TLS Yalaani Vikali Udhalilishaji na Ukatili wa Kijinsia wa Binti kutoka Yombo Dovya, Dar es Salaam

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimelaani vikali kitendo cha udhalilishaji na ukatili wa kijinsia kilichooneshwa kwenye video inayosambaa mitandaoni, ikimuonesha mwanamke akifanyiwa vitendo hivyo na kundi la wanaume zaidi ya wanne. TLS imelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika na kuhakikisha haki inatendeka. Chama hicho pia kimetoa wito kwa jamii kusimama pamoja kupinga udhalilishaji na ukatili wa kijinsia. TLS pia imeahidi kushirikiana na vyombo vya usalama na haki jinai katika kufuatilia suala hili kwa karibu na kuhakikisha wahalifu wanafikishwa Mahakamani.

Tamko hilo linasomeka.

“Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimepata taarifa kupitia mitandao ya kijamii na taarifa maalum kwa Umma kutoka kwa Jeshi la Polisi Tanzania juu ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mwanamke anayesemekana anaishi eneo la Yombo Dovya Jijini Dar es Salaam akifanyiwa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia na kundi la Wanaume huku wakirekodi video ya vitendo vile viovu. Tukio hilo sio tu ni kinyume na sheria za nchi yetu lakini pia ni kinyume na maadili na utamaduni wetu kama Watanzania.

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kinalaani kitendo hiki kiovu na tunalitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki za kisheria na kuhakikisha wahalifu wote walio tenda kitendo kile na waliowezesha kutendwa kwa kitendo kile kiovu wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani mara moja ili haki iweze kutendeka. Aidha TLS inapinga vitendo vyote vya kikatili na udhalilishaji dhidi ya wanawake na iko tayari kushirikiana na vyombo vyote vya usalama na haki jinai katika kuhakikisha wahalifu hao wanafikishwa katika mamlaka sahihi za haki ili kujibu mashitaka yao. TLS pia kupitia kifungu cha 4 (e) cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act, Cap. 307 R.E. 2002) inaendelea kufuatilia mwenendo wa suala hili kwa ukaribu zaidi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na vinavyosimamia haki jinai ili kuhakikisha hatua stahiki kwa waliohusika zinachukuliwa kwa wakati na kwa mujibu wa Sheria.

Kila binadamu anastahili heshima, haki na usawa katika jamii yetu. TLS inatoa wito kwa jamii kusimama pamoja kupinga udhalilishaji, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia wa aina yoyote ile ikiwemo kuacha mara moja kusambaza video zinazohusu tukio hili ili kulinda haki ya mhanga.

Tanzania bila udhalilishaji, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia inawezekana!

Imetolewa na Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)​

Boniface A.K Mwabukusi - Rais”
Soma pia: Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa mande na wanaume watatu

IMG_5491.jpeg
 
Lawyers wakiamka na kuanza kufuatilia ukiukwaji wa sheria na kutaka wahusika kuchukuliwa hatua, then tutabadilika. Lakini inatia kichefucefu unaposikia wakili msomi ndio anaungana na wapigaji kuhalalisha uvunjifu wa sheria? Inadhalilisha mno fani.
Kwa hili la huyu binti, naunga mkono hoja
 
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimelaani vikali kitendo cha udhalilishaji na ukatili wa kijinsia kilichooneshwa kwenye video inayosambaa mitandaoni, ikimuonesha mwanamke akifanyiwa vitendo hivyo na kundi la wanaume zaidi ya wanne. TLS imelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika na kuhakikisha haki inatendeka. Chama hicho pia kimetoa wito kwa jamii kusimama pamoja kupinga udhalilishaji na ukatili wa kijinsia. TLS pia imeahidi kushirikiana na vyombo vya usalama na haki jinai katika kufuatilia suala hili kwa karibu na kuhakikisha wahalifu wanafikishwa Mahakamani.

Ujumbe huo unasomeka.

“Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimepata taarifa kupitia mitandao ya kijamii na taarifa maalum kwa Umma kutoka kwa Jeshi la Polisi Tanzania juu ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mwanamke anayesemekana anaishi eneo la Yombo Dovya Jijini Dar es Salaam akifanyiwa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia na kundi la Wanaume huku wakirekodi video ya vitendo vile viovu. Tukio hilo sio tu ni kinyume na sheria za nchi yetu lakini pia ni kinyume na maadili na utamaduni wetu kama Watanzania.

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kinalaani kitendo hiki kiovu na tunalitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki za kisheria na kuhakikisha wahalifu wote walio tenda kitendo kile na waliowezesha kutendwa kwa kitendo kile kiovu wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani mara moja ili haki iweze kutendeka. Aidha TLS inapinga vitendo vyote vya kikatili na udhalilishaji dhidi ya wanawake na iko tayari kushirikiana na vyombo vyote vya usalama na haki jinai katika kuhakikisha wahalifu hao wanafikishwa katika mamlaka sahihi za haki ili kujibu mashitaka yao. TLS pia kupitia kifungu cha 4 (e) cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act, Cap. 307 R.E. 2002) inaendelea kufuatilia mwenendo wa suala hili kwa ukaribu zaidi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na vinavyosimamia haki jinai ili kuhakikisha hatua stahiki kwa waliohusika zinachukuliwa kwa wakati na kwa mujibu wa Sheria.

Kila binadamu anastahili heshima, haki na usawa katika jamii yetu. TLS inatoa wito kwa jamii kusimama pamoja kupinga udhalilishaji, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia wa aina yoyote ile ikiwemo kuacha mara moja kusambaza video zinazohusu tukio hili ili kulinda haki ya mhanga.

Tanzania bila udhalilishaji, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia inawezekana!

Imetolewa na Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)​

Boniface A.K Mwabukusi - Rais”
Soma pia: Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa mande na wanaume watatu

Ni jambo jema kwa TLS kufanya hivyo.

Lakini tunakuomba Bwana Advocate Mwabukusi na TLS unayoiongoza kwamba ianzishe Mpango Maalumu kabisa wa kuliangazia janga kubwa sana na baya kabisa lililoibuka kwa kasi miaka ya hivi karibuni, janga la Wananchi kutekwa na Watu wasiojulikana (Forced disappearence)
 
Back
Top Bottom