Tofauti 3 kati ya Samia Suluhu na Hayati Magufuli

Magufuli si anaonekana hakuwa kiongozi mzuri hivyo kama angehama chama na akashindwa uchaguzi jibu lingekuwa ni kwa sababu hakuwa kiongozi mzuri, sasa samia ambaye anaonekana anaongoza vizuri haijawahi kutokea na wananchi wanamkubali basi afanye kuhama chama kisha agombee tuone.
Kiongozi yoyote wa CCM akihama chama hatoboi
 
Karne hii itamalizika hatotokea Mzalendo kama JPM

Jamaa alithubutu sana kwa kweli
 
Samia ni legacy ya Magufuli kwa hiyo huwezi kuwashindanisha.

Samia anavyofanya vizuri ndiyo Magufuli anafurahia alichagua jembe
Magufuli alipora korosho za wakulima samia hajapita. Kupora
Magufuli hajawahi kuajiri watu samia ana ajiri kila kona
Samia kashusha makato kwenye bodi ya mikopo yule mwingine alichkulia kama chanzo cha mapato
Magufuli akipenda sifa hata kwa mambo madogo sana
Aliua, aliteka, alipora mali za watu na akipenda kudanganya hadharani
 
4. Roho mbaya kwa watumishi wa Uma,
Magufuli aliona ni dhambi kuwaongezea mishahara watumishi wa Uma na hata Ile nyongeza ya Kila mwaka alifuta,wakati mama SSH anaona wafanyakazi nao ni binadamu kama Yeye
5 Magufuli alikuwa hathamini mali za watu. Alikuwa hana HURUMA na watu asio wajua, alibomoa nyumba za watu kule Kimara na kuwaacha wa Mwanza kwa sababu tu walimpigia kura. Leo naamini kuwa Mama Samia kwa hekima, busara na huruma aliyonayo atawakumbuka hawa wahanga wa Kimara - Mbezi, suala la muda tu.
 
Magufuli alipora korosho za
wakulima samia hajapita. Kupora
Magufuli hajawahi kuajiri watu
samia ana ajiri kila kona
Samia kashusha makato
kwenye bodi ya mikopo yule
mwingine alichkulia kama
chanzo cha mapato
Magufuli akipenda sifa hata
kwa mambo madogo sana
Aliua, aliteka, alipora mali za
watu na akipenda kudanganya
hadharani
Hebu nikumbushe watu watano tu waliyouliwa na Magufuli?
 
5 Magufuli alikuwa hathamini
mali za watu. Alikuwa hana HURUMA na watu asio wajua,
alibomoa nyumba za watu kule
Kimara na kuwaacha wa
Mwanza kwa sababu tu
walimpigia kura. Leo naamini
kuwa Mama Samia kwa
hekima, busara na huruma
aliyonayo atawakumbuka
hawa wahanga wa Kimara -
Mbezi, suala la muda tu.
Huruma ya kuwaongezea mitozo huku wengine wanaruhusiwa kula kwa urefu wa kamba zao?
 
Ujinga mtupu tu kumsifia mtu ameingia tu na kuporomosha uchumi wa nchi kutoka uchumi wa kati.
Alichofanya samia ni kuwapa ishara fisadi na wapigaji kwamba sasa wanaweza kuendelea na upigaji bila shaka wala wasiwasi. Magufuli hajawahi kua kikwazo kwa uwekezaji kutoka nje wala nchi haikuwahi kua na shida ya kukimbiwa na wawekezaji wa kweli. Waliyokimbia ni wawekezaji wababaishaji tu.
Mkuu hapa najua hutaeleweka kwa mtoa mada
 
