TMA: Sekta zijipange kukabiliana na upungufu wa mvua

TMA: Sekta zijipange kukabiliana na upungufu wa mvua

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2014
Posts
924
Reaction score
1,096
Dar es Salaam, Tarehe 26/10/2022

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka. Maeneo hayo yakijumuisha mikoa ya (Tabora, Kigoma Kusini, Katavi, Mbeya, Rukwa, Soingwe,Njombe, Iringa, Ruvuma na Morogoro Kusini) katika kipindi cha miezi ya Novemba, 2022 hadi Aprili, 2023.

Wakati wa akitoa utabiri huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri, TMA alisema katika nusu ya kwanza ya msimu (Novemba, 2022 – Januari, 2023) vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza, hivyo sekta mbalimbali zinatakiwa kujipanga na kukabiliana na hali hiyo.

“Upungufu mkubwa wa unyevunyevu katika udongo unatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi yanayopata mvua za Msimu na kuathiri ukuaji wa mazao na upatikanaji wa malisho kwa ajili ya mifugo. Vilevile, kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kupungua na kuathiri upatikanaji wa maji kwa matumizi mbalimbali kama vile umwagiliaji na uzalishaji wa nishati. Mamlaka zinashauriwa kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa pamoja na kuweka miundombinu ya uvunaji maji sambamba na kuandaa na kutekeleza mipango mkakati ya kuhimiza kilimo himilivu”. Alifafanua Dkt. Kabelwa.

Alisema, “Katika nusu ya kwanza ya msimu (Novemba, 2022 – Januari, 2023) vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza hata hivyo, ongezeko la mvua linatarajiwa katika nusu ya pili ya msimu (Februari- Aprili, 2023). Aidha, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa mwezi Mei, 2023 katika maeneo mengi.Maeneo ya mikoa ya Singida na Dodoma mvua za Msimuzinatarajiwa kuanzakwa kuchelewa katika wiki ya pili ya mwezi Januari, 2023“.Alizungumza Dkt. Kabelwa

Mvua za chini ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Singida, Dodoma, Ruvuma, Lindi na Mtwara.Aidha, mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Njombe, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

Akizingumzia kuhusu Msimu wa Vuli kwa miezi ya Oktoba hadi Disemba 2022 katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka, alisema Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia) pamoja na Zanzibar (visiwa vya Unguja na Pemba), msimu unatarajiwa kuendelea kama utabiri ulivyotolewa tarehe 2 Septemba, 2022, ambapo maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hadi wastani. Aidha, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa katika mwezi Januari, 2023.
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa imesema kutakuwa na mvua za chini ya wastani Kwenye mikoa 14

Aidha Dkt. Hamza amesema hali hiyo itasababisha upungufu wa Maji Kwenye mito na hivyo kutakuwa na hali ya kugombea Maji Kati ya binadamu na Wanyama na maradhi yataongezeka

Wakulima wanashauriwa kuwasiliana na maafisa ugani kupata ushauri wa mbegu za muda mfupi wanazopaswa kutumia

Chanzo: ITV habari
 
Na tumeruhusu chakula kiuzwe nje.

Hata kama kuna akiba ya chakula ya Taifa bado haikuwa wazo zuri kufungua mipaka wakati tunafahamu kuna uhaba wa mvua??

Hayakuwa maamuzi mazuri.
 
Tayari kimenuka huko 👇

Screenshot_20221026-154255.png
 
Au Magufuli angekuwepo angeleta Mvua😁
Hapana unapokuwa Rais lazima ujue kuna uncertainty so lazima ujiandae kwa mazingira hayo..

Sasa hakuna alifanya badala yake serikali ya mama ndio mwaka huu imetenga pesa za kujenga mabwawa ya kuvuna maji.kwa ajili ya matumizi na kilimo..

So anakutana na Majanga ambapo yule angefanya sehemu yake athari zisingekuwa kubwa.
 
Watu watalaumu serikali ya mama 😬😬

Wakati walikuwa na Rais wao waliyemwita chuma hakuna cha maana alifanya kwa ajili ya tahadhari kama hizi na alipuuza sekta ya Maji.
Magufuli anahusika vp na huu ukame wa sasa, au yeye ndiye kauleta? Ni jukumu la serkali iliyopo madarakani kutatua changamoto na matatizo yaliyopo kwa wakati huo. Mwache mama apambane na hali yake. Wala hajesema ameshindwa sana sana wewe ndiye unataka kumdhalilisha.

Jinsi ulivyo na chuki na Magufuli unasahau kwamba kabla ya Magufuli pia kulikuwepo maraisi (Kikwete na Mkapa). Tena wakati wa Mkapa na Kikwete ndio lilitokea janga la ukame wa kutisha mbona Kikwete au Mkapa hawakujenga hayo mabwawa au kufanya hicho unachotaka Magufuli afanye na bado huwamlaumu? Nani kakuambia Magufuli ndiye alitakiwa kufanya kila kitu hapa TZ?

Unakomaa kumlaumu tu Magufuli ambaye katika kipindi chake cha uongozi hakukuwa na janga la ukame wa kutisha kama sasa na wakati wa Mkapa na Jk?

ACHA CHUKI BINAFSI NA USIPENDE KULAUMU MAREHEMU MAANA NI SAWA NA UTAHIRA.
 
Watu watalaumu serikali ya mama 😬😬

Wakati walikuwa na Rais wao waliyemwita chuma hakuna cha maana alifanya kwa ajili ya tahadhari kama hizi na alipuuza sekta ya Maji.
mbona inasifiwa kwa mambo ya kipuuzi wacha ilaumiwe pia kwa mambo ya kipuuzi
 
Na tumeruhusu chakula kiuzwe nje.

Hata kama kuna akiba ya chakula ya Taifa bado haikuwa wazo zuri kufungua mipaka wakati tunafahamu kuna uhaba wa mvua??

Hayakuwa maamuzi mazuri.
Kwa hiyo mkulima ndio wa kupangiwa bei na asipotakiwa kuuza?
Njoo ulime uone gharama zake!
 
Angemalizia KWA kusema njaa kubwa sana itatokea serikali ifunge mipaka kuokoa chakula kilichopo!!!


Nilianzisha uzi juzi kuhusu bei ya mahindi,nikazodolewa leo mtabiri anasema mvua ni KIDOGO KWA mikoa 14 ,KAZI ipo!

Bashe zuia mipaka chakula kisitoke watu watakufa njaa!!

Chawa endeleeni kubeza!!!
 
Back
Top Bottom