TLS Yalaani Vikali Udhalilishaji na Ukatili wa Kijinsia wa Binti kutoka Yombo Dovya, Dar es Salaam

Mie niko tofauti kidogo.
Kwani huyu binti kasema nini mpaka saizi?

Jamaa waliokamatwa je wao wamesema vipi?

Hili jambo linahitaji utulivu, watu wanalipapatikia kihisia sana na hili ndio tatizo la kulelewa na singo mama, wana judge mambo kwa feelings kuliko kufikiri hata kidogo.

Vipi kama ikija kujulikana wote kwa pamoja(majamaa na mdada)waliamua kurekodi video kwa hiyari yao, ila wakaamua kuigiza kama binti anashurutishwa??? Labda kwa lengo fulani kama kutafuta Kiki???

Siungi mkono matendo ya namna hiyo lakini tusubiri kidogo uchunguzi ndio tuongee.

Watu wamelipokea hili tukio kwa hisia sana(singo mama product) hivyo kila mtu anatoa matamko tu kana kwamba imethibitika ni ukweli.

Mara ngapi tunaonaga video za x unakuta mwanamke anashurutishwa kweli kweli lakini mwisho wa siku unaona ni maigizo tu.
 
Hii 👆 issue tisi hawausiki Kweli😂
 
Ila nimeshtuka sana nilipoona polisi imetoa namba za simu kuomba isaidiwe kuwapata. Jeshi lenye kila aina ya nyenzo linaombaje kusaidiwa na raia kuwakamata washenzi kama wale? Wakija wahalifu wakubwa kama kina Carlos jeshi litafanyaje?
Sasa jaribu ata kumtukana mkuu wa mkoa, utashangaa namba zako wamepata wapi😂​
 
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimelaani vikali kitendo cha udhalilishaji na ukatili wa kijinsia kilichooneshwa kwenye video inayosambaa mitandaoni, ikimuonesha mwanamke akifanyiwa vitendo hivyo na kundi la wanaume zaidi ya wanne. TLS imelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika na kuhakikisha haki inatendeka. Chama hicho pia kimetoa wito kwa jamii kusimama pamoja kupinga udhalilishaji na ukatili wa kijinsia. TLS pia imeahidi kushirikiana na vyombo vya usalama na haki jinai katika kufuatilia suala hili kwa karibu na kuhakikisha wahalifu wanafikishwa Mahakamani.

Ujumbe huo unasomeka.

“Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimepata taarifa kupitia mitandao ya kijamii na taarifa maalum kwa Umma kutoka kwa Jeshi la Polisi Tanzania juu ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mwanamke anayesemekana anaishi eneo la Yombo Dovya Jijini Dar es Salaam akifanyiwa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia na kundi la Wanaume huku wakirekodi video ya vitendo vile viovu. Tukio hilo sio tu ni kinyume na sheria za nchi yetu lakini pia ni kinyume na maadili na utamaduni wetu kama Watanzania.

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kinalaani kitendo hiki kiovu na tunalitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki za kisheria na kuhakikisha wahalifu wote walio tenda kitendo kile na waliowezesha kutendwa kwa kitendo kile kiovu wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani mara moja ili haki iweze kutendeka. Aidha TLS inapinga vitendo vyote vya kikatili na udhalilishaji dhidi ya wanawake na iko tayari kushirikiana na vyombo vyote vya usalama na haki jinai katika kuhakikisha wahalifu hao wanafikishwa katika mamlaka sahihi za haki ili kujibu mashitaka yao. TLS pia kupitia kifungu cha 4 (e) cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act, Cap. 307 R.E. 2002) inaendelea kufuatilia mwenendo wa suala hili kwa ukaribu zaidi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na vinavyosimamia haki jinai ili kuhakikisha hatua stahiki kwa waliohusika zinachukuliwa kwa wakati na kwa mujibu wa Sheria.

Kila binadamu anastahili heshima, haki na usawa katika jamii yetu. TLS inatoa wito kwa jamii kusimama pamoja kupinga udhalilishaji, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia wa aina yoyote ile ikiwemo kuacha mara moja kusambaza video zinazohusu tukio hili ili kulinda haki ya mhanga.

Tanzania bila udhalilishaji, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia inawezekana!

Imetolewa na Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)​

Boniface A.K Mwabukusi - Rais”
Soma pia: Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa mande na wanaume watatu

Ofisi ya Fatma Karume wakati wa bwana Magufuli ilipigwa na bomu. Je, bwana Mwabukusi amejidhatiti kiulinzi ?
 
Mie niko tofauti kidogo.
Kwani huyu binti kasema nini mpaka saizi?

Jamaa waliokamatwa je wao wamesema vipi?

Hili jambo linahitaji utulivu, watu wanalipapatikia kihisia sana na hili ndio tatizo la kulelewa na singo mama, wana judge mambo kwa feelings kuliko kufikiri hata kidogo.

Vipi kama ikija kujulikana wote kwa pamoja(majamaa na mdada)waliamua kurekodi video kwa hiyari yao, ila wakaamua kuigiza kama binti anashurutishwa??? Labda kwa lengo fulani kama kutafuta Kiki???

Siungi mkono matendo ya namna hiyo lakini tusubiri kidogo uchunguzi ndio tuongee.

Watu wamelipokea hili tukio kwa hisia sana(singo mama product) hivyo kila mtu anatoa matamko tu kana kwamba imethibitika ni ukweli.

Mara ngapi tunaonaga video za x unakuta mwanamke anashurutishwa kweli kweli lakini mwisho wa siku unaona ni maigizo tu.
Uwezo wako wa kuchanganua mambo ni mdogo sana samahani kwa kukuambia hivyo.
 
Ila nimeshtuka sana nilipoona polisi imetoa namba za simu kuomba isaidiwe kuwapata. Jeshi lenye kila aina ya nyenzo linaombaje kusaidiwa na raia kuwakamata washenzi kama wale? Wakija wahalifu wakubwa kama kina Carlos jeshi litafanyaje?
ukiona hivyo hawana nia ya kuwatafuta sababu washawajua ila hawana nia ya kuendelea mbele zaidi.
 
Ila nimeshtuka sana nilipoona polisi imetoa namba za simu kuomba isaidiwe kuwapata. Jeshi lenye kila aina ya nyenzo linaombaje kusaidiwa na raia kuwakamata washenzi kama wale? Wakija wahalifu wakubwa kama kina Carlos jeshi litafanyaje?
Hatari sana,na washarahisishiwa
Video wamepiga

Ova
 
Back
Top Bottom