Kuna midigree inatisha ukisikia mpaka unajiuliza huyu mtu kweli namvyomjua ni kilaza hivi amewezaje kuviweka kichwani. Kumbe ukianza kuongea naye hamna kitu ila Cheri chake kinatisha.
Mfano bankink na financial services, sijui highway engineering sijui educational policies and planing etc. Wengi wao waliosoma kichwani hamna kitu kabisa lakini wamegraduate Sasa sijui huko vyuoni wanasomea kweli au wanaenda kuchukua hiyo modigrii.
Mkuu, siyo kwamba wewe ndiye mwenye shida!? Inawezekana wao wanaongea madini tupu kuhusiana na maeneo yao ya kitaalamu waliyoyasomea, na wewe unashindwa kabisa kuwaelewa ama hata kutambua kidogo mantiki zilizopo nyuma ya kauli zao.
Labda kitu kimoja tu naweza kukuuliza, vipi maisha yao ya ujumla yanaendana na elimu zao? Mathalani, wanaishi katika makazi mazuri, watoto wanasoma shule zenye hadhi, wanamiliki magari kwa ajili ya usafiri binafsi, wanatibiwa katika hospitali zenye hadhi, wanajitoa kwa michango mikubwa katika shughuli za kijamii, n.k.
Kama majibu kwa yote ni ndiyo, na wewe unaishi kibabaishaji na tena kwa kupigika, basi tambua tathimini yako si ya kuaminika, bali unawaonea wivu tu. Kama hutajichunga muda si mrefu atageuka kuwa mchawi ili upambane nao kwa kupitia nguvu za giza.
Hakuna njia ya mkato katika maisha ndugu, rudi shule uende ukasome tu ndugu ili uweze kufanana nao. Wivu ni mzuri lakini uwe wa maendeleo, vinginevyo utawachukia watu bila ya kuwa na sababu zozote zile za msingi.