TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Ineeleweka vyema sana hongera TLS kwa kutimiza wajibu wenu.
Nadhan sasa nchi itasonga mbele kwenye nyanja ya kufuata katiba na sheria za nchi
 
Hapo hao wanasheria wameweka kifungu chochote kwamba rais akifa na balaza la mawaziri linakufa kweli? Kipo hicho kifungu?

Alafu kwa nini umepanic sana? Haya ni maisha tu hata nyie chadema mkijipanga iko siku mtashika madaraka labda 2300 huko

Yaani mimi kabisa ni wa kupanikishwa na ww, au unajitafutia umaarufu kupitia kwangu? Rais mpya akiapishwa baraza la mawaziri linakoma. Mimi sio mwanasheria, hivyo sina utaalamu wa kutaja vifungu kwa namba zake, ila ninaelewa kwa mantiki.
 
Mimi naona katiba yetu inakanganya sana..!, sasa kama hivi ndivyo mbona Rais leo alikuwa na kikao na hilo baraza la mawaziri?? Litaitwaje baraza la mawaziri na automatically wanapaswa kiteuliwa upya na kuapa ndio kuwe na mawaziri??
 
Yaani mimi kabisa ni wa kupanikishwa na ww, au unajitafutia umaarufu kupitia kwangu? Rais mpya akiapishwa baraza la mawaziri linakoma. Mimi sio mwanasheria, hivyo sina utaalamu wa kutaja vifungu kwa namba zake, ila ninaelewa kwa mantiki.

Muktadha wa Rais aliye madarakani anapofariki ndio unaozungumziwa hasa hapa sio kula kiapo tuuu bali kula kiapo iwapo Rais aliyoko madarakani amefariki na Vice wake kula kiapo kama Rais mteule! Naomba usichanganye mambo! Mjadala huu mtamu sana!

Mkuu weka vifungu vinavyo ongea kuhusu waziri mkuu na mawaziri na baraza lote tusi assume tafsiri za TLS weka vifungu!
 
Hawa TLS naona wanapuyanga tu!! Tatizo ukishajiona unajua sana mara zote lazima uharibu, hawa wanadhani sheria/katiba wanaijua sana kumbe wanapuyanga tu!!!

Kwanza uongozi wa SASA bado ni wa Serikali ya awamu ya Tano!! Si awamu ya Sita kama wengi wanavyodhani!

Mh: SSH ni Rais wa Sita lkn anaongoza Serikali ya awamu ya Tano ndio maana hata ilani anayoitumia haitabadilishwa!!!
 
Hawa TLS naona wanapuyanga tu!! Tatizo ukishajiona unajua sana mara zote lazima uharibu, hawa wanadhani sheria/katiba wanaijua sana kumbe wanapuyanga tu!!!

Kwanza uongozi wa SASA bado ni wa Serikali ya awamu ya Tano!! Si awamu ya Sita kama wengi wanavyodhani!

Mh: SSH ni Rais wa Sita lkn anaongoza Serikali ya awamu ya Tano ndio maana hata ilani anayoitumia haitabadilishwa!
 
Nikueleze vifungu mimi ni mwanasheria, kama ww ni mwanasheria nitajie kufungu kinachowalinda hao mawaziri.

Katiba iko kimya kuhusu waziri na baraza kwa muktadha unao ongelewa hapa na ndio maana hakuna kifungu kilicho vunjwa na kinacho toa ushauri wowote kwenye muktadha huu
 
Nitajie kifungu kinachoonyesha hayo majukumu inapotokea rais aliyeko madarakani akiwa amefariki. Watu wa TLS mje mtoe ufafanuzi wa hili suala la huyu Mheshimiwa.
Hiyo hapo
Screenshot_20210319-232218.jpg
 
Kwanini hivyo vipengele mnavyotaka vitumike ni kwa mawaziri tu wakati kuna wengi tu wameteuliwa na rais na kuapa mbele yake?

Kwa mantiki ya kawaida kabisa rais anapoapishwa anaunda serikali yake, na serikali ni mawaziri kwanza. Hao wengine anaendelea nao kadiri muda unavyoenda. Hata Magufuli alipoapishwa alianza kuteua mawaziri kwanza, kisha ndio alikuja kubadili katibu Mkuu Kiongozi, jaji Mkuu, IGP, CDF, wakuu wa mikoa, wilaya nk.

