Toa mbinu za kukiua Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Mbona mnawashwa sana kwenye nusu kipenyo chenu? Mkilala cdm mkiamka cdm. Halafu wananchi iko mioyoni mwao. Ni mpango wa Mungu kamwe binadamu hawezi kupangua ,ni kama uhai na kifo. Aluuuhhh!
 
Why bringing CHADEMA to its demise?? CHADEMA inaweza ika ishi sambamba na CCM, CUF, ACT na vingine vingi, for so long as tunatii misingi ya sheria, Siasa safi na utawala bora. Tanzania ni ya wote.
 
Serikali ilifanya tathmini ya viwanda 156 vilivyobinafsishwa tangu mwaka 1990, na kubaini 68 havikuwa vinafanya kazi kwa mujibu wa mikataba. Kati yake, serikali ilipanga kurejesha viwanda 48 kwa ajili ya uwekezaji.
 
CHADEMA hakiwezi kuuawa na CCM wala na Serikali wala na mafisadi wala na mamluki(Mbowe,Lema + CHAUMA) wala na vyombo vya ulinzi na usalama labda kikiboronga kikajiua chenyewe.
 
CHADEMA hakiwezi kuuawa na CCM wala na Serikali wala na mafisadi wala na mamluki(Mbowe,Lema + CHAUMA) wala na vyombo vya ulinzi na usalama labda kikiboronga kikajiua chenyewe.
Kumbe ndio viwanda vyetu vilivyo Chadema Lazima ife
 
Tatizo kubwa linaloimaliza Tanzania ni "Udiktekta dhidi ya Demokrasia".
Maoni yangu Mimi nikiwa kama mwanazuoni, msomi na raia wa kawaida ni kwamba Njia ya kuuwa upinzani ni kuuwa demokrasia na kuuwa demokrasia ndiko kuanzisha udiktekta na udiktekta wenyewe unadumu tu kama Wale Deep state Goverment watapata maslahi sawa.

Naomba nikufafanulie kidogo hapa.
1. Demokrasia hipo ili kuondoa Deep state masters, yaani mamlaka nyuma ya mamlaka, serikali nyuma ya serikali, taifa nyuma ya taifa. (H.Polepole anakiita kitu hiki ni Mondo pallarel state, Futungo kule botswana na hapa kwetu Tanzania ni Wauni)

2. Kwanini kuuwa upinzani ndiko kuuwa demokrasia?, Embu fikiria Kuna kuwa na chama kimoja na vingine vyote vyama vya mfukoni, kisha chama hicho kimoja kinakuwa na wakubwa wake "Mapapa", wa chama. Katika hali hiyo taifa linakuwa salama endapo tu Mapapa hayo yatapata maslahi sawa, na endapo yataanza kuumizana wao kwa wao ndipo hatari kwa taifa utokea.

3. Udiktekta unadumu kwa kuumiza wengine, kuwa na nguvu za kimamlaka kupitiliza, na Kuwa chini ya Deep state Gov.

Kitu ninachoitaji kukwambia hapa ni kwamba Kuuwa upinzani ndio kuuwa taifa, na hapo ndipo hali itakuwa mbaya zaidi ya ilivyo sasa.

Mimi naoni yangu ni kusikilizana na kuunda muundo wa dola utakaoliacha taifa salama, demokrasia ya kisisasa iliyo safi, haki za watu, amani na ustawi wa pamoja. Kinyume na hapo tunajaribu kutengeneza jini lisiloweza kutulizwa kwa ubani wala vumba, litatutafuna wenyewe kwa wenyewe.

taifa imara alilindwi kwa kuumiza wengine bali kwa muundo uliobora na unatoa fursa sawa kwa wote.

Tembelea www.katibampya.com
 
Tulitaka ujue kazi zaidi yetu ili ujue kwa nini ndugu yetu aliuwawa na wewe bado unazengewa zengewe​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…