Sifahamu chochote, ila ambacho nina uhakika nacho ni hiki. Kiongozi yoyote wa ummah, ni zao la jamii anayotoka. Hivyo tabia za kiongozi huakisi mno tabia na aina ya jamii inayotawaliwa....
Tusiwatenge viongozi kama ni binadamu wa aina nyingine tofauti na sisi. Hujiulizi kwanini, watu wanaoonekana ni wazalendo na wachukia ufisadi, hubadilika mno pindi wamepata madaraka.
Mwanafalsafa wa kijerumani Max Weber anasema ukiona kiongozi anaishi kama mtawala "mfalme" na anategemea sana nguvu zake na hulka "charisma" kuliko sheria, kanuni na taratibu basi fahamu fika kwamba jamii anayoiongoza iko nyuma mno kimaendeleo.
Tembea sehemu muhimu za nchi hii kama, taasisi za kielimu, masoko ya ummah, maofisi ya ummah, hospitali za ummah na taasisi za kifedha, halafu angalia aina ya watu waliopo huko ndiyo utafahamu kwanini Tanzania ipo hapa ilipo. Kuna hatari kubwa mno.
Watanzania tusitafute mchawi kabisa, ilhali sisi wenyewe ni watu wa hovyo. Jamii ambayo imejiaminisha kwamba fedha, mali na starehe ndiyo malengo makuu ya binadamu hapa duniani, usitegemee itakuza viongozi wazuri.
Vijana leo hii wanaingia kwenye siasa au wanafanya kazi ili wapate ukwasi wa kupondea raha. Waende sehemu wanywe pombe, wapate wanawake, wawe maarufu au wapate vyeo.
Hedonistic Societies are inherently destructive. Ancient Rome is a prime example.....