Tetesi: Tishio la Tsunami: Gari ya matanagzo inatangaza Kuchafuka kwa Bahari maeneo ya Coco Beach

Tetesi: Tishio la Tsunami: Gari ya matanagzo inatangaza Kuchafuka kwa Bahari maeneo ya Coco Beach

Ambao tupo Huku Manyara laweza Kutupata?
 
Kuna Gari ya matangazo inapita kutahadharisha Raia Juu ya kuchukua Tahadhari kwa wananchi wanaoishi karibu na fukwe za coco beach waondoke kwani bahari inaweza kuchafuka muda wowowte.

Nimejaribu kuangalia kwenye webdite ya TMA sijaona warning yoyote


Labda wamechukua tahadhari kutokana na yaliyotokea Japan
 
Duuh pale ilipo tuu ni chafu ikichafuka zaidi itakuwaje,emmbu ngoja nijisogeze na povu langu nikaisafishe
 
Kama nimeelewa honcho kikatoliki ni zoezi la kujinusuru endapo tsunami itatokea.
Si kwamba Kuna tsunami
 
TMA ukute wako sumbawanga kupata usaidizi wa utabiri wao kama wao ni kubeti tu hawana lolote
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji859][emoji859][emoji859][emoji859][emoji87][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Yalikuwa ni mazoezi ya kukabiliana na Tsunami endapo itatokea na namna watu wanavyoweza kuitikia wito pale hatari inapokuwepo.
 
Kwahio pamoja na kuweka hio attachment hamjaelewa tu kuwa hilo ni zoezi? Tsunami evacuation drill?
 
Serikali Yakanusha....Yasema Hakuna Tishio Lolote la Sunami Katika Bahari ya Hindi




Serikali kupitia Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu imesema hakuna tishio lolote la Sunami katika Bahari ya Hindi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni Septemba 5,2018, Mkurugenzi wa idara hiyo, Kanali Jimmy Said alisema, Taarifa ya Sunami inayosambaa mitandaoni si ya kweli.

Alisema walikuwa wanafanya mazoezi ya utayari kwa magari ya zimamoto na watu wa hatua mbalimbali wakichukua.

“Taarifa za Sunami zinapotolewa wananchi hawachukulii uzito hivyo leo tulikuwa tunaangalia kama wananchi watalichukuliaje hili jambo,” alisema Kanali Said.

Alisema wamejipima mambo mengi na kwamba kama kungekuwa na tishio hilo kituo cha mawasiliano na dharura kilichopo chini ya Waziri Mkuu idara ya maafa ndiyo inaratibu kutoa taarifa ya Sunami.
Advertisement
 
Back
Top Bottom