Kuna tofauti kubwa kati ya
mabinti wa UDSM na wale wa
UDOM. Mbali na kwamba
wote ni wazuri na
wamemeenda vidato lakini
zipo tofauti kubwa baina yao
zinazowatofautisha. Kwa
ujumla tofauti zao ni hivi
zifuatazo;
Muonekano (image)
Binti wa UDSM mara nyingi
atapenda avae vitu mpaka
aonekane kama
mwanamitindo. Atajiwekea
make up za kila aiana
japokuwa tayari ana uzuri
natural. Atataka avae fasheni
mpya mpya zinazotokana
kwa kuwa yuko town na mara
nyingi hata kama boom
haliruhusu kuna wananchi
wengi wa kuwapiga mizinga.
Nguo zao wananunulia
Mlimani City, Quality Center,
Makumbusho, Mwenge kwa
White na maeneo mengine
kama hayo. Jinsi
wanavyovyaa unaweza
ukawaogopa kudhani ni
expensive saaaaana.
Binti wa UDOM kwa upande
mwingine anavaa kawaida tu.
Viatu vyake vya mchomekeo
wanavinunua pale SabaSaba
lakini waulize wavulana
UDOM sasa, watakwambia
binti katoka bomba yule si
mchezo. Viatu vyao ni bei za
kawaida na huvumilia hali
zote za hewa. Huwa shopping
zao wanafanya Saba Saba.
Sehemu ya kuangalia movie
(cinema)
UDSM huwezi kumpeleka
binti kucheka movie room
kwako! Sijui eti Hall 3 au
ghetto Survey! Utampeleka
Suncrest Quality Center au
Mlimani City na hapo uweke
bajeti ya PopCon na
mazagazaga kibao ya kucheki
cinema.
Binti wa UDOM wewe tu na
laptop yako unamkaribisha
chumbani Block 9, 10, etc
maeneo ya Haiti mnacheki
movie huku mkinywa maji ya
kudownload, bites za
Discount shop au chai.
Umemaliza.
Sehemu ya kukutania (Date
location)
Kama unadhani binti wa
UDSM utampeleke room yako
namba 2409 kule Hall 3 sahau!
Kama huna ghetto la ukweli
Survey au Sinza au Ubungo
Maziwa au unamiliki nyumba
kabisa jua imekula kwako.
Sehemu ya kukutania lazima
iwe ya kueleweka na
treatment isomeke vizuri
kama misosi iliyosimama,
Pizza, Burger, Chicken Chips,
etc. Hapo lazima Bamaga
upajue vizuri, Mikocheni na
Sinza. Kishushio Savanna au
Red Bull. Mjomba huna hivyo
UDSM utawapata wa
kuhesabu kukusikiliza
maelezo yako ya kuunga
unga.
Binti wa UDOM yeye hata
hajali. Wewe tu, uwe kule
porini mnapaita Ng'ox au
Social Room kwako atakuja.
Mtengenezee chai kwa ule
mkate wako wa juzi halafu
anza kumwaga point zako.
Huna haja ya kupajua Area D,
Area C wala Lodge za Area A
ila ukikosea ukakuta mwenye
kaupepo ka jiji lazima kuku
wa Club Maisha na 84 ujue bei
yake.
Upatikanaji wao
(Availability)
Binti wa UDSM atakuona
akitaka kukuona si kinyume
chake. Ukimpigia simu
mkutane atakupa sababu
kibao utabaki kichwa
kinakuuma ila yeye
akikupigia simu mkutane
hataki kusikia sababu yako
hata moja. Anapenda yeye
awe na control.
Binti wa UDOM yeye
anaelewa principle ya give
and take vizuri sana.
Anaelewa mla lazima aliwe
na anaelewa ili uhusiano
uwepo lazima kila mtu aplay
part yake. Ukimpigia simu
baada ya dakika au saa
chache utamuona na
wanapenda kutembea na
wavulana wao campus. Kama
unabisha angalia idadi ya
mabinti wa UDSM
wanaotembea na boys ndani
ya campus na wale wa UDOM
wanaofanya hivyo ndani ya
campus.
Mtazamo wao kuhusu
mapenzi (Perception of love)
Binti wa UDSM atakupenda
kwa ile ulichona nacho.
Kichwa class, una hela au
famous. Nje ya hapo ni wa
kuhesabu bro.
Binti wa UDOM atakupenda
jinsi ulivyo hasa kama shule
kasoma Songea huko kwao
vijijini chuo katua Dodoma,
ila ukikuta ana kahewa ka
Dar kidogo lazima utasanda.
Yale yale.
Mwandishi wa Makala hii
amejitambulisha kama shabiki
mkubwa wa Orijino Komedi,
Mhitimu wa Digrii ya
Ukandarasi na sasa ni chizi
hospitali ya Lutindi Tanga.