Rais Samia Suluhu ameingia madarakani tarehe 19 Machi 2021 baada ya kufariki kwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli. Hadi leo tarehe 2 Julai 2022 Rais Samia Suluhu ana siku 470 madarakani. Licha ya kuwa madarakani kwa siku chache, Rais Samia Suluhu ameweza kuonesha utofauti mkubwa sana na mtangulizi wake. Ziko tofauti nyingi sana kati ya Samia na Magufuli. Binafsi nitatazama tofauti tatu alizonazo Magufuli na Samia na Samia Suluhu.
Samia Suluhu ni muuni wa Multilateralism na JPM alikuwa muuni wa Economic Nationalism

Rais Samia ni ni mtu anayeamini hasa katika kujenga ushirika mzuri na mataifa na mashirika ya nje ili kuifungua nchi na kuchochoe maendeleo. Ndio maana unaona Mama anafanya sana safari za nje na kupewa mikopo ya mashirika na nchi mbali na wawekezaji wengi kuja nchini kuwekeza. Samia anaamini kwamba Tanzania haipaswi kuwa kama kisiwa, bali ifunguke watu waje kuleta fursa ili kutoa ajira za kutosha na watu wanufaike. Hii ni tofauti na JMP ambaye ni Economic Nationalist. Ni mtu anayepinga masuala ya utandawazi na ushirikiano bali anaamini kwamba rasilimali za nchi husika lazima zinufaishe watu wa eneo husika kwanza kabla ya mtu yeyote pasi na kujali watu wengine watajisikiaje.

Ndio maana JPM alipokuwa Rais aliona kwamba Mikataba ya madini hainufaishi watanzania kama inavyopaswa, hivyo aliamua kubadilisha sheria za sekta ya madini akiamini kwamba watanzania hawatendewi haki, kitu ambacho kilidunisha sana imani ya wawekezaji na kuteteresha uchumi kwa kiasi fulani. Kwa nchi kama Tanzania ambayo bado uchumi wake ni dhaifu, uongozi aina ya Magufuli ni ngumu kufanya kazi ndio maana tulijijitutumua kwamba "Hii nchi ni tajiri" lakini miradi yote mikubwa aliyotekeleza alichukua mikopo ya siri ambayo hata Bunge halikuhusishwa katika kukopa kwake na kulianchai taifa madeni makubwa.

Samia ana ustahamilivu mkubwa wa kisiasa kuliko Magufuli
Wakati wa JPM kulikuwa na matukio ya kutisha sana ya watu kutekwa na kuuwawa kwa siri kubwa na vikosi vya watu wasiojulikana. Rais Samia ana siku 470 tu madarakani na unaweza kusema ni mapema sana kumjua ni mtu wa aina gani, lakini siku hizo zinatosha sana kusema Rais Samia si mtu wa kaliba ya JPM. Uvumilivu wa kisiasa ni ule uwezo wa kuheshimu mawazo ya mwingine na pia kuwapatia haki zote za msingi hata wale walio kinyume na wewe bila kuwafanyia ubaya.

JPM licha ya kuwa na huruma na wanyonge, lakini alikosa kaba dhidi ya watu waliomkosa waziwazi. JPM katika wakati wake waandishi wa habari walikufa, kutekwa, kujeruhiwa, kufungwa, kupewa kesi na wengine kukimbilia ughaibuni kuhofia maisha yao. Haya yote hatuyaoni ndani ya wakati wa Rais Samia Suluhu. Rais Samia hutukanwa sana na vijana mtandaoni, huchorwa katuni na waandishi wa habari wanaandika watakavyo kumhusu lakini yeye ametulia akiwekeza akili yake katika kuleta maendeleo kwa watanzania.

Rais Samia Suluhu ni reformist na JPM ni conservative (Mhafidhina)

Rais Samia Suluhu amejipambanua vyema tangu aingie madarakani kwamba yeye ni mwana mabadiliko. Kama umepata kusoma barua yake ya wazi kwa Watanzania jana wakati tunaadhimisha miaka 30 demokrasi ya vyama vingi Tanzania, utaamini kwamba Rais Samia Suluhu ni mtu anayewiwa kuleta mabadiliko. Rais Samia kama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Chama chake kimetamka dhahiri kwamba kinayo nia ya dhati ya kutaka kuandika Katiba Mpya, jambo ambalo lilikuwa ni dhambi kubwa hata kulitaja tu wakati wa JPM.

