TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Ushauri huu uanaendelea...

Nashauri kwa negligence iliyofanywa na Jeshi letu la polisi kuhusu kadhia hii ya kifo cha Mzee Ali Mohamed Kibao, Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu , kukutwa ameuwawa na mwili wake kutupwa eneo la Kunduchi Ununio,

watu wanne wawajibike!.

1. Waziri - kwa ajali kazini

2. IGP - kwa negligence ya RPC wake

3. RPC -DSM - negligence

4. OCD Kinondoni - negligence, na hawa wawili wa mwisho RPC na OCD wanaweza kufikishwa kwa Pilato!.

Ni wakati sasa Rais Samia kukasirika kama enzi za Nyerere!.

P
 
Enzi hizo
 
Hata kama hao uliowataja watajiuzuru nyadhifa zao bado haitasaidia kitu, utekaji bado utaendelea kama kawaida
 
huu ni uthibitisho wanaofanya vitendo hivyo ni watu wasiojulikana。
p
 
Kwa sasa nakataa tiss kuna zaid ya Tis
 
Kwa sasa nakataa tiss kuna zaid ya Tis
Sasa hivi ukiwa Kariakoo watembea huku ukiangalia begani kujilinda na Noah yoyote itayopita karibu yako kwa kuhofia kutekwa.

Upo uwezekano wa kuwepo paramilitary force chini ya ex- senior army officer au former agents ambao wamezuiwa kupata na pengine huko kuna tensions zinopelekea kuwepo mgawanyiko kati ya watiifu na wale wahuni

Pili, yawezekana kuna kikosi maalum ambacho kipo detached na vyombo halali na hufanya kazi ziitwazo ad- hoc yaani hawana kinga ya kisheria wala hawawezi kuwajibishwa na yoyote akiwemo sponsor wao.

Tatu, mercenaries waweza kuwa ni sehemu ya mfumo huo ambao upo kwa muda mrefu na hawa hawawezi kujulikana maana mawasiliano nao ni simu tu kupata maagizo na kutekeleza kazi.

Nne, kama kumbukumbu zenu zipo sawa basi mtakumbuka watoto wa mitaani (wa miaka ya 1980-90s) ambao baadhi ni watu wazima sasa na wamo kwenye mfumo, hivyo nirahisi kutafuta na ku-organize contacts kwa ajili ya shuguli za utekaji na mengine.

Tano, wapo wahamiaji haramu ambao huweza kutumika kwa kazi zote chafu.

Hayo yote niloyataja hapo juu hayawezi kujitokeza katika nchi yenye mfumo imara wa ulinzi na usalama na wakawa wadunda tu mitaani na Noah kutafuta targets zao kama bwana Bonge kule Kiluvya.

Serikali itakuwa ilipata ripoti iloshiba (baada ya tukio la Ali Kibao) na ni lazima hao wasojulikana wana nguvu kubwa nyuma yao inozuia kuwafanya kuwa exposed na kufikishwa mbele ya sheria.

Hii yote chanzo chake nimekiongelea mara nyingi humu, Kleptokrasia.

Huu ni mfumo hatari sana kwa sasa kwa usalama wa taifa na raia wake na umejikita kiasi cha kila mtanzania kujionea wenyewe kwani ukiangalia Chadema, hawapigi kelele za bure.
 
Kwanini idara isiingilie kati kukomesha jambo hilo ambalo limekuwa mtihani kwa wanachi na wao Ndiyo wenye dhamana kikatiba ??
Tanzania tuna majeshi makubwa matatu na ndani yake kuna majeshi madogo madogo mengi。

Majeshi makubwa ni
  1. JWTZ- (TPDF)chini ya CDF - kulinda usalama wa nchi na mipaka yetu。 Chini yake kuna JKT,Anga,Marine
  2. Polisi -(PT)chini ya IGP- kulinda usalama wa raia na mali zake。 Chini yake kuna Trafiki
  3. Usalama wa Taifa (TISS)chini ya DGIS - kulinda usalama wa serikali na viongozi wake。Chini yake kuna GSU na PSU
kisha kuna majeshi madogo 4 chini ya ma Kamishna
  1. Magereza - wafungwa
  2. Uhamiaji
  3. Zimamoto na uokoaji
  4. Madawa ya kulevya
chini ya hapo uanafuata majeshi USU, para military
wakiongozwa na
  • Mgambo
  • KMKM
  • Wanyamapori
  • Makampuni ya ulinzi
P
 
Naomba nikurerekebishe tu, technicaly TISS sio jeshi, ni organization yenye paramilitary elements ndani yake. Hawa qualify na hawatambuliki kama jeshi just intelligence organization
Polisi sio jeshi, ni paramilitary organization.

So kwenye upangaji wako, unatakiwa utambue jeshi pekee nchi hii ni TPDF only, hayo mengine yana belong to paramilitary organization
Police, uhifadhi ( ambao walikuwepo miaka mingi ila kisheria tu ndio walikuwa hawana muunganiko), uhamiaji, zimamoto,magereza

Madawa DCEA, hawa nao si jeshi, similar to TISS , japo wana kazi ya tofauti. Ni organization si jeshi

Mgambo na KMKM hao ni division ndogo za TPDF , KMKM wana belong upande wa zanzibar so si majeshi yanayo jitegemea
 
Kumbe TISS ni wapo kwaajili ya usalama wa Serikali na Viongozi wake tu ??
🙆‍♂️🤦‍♀️😭
Sikujua ! 👌👌
Kwanini inaitwa Usalama wa Taifa sasa badala ya kutambulika kama usalama wa Serikali na Viongozi wake ili kueleweka vizuri ??
 
Kwa hili tishio la usalama wa Tundu Lissu aliloshikwa sikio kuwa kuna njama zinapangwa kumshughulikia Tundu Lissu afunguka A-Z wasiojulikana kutaka kumuumiza!
kama ni kweli njama hizo zilikuwepo ila sasa hazita tekelezwa tena kwasababu tayari zimeisha kuwa exposed

Then hoja za bandiko hili bado zina sadifu!。
P
 
Back in days when Advocate P alikuwa critical thinker.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…