Uchaguzi 2020 TLP na UDP zajiondoa kumpigia debe Magufuli

Uchaguzi 2020 TLP na UDP zajiondoa kumpigia debe Magufuli

Waandishi wa habari na title za kuuza magazeti.
 
WAMECHEMKA! TLP WALITANGAZA KUMUUNGA MKONO MAGUFULI KWENYE MKUTANO WAO MKUU UNAOTAMBULIWA NA KATINBA, WALIMWALIKA NA POLEPOLE, NA MKUTANO ULE UNATAMBULIWA NA MSAJILI, NA INAWEZEKANA NA MSAJILI AU MWAKILISHI WAKE ALIKUWEPO! HAYO ANAYOYASEMA KWAMBA TLP WALIONYWA WAKATII YAMEFANYIKA LINI TENA?
 
Nimeitoa mahali, samahani kwa kutomtaja mwandishi!

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imesema vyama vya Tanzania Labour (TLP) na United Democratic (UDP) ambavyo vilitangaza kumuunga mkono mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli, vilisitisha mpango huo kwa sababu vilikuwa havijafuata kanuni na sheria za uchaguzi.

[https://res]

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sity Nyahoza, alisema hayo jana wakati akihojiwa na Radio One kwenye kipindi cha Kumepambazuka.

Mapema mwaka huu, Mwenyekiti wa Taifa wa TLP, Augustino Mrema, na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, kwa nyakati tofauti, walitangaza kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, vyama vyao havitaweka wagombea urais badala yake vitamuunga mkono mgombea wa CCM.

Hata hivyo, Nyahoza jana alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, viko vyama ambavyo vilishawahi kupewa onyo na vikarekebishika.

"Mfano kuna Chama cha UDP na TLP walitangazaga kwamba wanamuunga mkono mgombea wa CCM, tukawaambia kuna utaratibu wake, hivyo hamjafuata inabidi mfuate. Wakaona hawajafuata utaratibu ikabidi wakae kimya, sasa hivi unawasikia tena?" Alihoji.

Alisema hivi sasa UDP baada ya kuelezwa walielewa na wanaendelea na kazi zao za kampeni na wana wagombea wao ambao wanaendelea kutangaza sera za chama chao.

Nyahoza alisema TLP kwa upande wake kiliweka hadi na bango na baada ya kuelezwa hakijafuata utaratibu, kiliyatoa sasa wanaendelea na kampeni zao.

"Kwa hiyo vyama ni sikivu, vile ambavyo siyo sikivu wawe wasikivu na kuzingatia sheria na kanuni maana kama mgombea wa chama chako msipokuwa wasikivu ukishinda kwenye uchaguzi itakuwaje," alisema.

Aidha, Nyahoza alisema vyama lazima vitambue kuwa kama huna amani na utulivu huwezi kuwa na uchaguzi.

"Unapokaa jukwaani ukaongea ukanadi sera yako au hata ukaongea mambo yako yawe ya ovyo au ya msingi ujuwe unaongea sababu kuna amani, huwezi kwenda kukaa sehemu risasi zinapigwa, vurugu watu wanafukuzana utapataje muda wa kukaa," alisema.

Aliongeza kuwa msajili wa vyama vya siasa ambaye kisheria ndiye msimamizi na mlezi wa vyama vyote vya siasa, ataendelea kuvishauri na kuvionya vile ambavyo vinakiuka sheria na kanuni.

"Msajili ni mlezi wa vyama vya siasa hivyo inapotokea mtu amekiuka sheria taratibu kwenye kampeni wajibu wake kama mlezi ni kumuonya kwamba unachofanya siyo sahihi, akiendelea kufanya unamuonya tena si unajua mambo ya ulezi tena na ndiyo maana unaona tunawaandikiaga barua sana vyama vya siasa vile ambavyo vinakiuka taratibu na sheria," alisema.

My take:
Hii inaonesha jinsi gani wanavyotapatapa! Wamekuja kuhalalisha ujinga wao baada ya CHADEMA na ACT-wazalendo kuwabana kuhusu ushirikiano wa Mrema, Cheyo na Magufuli! Msajili aache double standards!
 
