Na Happiness Katabazi
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA,) Togolai Kimweri anayekabiliwa na mashtaka matano ya matumizi mabaya ya ofisi na mwenzake, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Taifa (TISS) Rashid Othman, Ikulu waliliridhia kwa maandishi ujenzi wa ghorofa 18 wa jengo linalotazamana na Ikulu.
Kimweri alitoa Maelezo hayo jana mbele ya hakimu Mkazi, Sundi Fimbo wakati alipokukua akiongozwa na Wakili Richard
Rweyongeza na Henri Masaba kutoa utetezi wake ambapo alieleza kuwa ni Idara hiyo ya Usalama wa Taifa (TISS) iliiomba TBA iwapatie ghorofa kwa ajili ya ofisi ya TISS.