Tofauti kati ya mabinti wa udsm na wa udom?!!!!!

Tofauti kati ya mabinti wa udsm na wa udom?!!!!!

MAULA

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
1,056
Reaction score
171
Kuna tofauti kubwa kati ya
mabinti wa UDSM na wale wa
UDOM. Mbali na kwamba
wote ni wazuri na
wamemeenda vidato lakini
zipo tofauti kubwa baina yao
zinazowatofautisha. Kwa
ujumla tofauti zao ni hivi
zifuatazo;
Muonekano (image)
Binti wa UDSM mara nyingi
atapenda avae vitu mpaka
aonekane kama
mwanamitindo. Atajiwekea
make up za kila aiana
japokuwa tayari ana uzuri
natural. Atataka avae fasheni
mpya mpya zinazotokana
kwa kuwa yuko town na mara
nyingi hata kama boom
haliruhusu kuna wananchi
wengi wa kuwapiga mizinga.
Nguo zao wananunulia
Mlimani City, Quality Center,
Makumbusho, Mwenge kwa
White na maeneo mengine
kama hayo. Jinsi
wanavyovyaa unaweza
ukawaogopa kudhani ni
expensive saaaaana.
Binti wa UDOM kwa upande
mwingine anavaa kawaida tu.
Viatu vyake vya mchomekeo
wanavinunua pale SabaSaba
lakini waulize wavulana
UDOM sasa, watakwambia
binti katoka bomba yule si
mchezo. Viatu vyao ni bei za
kawaida na huvumilia hali
zote za hewa. Huwa shopping
zao wanafanya Saba Saba.
Sehemu ya kuangalia movie
(cinema)
UDSM huwezi kumpeleka
binti kucheka movie room
kwako! Sijui eti Hall 3 au
ghetto Survey! Utampeleka
Suncrest Quality Center au
Mlimani City na hapo uweke
bajeti ya PopCon na
mazagazaga kibao ya kucheki
cinema.
Binti wa UDOM wewe tu na
laptop yako unamkaribisha
chumbani Block 9, 10, etc
maeneo ya Haiti mnacheki
movie huku mkinywa maji ya
kudownload, bites za
Discount shop au chai.
Umemaliza.
Sehemu ya kukutania (Date
location)
Kama unadhani binti wa
UDSM utampeleke room yako
namba 2409 kule Hall 3 sahau!
Kama huna ghetto la ukweli
Survey au Sinza au Ubungo
Maziwa au unamiliki nyumba
kabisa jua imekula kwako.
Sehemu ya kukutania lazima
iwe ya kueleweka na
treatment isomeke vizuri
kama misosi iliyosimama,
Pizza, Burger, Chicken Chips,
etc. Hapo lazima Bamaga
upajue vizuri, Mikocheni na
Sinza. Kishushio Savanna au
Red Bull. Mjomba huna hivyo
UDSM utawapata wa
kuhesabu kukusikiliza
maelezo yako ya kuunga
unga.
Binti wa UDOM yeye hata
hajali. Wewe tu, uwe kule
porini mnapaita Ng’ox au
Social Room kwako atakuja.
Mtengenezee chai kwa ule
mkate wako wa juzi halafu
anza kumwaga point zako.
Huna haja ya kupajua Area D,
Area C wala Lodge za Area A
ila ukikosea ukakuta mwenye
kaupepo ka jiji lazima kuku
wa Club Maisha na 84 ujue bei
yake.
Upatikanaji wao
(Availability)
Binti wa UDSM atakuona
akitaka kukuona si kinyume
chake. Ukimpigia simu
mkutane atakupa sababu
kibao utabaki kichwa
kinakuuma ila yeye
akikupigia simu mkutane
hataki kusikia sababu yako
hata moja. Anapenda yeye
awe na control.
Binti wa UDOM yeye
anaelewa principle ya give
and take vizuri sana.
Anaelewa mla lazima aliwe
na anaelewa ili uhusiano
uwepo lazima kila mtu aplay
part yake. Ukimpigia simu
baada ya dakika au saa
chache utamuona na
wanapenda kutembea na
wavulana wao campus. Kama
unabisha angalia idadi ya
mabinti wa UDSM
wanaotembea na boys ndani
ya campus na wale wa UDOM
wanaofanya hivyo ndani ya
campus.
Mtazamo wao kuhusu
mapenzi (Perception of love)
Binti wa UDSM atakupenda
kwa ile ulichona nacho.
Kichwa class, una hela au
famous. Nje ya hapo ni wa
kuhesabu bro.
Binti wa UDOM atakupenda
jinsi ulivyo hasa kama shule
kasoma Songea huko kwao
vijijini chuo katua Dodoma,
ila ukikuta ana kahewa ka
Dar kidogo lazima utasanda.
Yale yale.
Mwandishi wa Makala hii
amejitambulisha kama shabiki
mkubwa wa Orijino Komedi,
Mhitimu wa Digrii ya
Ukandarasi na sasa ni chizi
hospitali ya Lutindi Tanga.
 