Huku vunjo mabango makubwa ya mrema yamebandikwa picha za magufuli yaqni kushoto magufuli na mrema kuli. Tangu tumeanza kampeni hadi leo. Je tume ilishamwita au kumpa onyo mrema au sisem? Tuache double standard asei
 
Ila siasa ya nchi hii imejaa sanaa na maigizo, sijui kama ccm itakaa itoke madarakani kama wapinzani wenyewe ndio hawa.
 
Duu ! Hivi kuna watu bado wanateseka sana na urafiki wa CHADEMA na ACT Wazalendo? Najiuliza Je, ingekuwa vimeungana vyama vyote vya upinzani hali ingekuwaje?
 
Hizi ndo akili matope za kina mrema na cheyo
 
Kwahio wengine wanakatazwa kwa siri pasipo wananchi kujua, ile wengine wanakatazwa kwa makelele hadi kiziwi anasikia.

Hii Tume na yenyewe ingetangaza tu ilani yao sababu nao ni wagombea na sio wasimamizi kwa haya wanayoyafanya kwakweli hayafai.
 
Baada ya CHADEMA na ACT kuunganisha nguvu
Ofisi ya Msajili wa Vyama inavunja katiba ya nchi.

Katiba ya nchi inaruhusu watu, na kwa hivyo vyama, kuamua wanataka kuongozwa na nani.

Hii ni haki ya kimsingi ya kikatiba ambayo ukiiwekea sheria dhidi yake, sheria hiyo inakuwa batili, kwa sababu sheria itaenda kinyume cha katiba.

Ofisi ya Msajili inafanya hivi kwa kutahayari tu, baada ya habari za ushirikiano kati ya CHADEMA na ACT kushirikiana kupingwa.

Ni ujinga mtupu.
 
Kichekesho eti hawakufuata utaratibu kwan ata ungesema wamefuata utaratibu c tungejua wap sema umeona kule upande kule upande wa pili wameanza kuungana ivo unahofia msije mkashindwa kuthibit nch mnataka vyama vijitenge tukuelewe.
 
KIGOGO WA SERIKALI VS KABILA LA WAGOGO KAZINI YUPI NI YUPI

BORA MAENDELEO KARIBU ZINAWARUDISHA WAZUNGU, WACHINA, WASOUTH KOREA + ERROR TERM TWENDELEE KUCHAPA KAZI MTUMWA ITAKUWA MTUKISS

asa jailer - Bing video

Mkuu samahani, hivi huwa unaoongea nini? Maana kila mahali naona unaandika neno ERROR TERM, au ndio msemo unaobamba huko mtaani kwenu, sasa umehasika na hilo neno naona unalileta humu jf. Sio watu wote humu jf wanajua misemo ya hamasa ya huko mtaani kwenu.
 
Kumsaidia nguvu ya chama na mafanikio ya chama no matunda ya ruzuku, unayomtuhumu nayo uongo m.kiti was Chama Bora zaidi Tanzania. Tunamshukuru kwa kutumia vizuri ruzuku.
Too late to little. Baada ya ACT Kusema watampigia jura Lissu.NEC walikuwa wapi siku zote
 
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imesema vyama vya Tanzania Labour (TLP) na United Democratic (UDP) ambavyo vilitangaza kumuunga mkono mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli, vilisitisha mpango huo kwa sababu vilikuwa havijafuata kanuni na sheria za uchaguzi.

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sity Nyahoza, alisema hayo jana wakati akihojiwa na Radio One kwenye kipindi cha Kumepambazuka.

Mapema mwaka huu, Mwenyekiti wa Taifa wa TLP, Augustino Mrema, na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, kwa nyakati tofauti, walitangaza kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, vyama vyao havitaweka wagombea urais badala yake vitamuunga mkono mgombea wa CCM...

Wangeweka mwisho pale: "kwa hisani ya Dkt. Manoti.

Wameshauriwa kufanya hivyo kumpa bwana manoti uwanja maana wa kufanya yake.

Asijidanye nguvu ya umma inamwangalia.
 
Back
Top Bottom