TISS na CCM Party Comrades tumieni kesi ya Mbeya kuokoa Umoja wetu, na Muungano wetu, kuilinda CCM. FUTA IGA

TISS na CCM Party Comrades tumieni kesi ya Mbeya kuokoa Umoja wetu, na Muungano wetu, kuilinda CCM. FUTA IGA

Asalam,
Nimefuatilia mijadala ya huu mkataba wa kuuza Bandari. Mengi yamesemwa. Sitaki kuyarudia, Natoa ushauri tu sasa ili kulinda umoja wetu kama watanzania, muungano wetu na uimara wa CCM.
1. Vyombo na mifumo ya dola iwasaidie Majaji Mbeya KUFUTA HUU MKATABA bila kujali changamoto za dini zao, udhaifu wa utetezi hapa na pale, etc.
2. CCM itokee hapo sasa kurekebisha mambo na kurudisha mpira kapuni kwa kauli nzito majukwaaani kuwa TUNAHESHIMU MAAMUZI YA KIMAHAKAMA.

3. Suala la Bandari liachwe kwa muda lipoe hadi baada ya Uchaguzi 2025. Hapa ni kukipa chama tawala kupumua
4. Viongozi wa Dini na wale waheshimika ndani ya nchi watoke kupongeza haya maamuzi. Ili kujenga utulivu

5. Ilani ya Uchaguzi sasa irudi kujikita kwenye mipango na mwelekeo wa 2050. Yako mengi. Taifa liachane na udalali

6. CCM ianze kuheshimu na kuwatumia wataalamu nje ya mfumo kama TLS kupitia mikataba.
7. Tuvipe sasa uhuru vyombo kufanya kazi, mfano TPA, PPRA, TAKUKURU ETC wasogee kwenye usimamizi wa mambo mazito.

7. Tuendelee na miradi ya kipaumbele na kubotesha mahusiano na marafiki zetu wachina, warusi, Cuba, etc.

Kwa uchache. Lkn yako mengi ya kushauri mifumo. Tusigombane na wanaotukosoa.
we kafute kwanza huo ujinga wako
 
Nauhakika TISS watalisimamia hili ili kutuliza joto la kisiasa
Jeshi WTZ...TISS wamekula kiapo kulinda kutetea katiba ....kuna somo kwenye mafunzo yao....kumtoa hamna yyt ile mwanasiasa ....au Principal akienda kombo akawa hashauriki....kwa maslahi ya Taifa....nawasilisha
 
Jeshi WTZ...TISS wamekula kiapo kulinda kutetea katiba ....kuna somo kwenye mafunzo yao....kumtoa hamna yyt ile mwanasiasa ....au Principal akienda kombo akawa hashauriki....kwa maslahi ya Taifa....nawasilisha
Sawa
 
Unajua hata wanaotuongoza hawajui wanatumia nadharia au itikadi gani
Katiba yetu inatamka wazi Tz ni nchi ya kijamaa, ila kiuhalisia hatupo hivyo....tuna ubepari uchwari na ujamaa uchwara tu.
 
Back
Top Bottom