TMA: Sekta zijipange kukabiliana na upungufu wa mvua

Baada ya kuona mwezi wa 8 umepita bila mvua wakaona waje na utabiri wa kijinga kuwa kutakuwa na ukame. Wao sio Mungu kusema ndio wanapanga, mvua zitanyesha au kutonyesha apendapo Mungu.
 
UTABIRI PICHA.jpg

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema mikoa 14 inayopata msimu mmoja wa mvua inatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hadi wastani kuanzia mwezi Novemba 2022 na kati ya mwezi Aprili mwaka 2023.

Mkurugenzi wa Utabiri wa Mamlaka hiyo, Dkt. Hamza Kabelwa amesema hayo Oktoba 26, 2022 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa utabiri wa mwelekeo wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.

Ameitaja mikoa inayotarajiwa kupata mvua hizo ni Kigoma, Tabora, Katavi, Singida, Dodima, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Njombe, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na kusini mwa Morogoro.

================

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka. Maeneo hayo yakijumuisha mikoa ya (Tabora, Kigoma Kusini, Katavi, Mbeya, Rukwa, Soingwe,Njombe, Iringa, Ruvuma na Morogoro Kusini) katika kipindi cha miezi ya Novemba, 2022 hadi Aprili, 2023.

Wakati wa akitoa utabiri huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri, TMA alisema katika nusu ya kwanza ya msimu (Novemba, 2022 – Januari, 2023) vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza, hivyo sekta mbalimbali zinatakiwa kujipanga na kukabiliana na hali hiyo.

f8b29661-7e22-486a-9e48-ec10923531dd.jpg

“Upungufu mkubwa wa unyevunyevu katika udongo unatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi yanayopata mvua za Msimu na kuathiri ukuaji wa mazao na upatikanaji wa malisho kwa ajili ya mifugo. Vilevile, kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kupungua na kuathiri upatikanaji wa maji kwa matumizi mbalimbali kama vile umwagiliaji na uzalishaji wa nishati. Mamlaka zinashauriwa kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa pamoja na kuweka miundombinu ya uvunaji maji sambamba na kuandaa na kutekeleza mipango mkakati ya kuhimiza kilimo himilivu”. Alifafanua Dkt. Kabelwa.

Alisema, “Katika nusu ya kwanza ya msimu (Novemba, 2022 – Januari, 2023) vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza hata hivyo, ongezeko la mvua linatarajiwa katika nusu ya pili ya msimu (Februari- Aprili, 2023). Aidha, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa mwezi Mei, 2023 katika maeneo mengi.Maeneo ya mikoa ya Singida na Dodoma mvua za Msimuzinatarajiwa kuanzakwa kuchelewa katika wiki ya pili ya mwezi Januari, 2023“.Alizungumza Dkt. Kabelwa

Mvua za chini ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Singida, Dodoma, Ruvuma, Lindi na Mtwara.Aidha, mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Njombe, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

Akizingumzia kuhusu Msimu wa Vuli kwa miezi ya Oktoba hadi Disemba 2022 katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka, alisema Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia) pamoja na Zanzibar (visiwa vya Unguja na Pemba), msimu unatarajiwa kuendelea kama utabiri ulivyotolewa tarehe 2 Septemba, 2022, ambapo maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hadi wastani. Aidha, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa katika mwezi Januari, 2023.
 
Mambo yanaenda kua magumu mazao machache bei juuu Samiaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Ifike mahali tuache kutegemea mvua, hatutoweza kulaumu mabadiliko ya tabia ya nchi kwani sisi binadamu na mapilika yetu ndo tumeifikisha huku, hata Mungu hatuwezi kulaumu.
Lakini tutumie maji taka kuyabadilisha kwa ajili ya matumizi kwa kuyavuna, kusafisha na kuyatibu ili tutatumie tena.

Ifike mahali mimi na wewe tushachelewa mpatie Elimu mwanao haya mambo yatakuwa historia.
 
Dar es Salaam, Tarehe 26/10/2022

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka. Maeneo hayo yakijumuisha mikoa ya (Tabora, Kigoma Kusini, Katavi, Mbeya, Rukwa, Soingwe,Njombe, Iringa, Ruvuma na Morogoro Kusini) katika kipindi cha miezi ya Novemba, 2022 hadi Aprili, 2023.

Wakati wa akitoa utabiri huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri, TMA alisema katika nusu ya kwanza ya msimu (Novemba, 2022 – Januari, 2023) vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza, hivyo sekta mbalimbali zinatakiwa kujipanga na kukabiliana na hali hiyo.

“Upungufu mkubwa wa unyevunyevu katika udongo unatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi yanayopata mvua za Msimu na kuathiri ukuaji wa mazao na upatikanaji wa malisho kwa ajili ya mifugo. Vilevile, kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kupungua na kuathiri upatikanaji wa maji kwa matumizi mbalimbali kama vile umwagiliaji na uzalishaji wa nishati. Mamlaka zinashauriwa kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa pamoja na kuweka miundombinu ya uvunaji maji sambamba na kuandaa na kutekeleza mipango mkakati ya kuhimiza kilimo himilivu”. Alifafanua Dkt. Kabelwa.

Alisema, “Katika nusu ya kwanza ya msimu (Novemba, 2022 – Januari, 2023) vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza hata hivyo, ongezeko la mvua linatarajiwa katika nusu ya pili ya msimu (Februari- Aprili, 2023). Aidha, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa mwezi Mei, 2023 katika maeneo mengi.Maeneo ya mikoa ya Singida na Dodoma mvua za Msimuzinatarajiwa kuanzakwa kuchelewa katika wiki ya pili ya mwezi Januari, 2023“.Alizungumza Dkt. Kabelwa

Mvua za chini ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Singida, Dodoma, Ruvuma, Lindi na Mtwara.Aidha, mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Njombe, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

Akizingumzia kuhusu Msimu wa Vuli kwa miezi ya Oktoba hadi Disemba 2022 katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka, alisema Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia) pamoja na Zanzibar (visiwa vya Unguja na Pemba), msimu unatarajiwa kuendelea kama utabiri ulivyotolewa tarehe 2 Septemba, 2022, ambapo maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hadi wastani. Aidha, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa katika mwezi Januari, 2023.
Wajipangeje sijui...lakini... hivi si kuna wahuni flani walitokea Thailand, wakaja kututengezea mvua hivi, imekuwaje, wapo wapi na wanafanya nini, nimewakumbuka!!
 
Back
Top Bottom