Toa neno lolote kuhusu michango ya Harusi

Hasa ndugu zetu wakristo unapangiwa mpaka kima cha chini kuna mmoja simjui hanijui kapita tu ofisini kanipa kadi yake na usumbufu ukaanzia hapo kufuatiliana wengine usipochangia ndo mwanzo wa uadui.
 
Hasa ndugu zetu wakristo unapangiwa mpaka kima cha chini kuna mmoja simjui hanijui kapita tu ofisini kanipa kadi yake na usumbufu ukaanzia hapo kufuatiliana wengine usipochangia ndo mwanzo wa uadui.
It's true, ni changamoto kiukweli
 
Ndugu zangu mnatuvunja Moyo sisi tunaotaka msaada kutoka kwenu wana Jamii wenzetu. Mimi Binafsi ninatarajia kufunga ndoa hapo Mwezi wa tatu, na nina nia ya kuomba michango kwa ndugu na jamaa, kutokana na hali jinsi ilivyo kwa sasa suala la kusema naweza kulisimamia hili jambo lililo mbele yangu kwa nilichonacho mpaka Muda huu ni uwongo, hivyo nilikuwa nawaomba wazee kidogo mlegeze misimamo yenu, hali ngumu ndugu zangu, kama una uwezo wa kumsaidia mtu chochote we msaidie tu hata kama ni buku. Shukrani
 
Ndoa si suala la dharula, mpango. Unapotegemea kufanya harusi jipange wewe na ndugu zako, sio kuchangisha watu kwa lazima. Hadi inapelekea kununiana

Kuendekeza michango ya Harusi ni umaskini wa kujitakia.

Unapangiwa single 50/70
Double 100.
 
Tangu nimekuja mkoa mmojawapo nyanza za juu kusini nina mwaka sasa hakuna aliyeniomba mchango, lakini huko nilikotoka kwa mwaka nilikuwa napata kadi kumi za michango ya harusi.
 
Kumbe rafiki yangu umekuja kunisema huku sawa!
 
Fanya lililo ndani ya uwezo wako. Stop allowing people to control your life. Kama unauwezo wa kwenda kanisani ama kwa shehe na kufungishwa ukiwa na nguo za kawaida so be it. Tatizo jamii inatuforce tuishi inavyotaka.

Nimeona harusi bwana na bibi harisi walienda kanisani na batiki (mwanamke) na cardet na shati (mwanaume). Ilikua mwenge mwaka 2011. Mchungaji akawafungisha. Wakatoka hapo kila mmoja akaendelea na mishe zake. Mwanamke kariakoo kwenye biashara zake, mwanaume kazini kwake tegeta.

Jioni wakakutana nyumbani wakachoma nyama na ndizi na viazi. Ikawa imeishaaaa iyo. Tatizo saivi kisa mmealikwa ukweni 20 au 30 basi na nyie upande wa kiume mtataka kuonyesha tunaweza. Mbaya zaidi unakuta mdingi ama maza ndo kasimamia kidete kwamba anataka shughuli kubwa. Siku ya harusi unafatwa tu kaka hiki, kaka kile....huna mia unafaa kukopa. Shughuli ikiisha madeni.

Haya mainsta yasituzuzue tukaondoka kwenye reality. Tufanye kinachowezekana. Natamani nipige mchongo na muslim man ama woman tuunde planning za harusi zisizozidi laki tano. Eboo!! Jivike ujasiri braza. Kama hutapenda huu mfokeo basi nisamehe..hata usiuconsider. Endelea na kamati bro..
 
Wewe mbona ulichangiwa? Au kwakua Yako tayari imepita sasa za wengine hazina umaana.
 
Nasikia huku bongo vijana wamepunguza kuoa, kwahiyo hili tatizo linaenda kuisha usijali sana
 
Nasikia huku bongo vijana wamepunguza kuoa, kwahiyo hili tatizo linaenda kuisha usijali sana
Vijana wanaoa Leo kesho wapo single wana enjoy[emoji16][emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…