Peleka hayo mambo facebook au kwa waandishi wa BAAB KUBWA sehemu ya skonga battle na sio hapa mkuu.
 
Peleka hayo mambo facebook au kwa waandishi wa BAAB KUBWA sehemu ya skonga battle na sio hapa mkuu.

Umenifurahisha mkuu... Watu wengine bwana kila wanachokiona fb wanaleta huku.
 
MODS ondoeni hii takataka, vitoto vya siku hizi badala ya kuwaza "Law of conservation of energy'' au ''entrepreneurs who have changed the world of business'' kanawaza mademu. Then vikimaliza shule vinasema hakuna ajira vinatembea na bahasha...
 
grafani11 na HorsePower na Heaven on earth hebu pitieni hapa mtoe maoni maana kuna mtu hapa ameenda chuo anatoa tofauti ya wanawake wa UDOM na UDSM sasa sijui ni mwanamitindo anatafuta wa kuwapeleka sokoni au ni nani

hahaaa sasa baada ya kujua hizo tofauti zao sijui tunafanyaje...

manake sijathubutu kuendelea kusoma hadi mwisho hiyo post yake

kuna siku nilisoma comment ya mtu anasema yuko chuo kiinglish chake

nilibaki hoi,nahisi ndio type za huyo mtu
 
hahaaa sasa baada ya kujua hizo tofauti zao sijui tunafanyaje...

manake sijathubutu kuendelea kusoma hadi mwisho hiyo post yake

kuna siku nilisoma comment ya mtu anasema yuko chuo kiinglish chake

nilibaki hoi,nahisi ndio type za huyo mtu
@heaven on earth nafikiri anataka na sisi tuende huko tukapenge foleni maana anasema ni wazuri na wana viwango so tuumuunge mkono katika research yake
 
Ndo matatizo ya kuiga hayo... Kaona masanja kapewa like za kutosha fb akaona ye acopy na kupest... Jamii forum sio kama unavyoifikiria kijana... Jipange
 
@heaven on earth nafikiri anataka na sisi tuende huko tukapenge foleni maana anasema ni wazuri na wana viwango so tuumuunge mkono katika research yake

hahaa na mie nilikaona hako ka topic kwa Masanja then nae akacopy na kupaste huku.......

sasa kumbe huku watu wako kivingine kabisa
 
hili ni jukwaa la elimu sio jukwaa la ujinga. mtoa mada umekosea njia
 
yaan hyo post kaitoa masanja fb toka mwez wa6 ye ndo kaiona cjui juz,humu co fb mdau,km unataka umaarufu 2ma salam clouds huko km wakna daud wa kota,cjui jose b waukwel umaarafu ucio na faida
 
grafani11 na HorsePower na Heaven on earth hebu pitieni hapa mtoe maoni maana kuna mtu hapa ameenda chuo anatoa tofauti ya wanawake wa UDOM na UDSM sasa sijui ni mwanamitindo anatafuta wa kuwapeleka sokoni au ni nani

Mkuu nimekuja kwa sababu umeniita vinginevyo nilikuwa napita tu ...
Sijamuelewa mwandishi, sijui ni analyst wa wanafunzi wa kike wa vyuo au kama alivyosema yeye mwenyewe kuwa sasa ni chizi hospitali ya Lutindi Tanga na hivyo hakujua anamaanisha nini !!! Sijui alikuwa anataka kuwafedhehesha wanafunzi wa kike wa UDOM kwa ni washamba wasiojua kuvaa na wanapatika kirahisi au alikuwa anawafagilia wanafunzi wa UDSM kuwa ni expensive na wanajua maeneo ya gharama! Sijui alikuwa ana maana gani, kuwa wanafunzi wote wa UDOM and UDSM wanapatikana kwa urahisi kutegemea maeneo yao either wengine kwa gharama kubwa na hao wa mikoani kwa gharama ndogo?!
 
