Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo hao wanasheria wameweka kifungu chochote kwamba rais akifa na balaza la mawaziri linakufa kweli? Kipo hicho kifungu?
Alafu kwa nini umepanic sana? Haya ni maisha tu hata nyie chadema mkijipanga iko siku mtashika madaraka labda 2300 huko
We katiba ishasema baraza la mawaziri linavunjika pale raisi mpya anapokula kiapo.
Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Yaani mimi kabisa ni wa kupanikishwa na ww, au unajitafutia umaarufu kupitia kwangu? Rais mpya akiapishwa baraza la mawaziri linakoma. Mimi sio mwanasheria, hivyo sina utaalamu wa kutaja vifungu kwa namba zake, ila ninaelewa kwa mantiki.
Kiumbe gani?Huyu kiumbe lazma apigwe chini
Sio kijiwe hikiKaa pembeni,wewe hujui lolote,acha wenye akili wanyooshe mambo
Nikueleze vifungu mimi ni mwanasheria, kama ww ni mwanasheria nitajie kufungu kinachowalinda hao mawaziri.
Hiyo hapoNitajie kifungu kinachoonyesha hayo majukumu inapotokea rais aliyeko madarakani akiwa amefariki. Watu wa TLS mje mtoe ufafanuzi wa hili suala la huyu Mheshimiwa.
Kwanini hivyo vipengele mnavyotaka vitumike ni kwa mawaziri tu wakati kuna wengi tu wameteuliwa na rais na kuapa mbele yake?
Nikafikiri unaweka vifungu kumbe unaleta ngonjera.Kwa mantiki ya kawaida kabisa rais anapoapishwa anaunda serikali yake, na serikali ni mawaziri kwanza. Hao wengine anaendelea nao kadiri muda unavyoenda. Hata Magufuli alipoapishwa alianza kuteua mawaziri kwanza, kisha ndio alikuja kubadili katibu Mkuu Kiongozi, jaji Mkuu, IGP, CDF, wakuu wa mikoa, wilaya nk.
Hili halihitaji kujua sheria bali ni akili timamu na kuweza kupambanua mambo. Sasa ww unaleta ubishani ambao wala haukubebi bali unaonekana juha tu. Achana na hangover za siasa za uzalendo uchwara, hizi ni zama mpya na zina kitabu chake, unakwama wapi?
Katiba iko kimya kuhusu waziri na baraza kwa muktadha unao ongelewa hapa na ndio maana hakuna kifungu kilicho vunjwa na kinacho toa ushauri wowote kwenye muktadha huu
Utawala wa Huyu Rais haujakamilika kwa sababu hana makamu wa Rais ndiyo maana katiba inamtaka ndani ya siku 14 hawe ameteua makamu wa Rais. Hawezi vunja baraza kwa ssbabu inatakiwa ashauriane na makamu wake kuhusu waziri mkuu mpya hivyo baraza bado ni halali.Sasa kikao cha BLM alichoongoza leo Mh Rais ni batili? Tanganyika Law Society
Kama kinacho ongeleka kitaa juu ya ushupavu wa JW, ni kweli, basi jeshi libarikiwe sana.Mjadala huu mtamu sana watu wanauliza vifungu kwenye katiba vinavyosema kuhusu waziri mkuu Rais aliye madarakani anapo fariki!
TLS hoja zao zinazua maswali sana na ni assumptions tuu!
Maana kuna maana kubwa kama kwenye muktadha husika katiba inaponyamaza kuhusu waziri mkuu!
Mbona kwa Vice iko wazi kabisa? Hata kama katiba yetu ina mapungufu wasingeliweza sahau swala la PM kama kweli linahitaji kwenye muktadha tulionao!
Kuna maana kubwa sana katiba kutosema chochote kuhusu PM!
Mimi niko hapa nafatilia uzi huu nipewe vifungu.