Ndugu zangu mnatuvunja Moyo sisi tunaotaka msaada kutoka kwenu wana Jamii wenzetu. Mimi Binafsi ninatarajia kufunga ndoa hapo Mwezi wa tatu, na nina nia ya kuomba michango kwa ndugu na jamaa, kutokana na hali jinsi ilivyo kwa sasa suala la kusema naweza kulisimamia hili jambo lililo mbele yangu kwa nilichonacho mpaka Muda huu ni uwongo, hivyo nilikuwa nawaomba wazee kidogo mlegeze misimamo yenu, hali ngumu ndugu zangu, kama una uwezo wa kumsaidia mtu chochote we msaidie tu hata kama ni buku. Shukrani