Hili halihitaji kujua sheria bali ni akili timamu na kuweza kupambanua mambo. Sasa ww unaleta ubishani ambao wala haukubebi bali unaonekana juha tu. Achana na hangover za siasa za uzalendo uchwara, hizi ni zama mpya na zina kitabu chake, unakwama wapi?
 
Nikafikiri unaweka vifungu kumbe unaleta ngonjera.

Mna shida sana nyie watu
 
Katiba iko kimya kuhusu waziri na baraza kwa muktadha unao ongelewa hapa na ndio maana hakuna kifungu kilicho vunjwa na kinacho toa ushauri wowote kwenye muktadha huu

Ndio maana nimewataka TLS wajitokeza kwenye huu uzi wao watupe udadavuzi wa kisheria katiba inasemaje. Mimi ni mjuzi wa fani nyingine, naweza kutoa maelezo kwa usahihi kwenye fani yangu. Ila mtaalamu wa sheria akitoa vifungu naweza kuelewa kwa mantiki akisemacho, lakini usitegemee mimi nikutajie sijui kufungu namba ngapi, na section sijui A au B.
 
Cha msingi serikali ya CCM haiwezi kupoteza muda wa kuwatumikia wananchi kufuata vitu visivyo na tija.Tukimaliza kuzika kazi zinaendelea na atakaye tukwamisha atumvumilii.
 
Sasa kikao cha BLM alichoongoza leo Mh Rais ni batili? Tanganyika Law Society
Utawala wa Huyu Rais haujakamilika kwa sababu hana makamu wa Rais ndiyo maana katiba inamtaka ndani ya siku 14 hawe ameteua makamu wa Rais. Hawezi vunja baraza kwa ssbabu inatakiwa ashauriane na makamu wake kuhusu waziri mkuu mpya hivyo baraza bado ni halali.
 
Mjadala huu mtamu sana watu wanauliza vifungu kwenye katiba vinavyosema kuhusu waziri mkuu Rais aliye madarakani anapo fariki!

TLS hoja zao zinazua maswali sana na ni assumptions tuu!
Maana kuna maana kubwa kama kwenye muktadha husika katiba inaponyamaza kuhusu waziri mkuu!

Mbona kwa Vice iko wazi kabisa? Hata kama katiba yetu ina mapungufu wasingeliweza sahau swala la PM kama kweli linahitaji kwenye muktadha tulionao!

Kuna maana kubwa sana katiba kutosema chochote kuhusu PM!

Mimi niko hapa nafatilia uzi huu nipewe vifungu.
Kama kinacho ongeleka kitaa juu ya ushupavu wa JW, ni kweli, basi jeshi libarikiwe sana.

kwa muktadha huo, na kwa tamko hili la tls lenye amri ndani yake, naamini wameamua kumsaidia bega kwa bega mama. naona green buttons moja baada ingine ikiguswa kwa tz nzuri, ambayo haina kunguni na papasi waliojijengea mirija ya kunyonya via fulani.

leo inashangaza mtu anahoji kifungu gani kina tumika ili mama aanze na wateule wake, lakn alikuwa ahoji kwann sheria ya ukomo wa urais ambayo ipo kikatiba, inataka ivunjwe.

kama kulikuwa na maarifa ya kuweza kumwongezea mtu muda wa kutawala milele, maarifa hayo hayo yatumike ili mama achague wa kumsaidie na waape kwake.
 
Hoja ya TLS ina mantiki kubwa.

Rais lazima 'ateue' na kisha kutaka 'wateuliwa' wale kiapo kwake na kwa serikali yake.

Kwa muktadha huo ni dhahiri kwa sasa hakuna baraza la mawaziri 'halali'.

Maana inabidi Rais apendekeze jina la waziri Mkuu, alipeleke mbele ya Bunge apitishwe na kisha waziri Mkuu huyo afike mbele ya Rais kula kiapo cha kumtumikia Rais na baadaye washauriane 'kuunda' baraza la mawaziri ambao pia watatakiwa mawaziri hao kula kiapo cha utii kwa Rais.

Maana yake baraza hilo tuliloliona leo tarehe 19 March 2021 ktk 'kikao' cha 'baraza' la mawaziri ni la mpito tu, lazima utaratibu wa kikatiba wa kuteuliwa na kuapa utii kwa Rais mpya ufuatwe.

Back
Top Bottom