Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Kumekucha
Ndio maana serikali ilitumia gharama kubwa kuzuia mwamba asiwe Rais wa TLS
Ndio maana serikali ilitumia gharama kubwa kuzuia mwamba asiwe Rais wa TLS
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa nini.Hawana uwezo wa kuzuia
Huwezi kuhitimisha hoja bila tusi?Usiniulize maswali kama una uhalali au points sana au unajua sana, nyoko wewe
Mimi nipo nyuma kushotoNaelekea ukumbini
(LIVE VIDEO IPO CHINI)
Leo tarehe 5 Oktoba 2024, mawakili wote wa Tanzania bara, hasa wa jijini Dar es Salaam, wanakutana katika jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam, ili kujadili suala la utekwaji na upoteaji wa raia nchini Tanzania. Tukio hili la kitaifa linaandaliwa na Tanganyika Law Society (TLS) na limehudhuriwa na wanachama wa TLS pamoja na wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali.
Lengo kuu la kongamano hili ni kujadili hatua za kisheria, historia ya matukio haya, na mikakati ya kuzuia na kuwajibisha wahusika, sambamba na kuangalia namna ya kuwasaidia waathirika na familia zao.
Tukio hili ni la umuhimu mkubwa katika kulinda haki za binadamu na kupambana na vitendo vya upoteaji wa raia nchini.
Kongamano linaanza rasmi saa 9:00 asubuhi na litakuwa mubashara kupitia uzi huu pamoja na Wakili TV kwenye YouTube kwa wale ambao hawawezi kuhudhuria.
#WakoWapi #TLSSymposium #UtekwajiNaUpoteaji
Limeanza mkuu!Kongamano linaanza saa tisa asubuhi?
Kwa hiyo watu wapotee tuu!”Kama nchi, hakuna sheria inayoshughulikia upoteaji na utekwaji wa watu nchini” - Jaji mstaafu Makaramba
Hapa ndio penye shida kubwa“Tatizo kuu ni pamoja na kukataa tatizo lenyewe, serikali inakataa kuwa hakuna tatizo la watu kupotea ama kutekwa”
“Tanzania inatakiwa kuanzisha sheria mahususi kuhisiana na masuala ya upoteaji na utekwaji wa watu na kuhakikisha vitendo hivyo vinafanywa kosa kisheria”.
Jaji mstaafu - Makaramba
Kwa vile hawana uwezo wa kumzuia MunguKwa nini.
Mimi sijaelewa
Wanatengeneza mkakati au wanafundishana kwa slides?
Lakini wote hapo si Mawakili wasomi? Wanayajua hayo yote kuna haja gani ya kusomeshwa muda huu?ni kinyume na sheria kabla ya kuingia kwenye mkakati wa namna ya kudeal navyo.
Off point..!!!Yakiitishwa maandamano hujitokezi unamwachia Mwenyekiti wa Maisha Mbowe na mtoto wake ila vitu lainilaini kama hili Kongamano uko mstari wa mbele. Bibi Erythrocyte uwe unajitokeza hata kwenye maandamano anayoitisha Mwenyekiti wa Maisha Mbowe!
Ok karibu nikupe tibaHayakuhusu endelea na issue za uchawi.
Off point..!!!Yakiitishwa maandamano hujitokezi unamwachia Mwenyekiti wa Maisha Mbowe na mtoto wake ila vitu lainilaini kama hili Kongamano uko mstari wa mbele. Bibi Erythrocyte uwe unajitokeza hata kwenye maandamano anayoitisha Mwenyekiti wa Maisha Mbowe!
Ngoma inogilePatachimbika ,Ponda ndani ,mwamakula ndani ,pambalu ndani,muliro ndani.