Tanganyika Law Society muongozo wenu unanipa ukakasi Sana... Inamaanisha baada ya kifo Cha rais serikali yote inakoma?
Basi Makamu wa raisi aliendesha kikao Cha LEO Kimakosa maana aliendesha na Baraza ambalo limekwisha vunjika.
Nionavyo Mimi katiba yetu iliacha ombwe juu ya hii issue, ndio maana nchi nyingine wanaitisha uchaguzi ili kuunda serikali mpya.
Ninavyo sema hivi ninaona mbele yangu shida nyingi za kisheria, matharani uteuzi wa wabunge. Je wabunge walio ingia bungeni kwa tiketi ya raisi watatenguliwa ili Mama Samia akidhi takwa la kisheria la kuwa na nafasi 10?
TLs inaonaje hili ni awamu ya tano au awamu ya 6 ?
Karibuni kwa mtifuano