JPM ni mhafidhina ambaye alipenda sana kuendesha mambo kizamani akiamini kwamba nchi yetu kufuata mabadiliko ya dunia ni kuurejea ukoloni na pia ni mtego wa watu wa magharibi kutaka kuiba rasilimali zetu. Magufuli hakuamini mambo ya mabadiliko ya tabia nchi, hakutaka kusikia mambo ya uzazi wa mpango na ajenda nyingine za kimataifa, aliamini katika njia zake hasa zile zenye kulinda utamaduni wa mwafrika.
Sawa Chawa..
 
Haya yooote ni ya magu..alipanga kuwa mambo yakiwa magumu bongo atafanya km mama anavyo fanya leo.... Tofauti ni kuwa magu alitamani iwe mwishoni kabisaa ili wamchague milele.....lkn mama yeye hakusubili...
 
Umesahau sifa moja ya Mwendazake kuwa ni Katili huku SSH akiwa ni mpenda haki.
Samia kuonesha kuwa ni mpenda haki angehakikisha kuwa hao anaowateua kuwa RCs na DCs wanakuwa na ratiba ya wazi lini wanasikiliza wananchi na hii ibandikwe ofisini kwao,.
Hivi sasa sidhani kama wana ratiba hizo. Mfano ni RC wa Dar Amos Makalla hana ratiba hiyo tofauti na waliomtangulia!
Wanajifanya kutoa namba zao za simu ambapo wakipigiwa hawapatikani!!
Ni vizuri Samia akawasimamia na kuwaelewesha kuwa kazi yao ni kutatua kero za watu na sio kupokea simu za viongozi wenzao tu
 
Ratiba kila mtu anapanga kwa namna yake,sio kazi ya Rais kuwapangia.
 
Read between the lines wewe mbwiga! Sijasema awapangie nimeshauri ahakikishe wana ratiba na inazingatiwa! Wewe umekwenda ofisini kwa Makalla ukakuta ratiba na register? Unakaa Ikulu unampigia simu na kuzungumza nao unafikiri kila mwananchi ana fursa hiyo?
Ngoja ufukuzwe hapo Ikulu ndio utaelewa nini taabu ya kuwapata hawa viongozi.
 
Rais Samia Suluhu ameingia madarakani tarehe 19 Machi 2021 baada ya kufariki kwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli. Hadi leo tarehe 2 Julai 2022 Rais Samia Suluhu ana siku 470 madarakani. Licha ya kuwa madarakani kwa siku chache, Rais Samia Suluhu ameweza kuonesha utofauti mkubwa sana na mtangulizi wake. Ziko tofauti nyingi sana kati ya Samia na Magufuli. Binafsi nitatazama tofauti tatu alizonazo Magufuli na Samia na Samia Suluhu.
Samia Suluhu ni muuni wa Multilateralism na JPM alikuwa muuni wa Economic Nationalism

Rais Samia ni ni mtu anayeamini hasa katika kujenga ushirika mzuri na mataifa na mashirika ya nje ili kuifungua nchi na kuchochoe maendeleo. Ndio maana unaona Mama anafanya sana safari za nje na kupewa mikopo ya mashirika na nchi mbali na wawekezaji wengi kuja nchini kuwekeza. Samia anaamini kwamba Tanzania haipaswi kuwa kama kisiwa, bali ifunguke watu waje kuleta fursa ili kutoa ajira za kutosha na watu wanufaike. Hii ni tofauti na JMP ambaye ni Economic Nationalist. Ni mtu anayepinga masuala ya utandawazi na ushirikiano bali anaamini kwamba rasilimali za nchi husika lazima zinufaishe watu wa eneo husika kwanza kabla ya mtu yeyote pasi na kujali watu wengine watajisikiaje.

