Tatizo kubwa linaloimaliza Tanzania ni "
Udiktekta dhidi ya Demokrasia".
Maoni yangu Mimi nikiwa kama mwanazuoni, msomi na raia wa kawaida ni kwamba Njia ya kuuwa upinzani ni kuuwa demokrasia na kuuwa demokrasia ndiko kuanzisha udiktekta na udiktekta wenyewe unadumu tu kama Wale Deep state Goverment watapata maslahi sawa.
Naomba nikufafanulie kidogo hapa.
1. Demokrasia hipo ili kuondoa Deep state masters, yaani mamlaka nyuma ya mamlaka, serikali nyuma ya serikali, taifa nyuma ya taifa. (H.Polepole anakiita kitu hiki ni Mondo pallarel state, Futungo kule botswana na hapa kwetu Tanzania ni Wauni)
2. Kwanini kuuwa upinzani ndiko kuuwa demokrasia?, Embu fikiria Kuna kuwa na chama kimoja na vingine vyote vyama vya mfukoni, kisha chama hicho kimoja kinakuwa na wakubwa wake "
Mapapa", wa chama. Katika hali hiyo taifa linakuwa salama endapo tu Mapapa hayo yatapata maslahi sawa, na endapo yataanza kuumizana wao kwa wao ndipo hatari kwa taifa utokea.
3. Udiktekta unadumu kwa kuumiza wengine, kuwa na nguvu za kimamlaka kupitiliza, na Kuwa chini ya Deep state Gov.
Kitu ninachoitaji kukwambia hapa ni kwamba Kuuwa upinzani ndio kuuwa taifa, na hapo ndipo hali itakuwa mbaya zaidi ya ilivyo sasa.
Mimi naoni yangu ni kusikilizana na kuunda muundo wa dola utakaoliacha taifa salama, demokrasia ya kisisasa iliyo safi, haki za watu, amani na ustawi wa pamoja. Kinyume na hapo tunajaribu kutengeneza jini lisiloweza kutulizwa kwa ubani wala vumba,
litatutafuna wenyewe kwa wenyewe.
taifa imara alilindwi kwa kuumiza wengine bali kwa muundo uliobora na unatoa fursa sawa kwa wote.
Tembelea
www.katibampya.com