TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

TLS kwa mara ya kwanza nimeona mmetekeleza wajibu wenu wa kisheria kwenye nchi hii. Mawaziri wote ikiwemo waziri Mkuu inabidi waambiwe, na wasiendelee kutokea kwenye nafasi zao kwani kwa sasa hakuna baraza la mawaziri.

Nimemuona Majaliwa akiendelea kutambulishwa kama waziri Mkuu, wakati kikatiba hana uhalali huo. Tungekuwa na vyombo vya habari vinavyotekeleza wajibu wao walipaswa kulitangaza hili wazi wazi kuwa kwa sasa hakuna baraza la mawaziri, na waziri yoyote aliyekuwa kwenye baraza lililopita asiendelee kuingia ofisini au kutumia mali za ofisi kama gari nk, wakati hana uhalali huo.
Vipi bado upo na TLS au kwa mama?
 
Akikosea tu kufuata muongozo huo, ndio kitakuwa chanzo cha kuparangana kwa serikali yake... na mwanzo wa watendaji wake kutokuwa na nguzu za kisheria kufanya kazi zao... na hata wakitoa maamuzi, hayo maamuzi yatakuwa ni null and void ab nitio.

Ushauri wa bure, Mheshimiwa SS usome na uufanyie kazi.
Hajafuata, haya Sasa tuone huko kuparangana
 
Waziri mkuu ni jambo jingine. Katiba ikon clear kabisa kuwa waziri mkuu akiondoka/akiondolewa na baraza linavunjika. Hili la rais halina kifungu kama cha waziri mkuu. Ila nadhani ufafanuzi wa TLS uko sahihi.
Bado TLS wapo sahihi?
 
Vipi leo umepata jibu au bado?
Naona umekuja hapa kama kipofu, hujuia hata nini kilisemwa TLS na nini ambacho Mama amefanya leo.

kuweka kumbukumbu sawa hapa JF, TLS walisema kuapishwa kwa Mama Samia Suluhu kuwa rais maana yake ni kuvunjwa kwa baraza la mawaziri la zamani. Na kuundwa kwa baraza jipya kunaanza kwa kuteua waziri mkuu mpya ambaye kisheria anapitishwa bungeni kwanza kabla ya kuapishwa, na ndio mawaziri wengine wafuate kuteuliwa na wote wataapa kwa rais mpya!

Sasa leo mama Samia katangaza baraza lake la mawaziri (kabla ya kuteua kwanza waziri mkuu wake na kwenda bungeni kupitishwa)! Alichokifanya mama Samia ni kama anajichanganya, hajui afanye nini na kipi asifanye. Anadandia ukweli na kuuchanganya na uongo.
 
Wewe bado hujielewi, mama Samia alichofanya ni mabadiliko kidogo kwenye Baraza na sio kutangaza baraza jipya. Hivi huwa mnapeleka likizo hizo akili zenu?
 
Back
Top Bottom