Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,222
- 2,912
Toka oktoba 29, 2025 linapokuja suala la watu kuandamana, waandamanaji wamekuwa ni Jeshi la Polisi na Majeshi mengine katika maeneo mbalimbali ya nchi hususani mijini.
Hali ya askari kurandaranda mtaani wakiwa na silaha nzito badala ya raia walioshikilia mabango imekuwa ikiwatisha wananchi hali inayopelekea kujifungia ndani na kuacha shughuli zao kabisa.
Kitendo hiki kimekuwa cha madhara makubwa kwa wananchi na nchi kwa ujumla na kugeuka kuwa faida kubwa kwa Jeshi la Polisi na Majeshi mengine
Raia hufunga shughuli zao kwa siku husika hivyo kupoteza vipato vyao. Serikali inapoteza mapato yake lakini Jeshi la Polisi hulipwa "Posho ya uzururaji" huo kwa siku zote wanazopita mitaani.
Haya ni malipo ambayo hayakutengewa bajeti. Na anayelipa ni mwananchi anayekatwa kodi!
Ni sahihi kusema, wao (vyombo vya Ulinzi na Usalama) wanatamani hao wanaotangaza maandamano watangaze kila siku maana kwao ni neema.
Pia zipo tetesi mitaani kuwa baada ya kile kilichotokea Oktoba 29, 2025 majeshi (wakiwemo Polisi) waliendelea kupokea malipo ya kiasi kadhaa cha pesa kwa miezi kadhaa kwenye akaunti zao za benki ambazo hawakujua ni malipo ya nini hasa. Lakini wafuatiliaji wanafahamu malipo yale yalikuwa yanahusiana moja kwa moja na kilichotokea Oktoba 29, 2025. Malipo kama hayo yalifanyika pia kwa watoa huduma wa afya (kada ya afya) kwa sababu wanajua walivyohusika na majeruhi waliopokelewa kwenye vituo vya afya.
Ndio maana, hadi leo haujasikia kauli yoyote ya watu wa kada ya afya wakijibu tuhuma za majeruhi waliopolekwa kwenye vituo vyao zilizowahi kutolewa.