Tito Magoti na Theodory Giyan wafikishwa Mahakamani, wafunguliwa mashtaka 3 yakiwemo ya Uhujumu Uchumi na Utakatishaji Fedha

Tito Magoti na Theodory Giyan wafikishwa Mahakamani, wafunguliwa mashtaka 3 yakiwemo ya Uhujumu Uchumi na Utakatishaji Fedha

Haka kaneno ka 'kiswahili kitarafa' hapo mwanzoni kalianza kama mzaha!

Lakini leo umekuwa ni msamiati rasmi utumiwao kusoteshea watu magerezani bila ya dhamana!

Hata hivyo sasa lingetumiwa kwa mfano wenye maana halisi!

Suala la 'fojari' unalisukuna kwenye utakatishaji ili tu huyo raia akose dhamana, kudadadek!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio fresh kabisa....
wanaowaandalia wenzao mashtaka ya namna hii nafsi zao zitawasuta.....
washtakini watu kwa haki.....
usimuonee mtu....
wala usimuogope mtu...
Nyie in type za watu hamjawahi kufika polisi au hospitali za kiafrika na issue serious. Ukisikia uswahilini watu wanabambikiwa kesi usidhani ni utani, ukisikia watu wanakufa mahospitalini kwa uzembe usidhani ni story. Ukiwa Afrika unaishi kwa kubahatisha haupo salama kama unavyodhani. Hao polisi, dokta na manesi hawajali kuhusu utu wako na roho zao haziwasuti.
 
Yaani katika maelezo yote ya mshtaka siajona kosa ni lipi hasa, hiyo programme inaitwaje?
 

Afisa wa LHRC, Tito Magoti pamoja na mwenzake (kama wanavyoonekana pichani) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mchana huu

Hata hivyo bado haijafahamika wamefikishwa Mahakamani hapo kwa tuhuma gani

Tito Magoti pamoja na wenzake walitoweka siku 4 zilizopita kabla ya Polisi kujitokeza na kueleza kuwa waliwakamata na kuwashikilia.

====
UPDATE:

View attachment 1302260

View attachment 1302258View attachment 1302259
Magoti apandishwa kizimbani kwa Uhujumu Uchumi

Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo la kutakatsha pesa shilingi Milioni 17.

Katika shitaka hilo Magoti amejumuishwa na wenzake Mtaalam wa Masuala Mtandao wa LHRC Theodory Giyan, ambao wote mnamo February Mosi na Disemba 17 wanatajwa kumiliki Program za Kompyuta na baadaye kujipatika Milioni 17 ambazo si zao.

Shtaka linamkabili na Magoti na Giyani ni kuwa sehemu ya Mtandao wa kiuhalifu, pamoja na kumiliki Mtandao wa Kompyuta uliotengenzwa kwa ajili ya kufanya uhalifu.

Hakimu anayesimamia Kesi ya Magoti na Wenzake ni Janeth Mtega ambapo kesi hiyo sasa imesogezwa mbele hadi January 7, 2020 huku washtakiwa hao wakirejeshwa rumande kutokana na aina ya makosa wanayoshtakiwa kukosa dhamana.

Magoti alikamatwa Ijumaa la Disemba 20, akiwa maeneo ya Mwenge jijini Dar es salaam huku siku chache baadaye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam akithibitisha kuwa Jeshi hilo kumshikilia Tito Magoti lakini bila kueleza sababu yake.
Taaarifa za chini ya kapeti zinasema kuwa walikuwa wanaenda kupotezwa wazima wazima, kilichowaokoa ni Dereva aliye mpeleka Tito had kwa hao watekaji alipomfikisha tu waliompokea mmoja wao anafahamiana na huyo Dereva aliempeleka Tito na wakaanza kufanya Kazi Ya ziada kutaka kujua Kama Yule Dereva anamjua Tito wakakuta Yule Dereva anamfaham Tito na anamfaham mmoja wa watekaji, hivyo ikabidi watekaji na uongozi wao wajadiliane Kwa kina Kwa muda wa Siku Tatu ndipo wakaaamua kuwakabidhi Kwa mambo sasa baada ya kuona Hakuna jinsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwami anawapoteza watoto wa watu, aende sasa kumtetea mahakamani.

Vijana msipende kutumika na wanasiasa wa fursa dizaini ya hakina Mwami

Kigogo soon atajulikana, serikali ina mkono mrefu sio awa vijana badala ya kujiingiza kwenye shughuli za kujiongezea kipato wamekuwa wanatumika na wanasiasa fursa.

Pole sana madogo mkiwa NONDO lazima kuna kitu cha kujifunza hapa,kwamba walikuwa wakiwatumia wengi wao ni WANAFIKI na WAOGA.
 
Utii bila shuruti. Tii mamlaka ya nchi hususani mwenye mamlaka akisema hapendi kitu Fulani[emoji41]acha usifanye. Hutagombana na mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nchi sio mali ya mtu, nchi haiendeshwi kwa misingi ya mamlaka inapenda nini?
Bali kwa katiba na sheria za nchi, hata mamlaka yanaweza kuvunja katiba na sheria za nchi.

Na kama nchi zingekuwa zinafanya kile mamlaka zinavyotaka pansingekuwa na uchaguzi, katiba wala sheria maana mamlaka hizo hizo hazipendi baadhi ya sheria na vifungu vya katiba.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom