Tofauti kati ya Wakili mpenda haki na Wakili mfanya biashara

Joined
Apr 26, 2022
Posts
90
Reaction score
150
WAKILI MFANYA BIASHARA - lengo lake kuu ni kumsaidia mteja wake kushinda kesi, anatumia udhaifu wa sheria au mianya (loop holes) ya sheria, ujanja ujanja na mbinu mbalimbali za kisheria kumsaidia mteja wake kukwepa haki.

Anatumia sheria vibaya na hata kutoa hoja za uongo kupotosha Mahakama kwa makusudi. Anaweza kukubali hoja za ujanja au uongo kama inamsaidia mteja wake kushinda kesi.

Anaweza kutumia mbinu zisizo halali au zisizo za maadili dhidi ya mpinzani wake kwenye kesi (kuviziana Mahakamani) ili kushinda kesi au kufanya ujanja hata kwa mteja wake kuhalalisha au kuongeza malipo. Anafanya kesi kwa pesa tu. Mara nyingi hachukui kesi za watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha, anachagua kesi zile zinazolipa vizuri.

Lakini, WAKILI MPENDA HAKI - lengo lake kuu ni kupata haki. Hatumii hila au ujanja kumsaidia mteja wake kushinda kesi, bali anaisaidia Mahakama kufikia haki na kutoa uamuzi sahihi, sio kushinda kesi kwa hila. Anasimama kutetea haki za watu sio maslahi yake binafsi.

Wakili mpenda haki anatumia sheria kulinda jamii. Hatoi hoja za uongo wala kuipotosha Mahakama makusudi. Anaangalia haki iko wapi, anaweka haki mbele ya fedha. Anaweka maadili juu kabisa kama msingi wa kazi yake. Hatumii mbinu zisizo halali au zisizo za heshima kumshinda mpinzani wake. Anaweza hata kusimamia kesi bila malipo (pro bono) au kwa malipo kidogo. ⚖️

Mawakili hao wote ni wanataaluma halali. Tofauti sio sheria, bali dhamira, maadili na malengo yao.

Mwandishi: Zechariah Wakili Msomi
(0612275246 /
(0754575246 WhatsApp)
[email protected]
 
Good
 
Back
Top Bottom