mbele wind screen kiukweli ni hatari maana kama ulivyosema kuona ni shida.Ila pia kuweka tinted sana nayo ni hatari maana wajamaa wakikuvizia ndani ya gari umekwisha.Hakuna atayekuona japo muda mwingine pia huondoa usumbufu wa aliyeko nje kuweza jua nani yupo ndani ya gari hasa hawa dada zetu kuonewa na vibaka maana wakijua ni wadada huwaibia.
si wanunue bastola
 
Kutoroshea mademu wa chuo,wake za watu na kunyandulia humohumo.
 
Wanaoweka tint vioo vya mbele hawaweki huo uchafu unaitwa american tinted, kuna special tint za kuweka kioo cha mbele gharama yake kwa kioo cha mbele siyo chini ya 80,000 tzs, mimi nimeweka na ninaona vizuri tuu usiku
Nano Ceramic Hiyo, Wengi Wanaobwabwaja Wameweka bila Kufanya Utafiti
 
Watanzania huwa hatufanyi research ya kutosha. Hakuna hata mmoja aliyetaja shade level. Zipo, light, medium, dark, very dark mara nyingi zinakuwa rated kwa percentage % i.e 5%, 35%, 70% etc kuendana na kiwango cha mwanga ambao inaruhusu. Namba za juu 70, 80 ni light, unavyoshuka zinakuwa dark. 5% ndio darkest (limo tint)

Kabla hatujafika kwenye shade levels tint zipo aina tofauti tofauti. Kuna

Dyed tint - cheapest

Metalized - affordable

Carbon - medium

Ceramic - most expensive

Zote hizi zinapatikana kwa shade levels tofauti. Na zitakupa matokeo tofauti kuendana na ubora wa tint. Carbon na ceramic zina best heat rejection, uv protection, durability plus visibility.

Vioo vya mbele(driver and passenger side) inashauriwa kuweka 35% kuenda juu. Kwa ceramic na carbon hautapata shida kuona usiku . Windshield 70% au 80%
Kama unapata shida kuona, then haukuzingatia any of the above
 
Back
Top Bottom