Tofauti kubwa ya Ally Kiba na Diamond hii hapa

Nakubaliana na maelezo yako lakini kama wewe ni mfuatiliaji wa mijadala ya Diamond ungegundua kwamba wengi wao raha yao ni kuona Diamaond anapotea... na hili wanalisema wazi wazi... huyo Somji niliyemtaja ni mfano tu coz' nisingeweza kumtaja kila mtu! Sidhani kama hao uliowataja watu walikuwa wanawaombea mabaya bali walikuwa tu against na tabia zao!!

Uliza sababu za msingi zinazowafanya wamuombee mtu mabaya... lakini hakuna atakayekupa jibu... afadhali umetaja uovu wa akina Tiger Wood na MIchael Jackson! Uliza hao wanaotamani kuona Diamond ameshuka, kijana amefanya nini hasa so serioua... hakuna mwenye jibu! Wapo watakaokuambia ameikashifu Mbeya... ukiwaomba source inayoaminika iliyomnukuu Diamond akiiponda Mbeya, hakuna atakayekupa! Sasa wenye akili zao wanajiuliza... Diamond ambae anapiga show hadi wilayani na miji midogo kama TUnduma, hivi kweli inaingia akili azikashifu hotel za Mbeya?? Wengine wanadai oh, jamaa ni malaya sana... nani kasalimika? Huyo KIba mwenyewe wanayemlinganisha nae amezaa na wanawake watatu tofauti na wote amewapiga chini... kwahiyo Diamond akichapa akina Wolper inakuwa nongwa, lakini wengine wakizalisha huku na kule ni sawa tu!! Hata hao wanaosema Diamond ana dharau ukiwaliza dharau ipi wamefanyiwa wao kama wao, hakuna mwenye jibu! Kuna mtu humu amedai kwamba wakati Diamond anauza mitumba Magomeni alikuwa mshikaji wa jamaa mmoja ambae member wa humu JF ni mtu wake wa karibu! Lakini member huyu anadai hivi sasa Diamond hamkumbuki kabisa huyo jamaa.... aaaaaargh! Hili nalo limfanye mwingine kuwa na nongwa??

Kutokana na watu kutokuwa na hoja za msingi ndio maana wengine tunashawishika kuamini kwamba wengi wao wanasukumwa na chuki na wivu kwavile mtu asiye na husuda hawezi kuombea kuona mtu mwingine anaanguka tena kwa sababu ambazo wala hazikuhusu moja kwa moja!
 
Kipenda roho.....

dawa...!!!
mi sikujua km itakua big deal maana huko instagram jamani jana nimeona kuna watoto wameanzisha team km mbili kila page ya msanii wa bongo kutangaza akaunti yao maalum kwa chibu dangote si uswahili huo
afu mi naona ndo wanazidi kumharibia yaani
halafu wameingia kwa kiba wanatukana na mtu ukisifia mitusi hiyoooo
 

Na hapo ndio watu watajifunza maana ya muziki na hawatothubutu kumlipa mtu kama Davido kuja Tanzania kuimba playback, na kina Fally Ipupa wataendelea kutesa na Afro dance zao.
 

asante umemaliza na tufunge mijadala yote kwa leo
saaaf sana
 
Unaona sasa? Ili ufurahi ungependa kila mtu awe pro Domo hicho kitu sahau kabisa, huyo tutusa wenu Domo zingekuwa zinamtosha ushauri wa kumpa Wema angempa kitandani na siyo Instagram leo zile ndimu zinawahusu nunuweni kwa wingi mtengeneze juice.
Eh! Nitakuwa mtu wa ajabu kuomba kila mmoja awe pro-Diamond! Ikiwa hata Jesus mwenyewe na Muhammad wameshindwa kumshawishi kila mtu kuwa upande wao, itakuja kuwa Diamond!!! Nitarudia tena na tena... sina tatizo na Kiba na hata nyimbo zake nazisikiliza tofauti na nyinyi mnaojifanya kumponda Diamond huku siku zikiwa hazipiti bila kusikiliza nyimbo zake! Na kuwa more honesty, nyimbo yake ya Mwana-Dar es salaam binafsi haijanigusa lakini bado namkubali kwa nyimbo zake zingine nyingi tu!

Tuje hilo la Diamond na Wema.... aaaaaargh, sasa suala la Diamond na Wema kwanini limkere mwingine? By the way, hivi Team Wema si ndo walianza kumshambulia Diamond kwamba anamlostisha Wema na kutokana na hilo ndipo Diamond akaamua kutoa ufafanuzi?? Hii kulikuwa na kitu gani so special pale hadi tuone ilifaa uwe ni ushauri wa chumbani?? Kwani Diamond alizungumzia suala la chu'pi na sidiria za Wema pale?? By the way, hivi pale alikuwa anampa ushauri Wema au alisema tatizo ni Wema mwenyewe coz' keshamshauri sana kuachana na mashoga wa hovyo hovyo na pombe! Hivi ni suala la chumbani hili? Isitoshe, yeye alitoa ushauri wakiwa peke yao lakini baada ya kuona anasakamwa bila kosa akaamu kuweka mambo wazi!
 
