TISS walibariki UJENZI wa GHOROFA linalotazama IKULU

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Na Happiness Katabazi

ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA,) Togolai Kimweri anayekabiliwa na mashtaka matano ya matumizi mabaya ya ofisi na mwenzake, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Taifa (TISS) Rashid Othman, Ikulu waliliridhia kwa maandishi ujenzi wa ghorofa 18 wa jengo linalotazamana na Ikulu.

Kimweri alitoa Maelezo hayo jana mbele ya hakimu Mkazi, Sundi Fimbo wakati alipokukua akiongozwa na Wakili Richard

Rweyongeza na Henri Masaba kutoa utetezi wake ambapo alieleza kuwa ni Idara hiyo ya Usalama wa Taifa (TISS) iliiomba TBA iwapatie ghorofa kwa ajili ya ofisi ya TISS.

Kimweri ambaye alidai mashitaka yote Dhidi yake ni ya uongo ,alidai kuwa ujenzi wa jengo hilo ulifuata taratibu zote na kwamba anahisi kushtakiwa kwake kumetokana na kashfa aliyowahi kuipata Waziri John Magufuri iliyowahi kulipotiwa katika vyombo vya habari.

Mshitakiwa huyo alidai jengo Hilo linaipatia serikali asilimia 25 na mwekezaji anapata asilimia 75 mwekezaji na kwamba hajawahi kutoa hati ya viwanja namba 45na 46 vilivyopo mtaa wa Chimara kwa mwekezaji ili apate mkopo.

"'Mashitaka Dhidi yangu ni ya uongo kwani hati ya jengo Hilo haijawai kutoka hadi sasa ipo TBA na kwamba iwapo viwanja hivyo vingeuzwa wakati huo vingeuzwa kwa Sh 1.30 bilioni na sasa thamani hiyo inazidi Sh 9.8 bilioni.

“Jengo hilo lilikuwa na manufaa sababu liliipatia serikali ongezeko mara tano, mawaziri wanne wanaishi ndani ya jingo hilo akiwamo Meya wa jiji la Dar es Salaam pamoja na wajumbe wa tume ya Katiba ambao wanalipa kiasi cha Dola za Kimareksni 2,500 ambapo kwa mwezi ni Dola za kimarekani 70,000 na kwa mwaka ni Dola za kimarekani 800,000,” alidai Kimweri.

Alidai kuwa wakati ujenzi wa jengo hilo ulipofikia gorofa ya 15, aliwasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Idara ya Usalama wa Taifa na TBA ikampelekea machozi wa jengo Hilo ambao aliupitia na kuwataka waendelee hadi gorofa ya 18 kama ilivyopangwa ila sehemu ya Juu wapewe idara ya Usalama wa Taifa.

Kimweri alidai baadaye walipokea barua toka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Philimon Luhanjo ambaye kwa sasa a estate ikizungumzka kuhusu makubaliano hayo na kwamba hajawahi kupata malalamiko yoyote kuhusiana na ujenzi huo.

“Rais alipewa taarifa ya utendaji wa TBA kuhusu mradi huo na kamba katika vikao vya bajeti vya bunge vya 2007/2008 na 2008/2009 mradi huo ulitolewa taarifa zake bungeni katika hotuba ya John Magufuli na Shukuru Kawambwa.”Alidai mshitakiwa huo.

Alisisitiza kuwa taarifa zote kuhusu mradi huo zilikuwa zikitolewa Wizarani, yeye hakuwa mjumbe wa bodi, bodi ndiyo ilikuwa na uwezo wa kuupitisha huo mradi ama kuukataa na kwamba wazo lilikuwa mradi wa ujenzi wa gorofa sita lakini rasimu ya mkataba iliandaliwa na kupelekwa kwa Mwanasheria mkuu wa serikali Pamoja na mkataba unazungumzia gorofa 15 hadi 25.

Aliiomba mahakama kuifuta kesi hiyo na mashtaka yanayowakabili yeye na mwenzake kwa sababu alikuwa akihakikisha anafanya kazi kulingana na maelekezo ya sharia ya wakala.
Mbali na Mkurugenzi Mkuu wa TBA, Kimweri mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Msanifu Mkuu wake, Richard Maliyaga.

Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Leonard Swai, ukitoa ushahidi katika kesi hiyo, uliwaita jumla ya mashahidi 13 pamoja na vielelezo 20 na baada ya mashahidi hao kutoa ushahidi wao mahakama iliwaona washtakiwa wote wana kesi ya kujibu na kuwataka kuanza kujitetea.

Washtakiwa Kimweri na Maliyaga wanakabiliwa na mashitaka matano ya matumizi mabaya ya ofisi katika utoaji kibali cha ujenzi wa jengo la ghorofa 15 kiwanja namba 45 mtaa wa Chimara.

Swai akiwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao, alidai kuwa Agosti 6, mwaka 2007, mikataba miwili kwa ajili ya viwanja namba 45 na 46 washtakiwa hao waliitia saini. Alidai kuwa katika mkataba huo, upande wa serikali watamiliki asilimia 25 na mwekezaji asilimia 75 katika jengo la ghorofa 18. Alidai TBA ilitoa vibali vilivyotiwa saini na Maliyaga, kikiwemo cha kuongeza idadi ya ghorofa 15 hadi 18.

Wakili huyo wa TAKUKURU alidai kuwa eneo hilo lilikuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa gharofa tatu hadi sita kwa makazi na kwamba washtakiwa hao walitoa kibali kwa mwekezaji bilaya kupata idhidi kutoka kwa mamlaka husika.

Source: Tanzania Daima
 
huyu aliyempa kibali itakuwa alielekeza kivingine yeye kafanya kivingine.
 
huyu aliyempa kibali itakuwa alielekeza kivingine yeye kafanya kivingine.

sure Mkuu, huyu Mkurugenzi wa TBA atakuwa aliingizwa chaka. sidhani kama hata huyo Othman aliwahi kuonana naye ana kwa ana labda kwenye picha tu
 
mbaazi ikikosa maua lazima isingizie jua, hawa wahuni wamevunja sheria za nchi kwa kujenga jengo kinyume cha sheria wanaanza kutafuta mchawi, hilo jengo libomolewe na wahusika wafikishwe mahakamani
 
Hili ni jengo refu ,linaitazama Ikulu kwa chini, Tiss wanawajibu wa kufanya surveillance kwa kila jambo karibu na Ikulu. Ningeshangaa kama Tiss was ingekuwa wamehusika

kwani kuna majengo mangapi marefu yamejengwa na hayana vibali vya TISS? kwani sheria inasemaje kuhusu ujenzi karibu na ikulu?
 
hilo jengo serikali inabidi ilinunue tu na hamna ujanja tena.
 
Hili ni jengo refu ,linaitazama Ikulu kwa chini, Tiss wanawajibu wa kufanya surveillance kwa kila jambo karibu na Ikulu. Ningeshangaa kama Tiss was ingekuwa wamehusika

mkuu nisaidie kwani TISS wanashughurikia ujenzi wa majumba au ulinzi na usalama wa taifa hili.
 
kwani kuna majengo mangapi marefu yamejengwa na hayana vibali vya TISS? kwani sheria inasemaje kuhusu ujenzi karibu na ikulu?
Huwezi kujenga jirani na Ikulu jengo ambalo halijulikani nini matumizi yake, Tiss hawawezi kukaa kimya na kuangalia , hakuna jengo refu katiba na Ikulu kama hilo, na hata wamarekani wa Obama walipo kuja walipaswa na hofu sana na jengo hilo lilifungwa kwa wiki nzima , jengo ukikaa juu unamuona Rais wakati akifanya mazoezini ya kukimbia kwenye eneo la Ikulu , hii umeomba wapi?
 
kwani kuna majengo mangapi marefu yamejengwa na hayana vibali vya TISS? kwani sheria inasemaje kuhusu ujenzi karibu na ikulu?

Taasisi ya Mwalimu Nyerere ilizuiwa na TISS kujenga kitega uchumi maeneo hayohayo na kuamriwa wakajenge kwingine (next na Avalon house). Ni jukumu la TISS kuhakikisha usalama wa Ikulu
 
kwani kuna majengo mangapi marefu yamejengwa na hayana vibali vya TISS? kwani sheria inasemaje kuhusu ujenzi karibu na ikulu?

mimi kunakitu sijaelewa kwani TISS inahusikaje na majengo huyu jamaa kachanganyikiwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…