Ndio maana JPM alipokuwa Rais aliona kwamba Mikataba ya madini hainufaishi watanzania kama inavyopaswa, hivyo aliamua kubadilisha sheria za sekta ya madini akiamini kwamba watanzania hawatendewi haki, kitu ambacho kilidunisha sana imani ya wawekezaji na kuteteresha uchumi kwa kiasi fulani. Kwa nchi kama Tanzania ambayo bado uchumi wake ni dhaifu, uongozi aina ya Magufuli ni ngumu kufanya kazi ndio maana tulijijitutumua kwamba "Hii nchi ni tajiri" lakini miradi yote mikubwa aliyotekeleza alichukua mikopo ya siri ambayo hata Bunge halikuhusishwa katika kukopa kwake na kulianchai taifa madeni makubwa.

Samia ana ustahamilivu mkubwa wa kisiasa kuliko Magufuli
Wakati wa JPM kulikuwa na matukio ya kutisha sana ya watu kutekwa na kuuwawa kwa siri kubwa na vikosi vya watu wasiojulikana. Rais Samia ana siku 470 tu madarakani na unaweza kusema ni mapema sana kumjua ni mtu wa aina gani, lakini siku hizo zinatosha sana kusema Rais Samia si mtu wa kaliba ya JPM. Uvumilivu wa kisiasa ni ule uwezo wa kuheshimu mawazo ya mwingine na pia kuwapatia haki zote za msingi hata wale walio kinyume na wewe bila kuwafanyia ubaya.

JPM licha ya kuwa na huruma na wanyonge, lakini alikosa kaba dhidi ya watu waliomkosa waziwazi. JPM katika wakati wake waandishi wa habari walikufa, kutekwa, kujeruhiwa, kufungwa, kupewa kesi na wengine kukimbilia ughaibuni kuhofia maisha yao. Haya yote hatuyaoni ndani ya wakati wa Rais Samia Suluhu. Rais Samia hutukanwa sana na vijana mtandaoni, huchorwa katuni na waandishi wa habari wanaandika watakavyo kumhusu lakini yeye ametulia akiwekeza akili yake katika kuleta maendeleo kwa watanzania.

Rais Samia Suluhu ni reformist na JPM ni conservative (Mhafidhina)

Rais Samia Suluhu amejipambanua vyema tangu aingie madarakani kwamba yeye ni mwana mabadiliko. Kama umepata kusoma barua yake ya wazi kwa Watanzania jana wakati tunaadhimisha miaka 30 demokrasi ya vyama vingi Tanzania, utaamini kwamba Rais Samia Suluhu ni mtu anayewiwa kuleta mabadiliko. Rais Samia kama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Chama chake kimetamka dhahiri kwamba kinayo nia ya dhati ya kutaka kuandika Katiba Mpya, jambo ambalo lilikuwa ni dhambi kubwa hata kulitaja tu wakati wa JPM.

JPM ni mhafidhina ambaye alipenda sana kuendesha mambo kizamani akiamini kwamba nchi yetu kufuata mabadiliko ya dunia ni kuurejea ukoloni na pia ni mtego wa watu wa magharibi kutaka kuiba rasilimali zetu. Magufuli hakuamini mambo ya mabadiliko ya tabia nchi, hakutaka kusikia mambo ya uzazi wa mpango na ajenda nyingine za kimataifa, aliamini katika njia zake hasa zile zenye kulinda utamaduni wa mwafrika.
Wote ni sawa lakini mmoja anaua kwa siri wakati mwingine alikuwa anaua wazi wazi.
Mmoja ni mnafiki sana wakati mwingine ni muwazi hata katika uovu
Wote ni wamoja wanaendelea na ule ule mfumo bila kubadili kitu.

Ameshasema hamuelewi?
Sisi na Magufuli ni KITU kimoja
 
Kachukue form Lumumba Sasa uwanie ubunge wa Africa mashariki,unajikanyaga tu au unasubiri huruma ya mama.Uchawa haulipi.
 
Back
Top Bottom