Titles za degree za bongo zinatisha na zina maneno mazito ila ndani ya vichwa vya waliosoma hamna kitu, msitishwe na titles

deblabant

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2022
Posts
2,650
Reaction score
4,065
Kuna midigree inatisha ukisikia mpaka unajiuliza huyu mtu kweli namvyomjua ni kilaza hivi amewezaje kuviweka kichwani. Kumbe ukianza kuongea naye hamna kitu ila Cheti chake kinatisha.

Mfano banking na financial services, sijui highway engineering sijui educational policies and planing etc. Wengi wao waliosoma kichwani hamna kitu kabisa lakini wamegraduate Sasa sijui huko vyuoni wanasomea kweli au wanaenda kuchukua hiyo madigrii.
 
Hakuna elimu nzuri kama kufikiri vizuri.
 
Kuna ndugu yangu hupenda kuniambia......

ELIMU NI ILE INAYO BAKIA KICHWANI
Baada ya ku graduate πŸŽ“
πŸ€“πŸ€“πŸ˜ŠπŸ˜ŠπŸ˜Š
 
Hata vyuo vinavyotoa hizo digrii vinatofautiana hadhi. Muhimu kuangalia huyo mwenye digrii kasoma chuo gani.
 
Hahah kawaida hiyo afu ndo wanapewaga vyeo kina kina riz1🀣🀣
 
Mkuu, siyo kwamba wewe ndiye mwenye shida!? Inawezekana wao wanaongea madini tupu kuhusiana na maeneo yao ya kitaalamu waliyoyasomea, na wewe unashindwa kabisa kuwaelewa ama hata kutambua kidogo mantiki zilizopo nyuma ya kauli zao.

Labda kitu kimoja tu naweza kukuuliza, vipi maisha yao ya ujumla yanaendana na elimu zao? Mathalani, wanaishi katika makazi mazuri, watoto wanasoma shule zenye hadhi, wanamiliki magari kwa ajili ya usafiri binafsi, wanatibiwa katika hospitali zenye hadhi, wanajitoa kwa michango mikubwa katika shughuli za kijamii, n.k.

Kama majibu kwa yote ni ndiyo, na wewe unaishi kibabaishaji na tena kwa kupigika, basi tambua tathimini yako si ya kuaminika, bali unawaonea wivu tu. Kama hutajichunga muda si mrefu atageuka kuwa mchawi ili upambane nao kwa kupitia nguvu za giza.

Hakuna njia ya mkato katika maisha ndugu, rudi shule uende ukasome tu ndugu ili uweze kufanana nao. Wivu ni mzuri lakini uwe wa maendeleo, vinginevyo utawachukia watu bila ya kuwa na sababu zozote zile za msingi.
 
Chuo sio kigezo ni mtu mwenyewe...
Big no. Hata manchi yaliyoendelea yana vyuo wenyewe wanaita ni elite, na sifa za kujiunga na vyuo hivyo ni tofauti na mavyuo mengine ya ovyo ovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…