Kuna tofauti kubwa kati ya
mabinti wa UDSM na wale wa
UDOM. Mbali na kwamba
wote ni wazuri na
wamemeenda vidato lakini
zipo tofauti kubwa baina yao
zinazowatofautisha. Kwa
ujumla tofauti zao ni hivi
zifuatazo;
Muonekano (image)
Binti wa UDSM mara nyingi
atapenda avae vitu mpaka
aonekane kama
mwanamitindo. Atajiwekea
make up za kila aiana
japokuwa tayari ana uzuri
natural. Atataka avae fasheni
mpya mpya zinazotokana
kwa kuwa yuko town na mara
nyingi hata kama boom
haliruhusu kuna wananchi
wengi wa kuwapiga mizinga.
Nguo zao wananunulia
Mlimani City, Quality Center,
Makumbusho, Mwenge kwa
White na maeneo mengine
kama hayo. Jinsi
wanavyovyaa unaweza
ukawaogopa kudhani ni
expensive saaaaana.
Binti wa UDOM kwa upande
mwingine anavaa kawaida tu.
Viatu vyake vya mchomekeo
wanavinunua pale SabaSaba
lakini waulize wavulana
UDOM sasa, watakwambia
binti katoka bomba yule si
mchezo. Viatu vyao ni bei za
kawaida na huvumilia hali
zote za hewa. Huwa shopping
zao wanafanya Saba Saba.
Sehemu ya kuangalia movie
(cinema)
UDSM huwezi kumpeleka
binti kucheka movie room
kwako! Sijui eti Hall 3 au
ghetto Survey! Utampeleka
Suncrest Quality Center au
Mlimani City na hapo uweke
bajeti ya PopCon na
mazagazaga kibao ya kucheki
cinema.
Binti wa UDOM wewe tu na
laptop yako unamkaribisha
chumbani Block 9, 10, etc
maeneo ya Haiti mnacheki
movie huku mkinywa maji ya
kudownload, bites za
Discount shop au chai.
Umemaliza.
Sehemu ya kukutania (Date
location)
Kama unadhani binti wa
UDSM utampeleke room yako
namba 2409 kule Hall 3 sahau!
Kama huna ghetto la ukweli
Survey au Sinza au Ubungo
Maziwa au unamiliki nyumba
kabisa jua imekula kwako.
Sehemu ya kukutania lazima
iwe ya kueleweka na
treatment isomeke vizuri
kama misosi iliyosimama,
Pizza, Burger, Chicken Chips,
etc. Hapo lazima Bamaga
upajue vizuri, Mikocheni na
Sinza. Kishushio Savanna au
Red Bull. Mjomba huna hivyo
UDSM utawapata wa
kuhesabu kukusikiliza
maelezo yako ya kuunga
unga.
Binti wa UDOM yeye hata
hajali. Wewe tu, uwe kule
porini mnapaita Ng'ox au
Social Room kwako atakuja.
Mtengenezee chai kwa ule
mkate wako wa juzi halafu
anza kumwaga point zako.
Huna haja ya kupajua Area D,
Area C wala Lodge za Area A
ila ukikosea ukakuta mwenye
kaupepo ka jiji lazima kuku
wa Club Maisha na 84 ujue bei
yake.
Upatikanaji wao
(Availability)
Binti wa UDSM atakuona
akitaka kukuona si kinyume
chake. Ukimpigia simu
mkutane atakupa sababu
kibao utabaki kichwa
kinakuuma ila yeye
akikupigia simu mkutane
hataki kusikia sababu yako
hata moja. Anapenda yeye
awe na control.
Binti wa UDOM yeye
anaelewa principle ya give
and take vizuri sana.
Anaelewa mla lazima aliwe
na anaelewa ili uhusiano
uwepo lazima kila mtu aplay
part yake. Ukimpigia simu
baada ya dakika au saa
chache utamuona na
wanapenda kutembea na
wavulana wao campus. Kama
unabisha angalia idadi ya
mabinti wa UDSM
wanaotembea na boys ndani
ya campus na wale wa UDOM
wanaofanya hivyo ndani ya
campus.
Mtazamo wao kuhusu
mapenzi (Perception of love)
Binti wa UDSM atakupenda
kwa ile ulichona nacho.
Kichwa class, una hela au
famous. Nje ya hapo ni wa
kuhesabu bro.
Binti wa UDOM atakupenda
jinsi ulivyo hasa kama shule
kasoma Songea huko kwao
vijijini chuo katua Dodoma,
ila ukikuta ana kahewa ka
Dar kidogo lazima utasanda.
Yale yale.
Mwandishi wa Makala hii
amejitambulisha kama shabiki
mkubwa wa Orijino Komedi,
Mhitimu wa Digrii ya
Ukandarasi na sasa ni chizi
hospitali ya Lutindi Tanga.
Baada ya kulambwa DISCO sasa hivi una muda wa kutosha kuja kupost ugonjwa wako huku? Nampongeza sana Prof aliyekuning'iniza.

Na huyo uliyedai ndiye mwandishi wa hiyo makala siyo kweli ni wewe mwenyewe.
 
Kama mwandishi yuko lutindi hospital ni lazima huyu aliyetuma post hii yuko naye karibu sana na alimwibia utafiti wake wakati mmiliki akiwa amelala.
 
Back
Top Bottom