TISS na wasaidizi wengine wa Rais Samia, chukueni hili

TISS na wasaidizi wengine wa Rais Samia, chukueni hili

Mkuu naona unazunguuuka, we sema straight uwajibikaji, rushwa na ufisadi chini ya sa100 ndio habari ya mjini...acha maneno mingi!!!.
 
Kwa muda mfupi nimepata majibu mengi na mazuri. Wenye akili Sungwi au midomo kunuka wanaishia kutukana tu bila kuongeza au kukosoa kile nilichosema kwa wao kusema ambacho ni Bora au sahihi

hii ndiyo shida ya wavimba macho!! Ndugu yangu uliyesema TISS na CCM wapi na wapi! Unajua hao washauri wa Rais ni watu gani? Unajua hayo yanayotoka kwe umma hususani wakati huu ni ushauri wa akina nani?? Yako mengi ya kujifunza ngoja niishie hapo.

Vichwa Sungwi karibuni kwa mapovu zaidi
 
Shotocan. Kosoa kwa hoja au boresha unapoona hapatoshi. Matusi yana saidia Nini?
 
Kampeni gani tena jamani kwani kuna mshindani yeyote? Hizo hela mara 10 mngegawanyisha kila raia apate hata buku tena akanunue chochote anachotaka
 
Ni kweli. Kuna maboresho katika Idara mbalimbali lakini huduma ni za hovyo. Mfano nenda hospitalini, Kituo cha Afya, Zahanati hapa hakuna cha bure. Mpaka uingize mkono mfukoni. Gharama ya tiba ndo usiseme. Hakuna madawa. Nenda shuleni kuna maboresho. Walimu hakuna. Walimu hawafanyi kazi. Wengi ni waendesha bodaboda. Nenda kwenye barabara. Barabara nyingi huko vijijini sasa hivi hazipitiki. Hakuna matengenezo. Wakandarasi wamekimbia kazi. Muda mrefu hawalipwi. Nenda kwenye maji. Bado wananchi wanahangaikia maji. Mfano hai jana kwenye luninga wananchi wa hapo hapo Dar bado wanahangaikia maji. Wananchota maji kwenye madimbwi. Kwa huduma Tanzania bado sana.
 
Nani huyo
Rais anao wasaidizi waliosomea fani za Idara au Kitengo husika. Katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu japo Kampeni hazijaanza rasmi kwa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, lakini ukweli ni kwamba tupo busy na Kampeni. Ukizunguka huku na kule utaona mapikipiki, khanga, baiskeli nk.

Hivi karibuni tunaona Kampeni zimehamia kwenye vyombo vya habari kama vile mitandao ya Kijamii. Kila uchao utaona maandishi, "Mkoa fulani Rais Samia kaongeza bilioni kadhaa kwenye sekta fulani kutoka bilioni kadhaa zilizokuwepo miaka minne iliyopita.

Ni jambo jema kwa wasaidizi hao wa Rais kufanya yote hayo. Pamoja na hayo wasaidizi hao walitakiwa kufanya counter check au follow up ili kujua Kampeni hizo zinapokelewaje na wananchi hasa wa kawaida.

Si jambo la siri kuwa pamoja na maboresho katika sekta zinazosemwa kuwa zimeboreshwa, bado wananchi wanapoenda kupata huduma katika maeneo husika wanakumbana na changamoto lukuki zaidi ya ilivyokuwa kabla ya maboresho yaliyofanywa na Rais Samia.

Kwa mfano unamwambia mtu hospitali ya Mkoa ilikuwa Ina CT Scan mbili miaka minne iliyopita leo Rais Samia kaongeza vifaa hivyo 400, kama mwananchi anaenda kupata huduma inayohusisha kifaa hicho Kuna kuwa na changamoto za njoo kesho, njoo kesho kutwa, njoo wiki ijayo, Hapo anaambiwa kijanja ajiongeze ( atoe rushwa a.k.a hela ya maji).

Mwananchi huyo ambaye hakuona changamoto hizo wakati ST Scan zilipokuwa mbili, unapomwambia leo Samia kaongeza ST Scan 400 anakuelewa??? Huu ni mfano mmoja tu.

Mtu akizungumza mema na mazuri yaliyofanywa na Serikali wakati wa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli,baadhi ya watu wa kawaida na hata wakubwa wanatoa mapovu. Lakini ukweli ni kwamba Samia na Magufuli wakati ule walifanya kazi kubwa ndani ya muda mfupi. Uwajibikaji Serikalini uliimarika kwa kiwango kikubwa mno. Mambo ya njoo kesho mara wiki ijayo kauli za kuchochea mazingira ya rushwa yalipungua mno. Leo nenda maofisini uone, nenda Polisi uone, nenda Mahospitalini uone. Wananchi wa kawaida tunajua yanayoendelea huko.

Serikali ya Rais Samia imetekeleza hayo, sawa vema, swali ni kwamba kama mwananchi wa kawaida hapati huduma Bora, kwa wakati na bila mizengwe, maboresho hayo yana msaidia Nini? Kampeni hiyo inamsaidia Nini Rais Samia??

TISS, TAKUKURU na Idara nyingine za Serikali mpo, huo ni wajibu wenu tunawalipa kwa Kodi zetu. Msaidieni Mheshimiwa Rais.
mwingie anayefanya kampeni zaidi ya huyo aliyesambaza pikipiki na baiskeli zenye picha zake nchi nzima tangu mwaka 2023 yaani miaka mitatu kabla ya ratiba za kampeni yeye anaendelea na kempeni.
 
Nani huyo

mwingie anayefanya kampeni zaidi ya huyo aliyesambaza pikipiki na baiskeli zenye picha zake nchi nzima tangu mwaka 2023 yaani miaka mitatu kabla ya ratiba za kampeni yeye anaendelea na kempeni.

Mungu ni Mweza wa yote. tunaamini atafanya lolote wakati wowote.

novena iendelee.

unang'ang'ana kuongoza watu wasioukutaka. Unakiuka hata taratibu za chama chako, unajipatia nafasi ya kugombea kwa hila. huna haya wala aibu
 
Back
Top Bottom