Ooooh jamani...Mimi ndio maana nazidi kumpenda Kiba,ana busara sana jamani,wakati mwenzie anahaha kumdharau eti 'atamsaidia' lakini yeye anamsifia
Am speechless jamani nimefurahi sana (lakini haizidi juzi leaders)

Hahahaha..haizid juzi kwakweli..mimi bado nna furaha...go go kiba huu ni mwanzo tu
 
Na kazi ya kumpenda kiba ni ya demu wake si ndio eeee

Ha ha ha na kweli aisee...jamaa ana wivu huyo usikute anakula Ugali wa shikamoo hadi leo na kuny.a kwa foleni nyumbani kwahiyo lazima amchukie tu.
 
Uchawi sio lazima mtu akuroge hata kukuombea DUA mbaya tu ni uchawi pia.
Simply,,mtu kama anaringa ni yeye na maisha yake kwani hatuwezi kuwa sawa kwani vidole tu hatufanani itajakuwa tabia au malezi?

Mi si #TeamKiba wala #TeamDiamond ila siwez kumchukia kisa ni tabia zake ila kwangu atabaki kuwa Kiba ni anajua muziki na Diamond ni mwenye mafanikio zaid ya Kiba
 
Alikiba kwenye nyimbo yake fulani aliimba haya maneno na naona yanatimia.
"Yule alie kupa wewe, ndo kaninyima mimi, na kama riziki anatoa yeye........ ila Mungu ndo anatoa hata kwa foleni hata kama niko nyuma nitapata lazima."
 
Tatizo kubwa hapa Bongo, msanii yeyote akikataa kuburuzwa na hao akina Kusaga na wenzao( clouds media) ndio wanaanza kumsanyia fitina za kumshusha kisanii, tuliona kwa Sugu, Jaydee na sasa Diamond, hawa ni wasanii wanaojielewa, na wanajua nini wanafanya, mbona Mwz hakuzomewa na sehem zingine pia hakuzomewa, hapo ndio ufahamu ya kuwa wazomeaji wote walilipwa posho na ndio maana yule demu wa clouds alipomuita Ali Kiba akawaita pia wapambe wa Kiba kwa kusema Team Kiba mpoooooo! Ila ukweli Ali Kiba alijichanganya mwenyewe kwa kuridhika na mafanikio madogo aliyoyapata kipindi yupo juu, sasa hivi akubali tu kuwa mwenzake yupo juu na kumshusha hata mtumie media zenu hamtaweza coz mlishachelewa. Huo ndio ukweli. Vinginevyo labda wanamfanyia promo kiaina kupita Diamond ili kumrudisha juu!
 
NasDaz kuna movie inaitwa,'There is a thin line between love and hate" umeshawahi kuiona ni ya zamani kidogo. Je unakubaliana na hilo?
 
Kiba na diamond inaelekea wana udini na ukabila eeeh!!!
 

Mkuu NasDaz nmeamin wewe n mnafiki,na muongo kama demu wangu wa zamani hakuna sehemu niloandika diamond kaisha kwenye ile post that day,ila nilifurahia tu siamond kukosa tuzo..
 
Last edited by a moderator:

Hii post ndio ilipaswa aitume kuwajibu Team Wema watu wenye akili tungemuona amekomaa kiakili.
 

Attachments

  • 1413875138010.jpg
    53.3 KB · Views: 172
Hii post ndio ilipaswa aitume kuwajibu Team Wema watu wenye akili tungemuona amekomaa kiakili.

nimeiona nimemuonea huruma
sipati picha bi sandra anajiskiaje uchungu wa mwana
 
Tomboka mrembo!!

Hawa no wasanii wawili todauti kulingana na aina ya miziki yao. Kiba meseji sauti na upangaji wa vina no 100%. Kwa maana nyingine mziki wake Una utamu masikioni. Diamond yeye bora soko. Ukisikiliza nyimbo zake ni mule mule naweza sema ubunifu si mkubwa Sana ndo maana hata yeye alisema h@mini kwenye talent.
Mziki ukiwa na maudhui Mara nyingi fani inakuwa ndogo, na fani ikiwa kubwa maudhui ni kidogo. So kiba ni Mzee wa maudhui na diamond ni Mzee wa fani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…