Nyerere was very clever, Ndiyo maana hata uhuru kaupata kwa kuwashinda wazungu kwa hoja na siyo kwa kumwaga damu unnecessarily....
Wewe hujamsikia yule mama aliyesema amewanyoosha tayari?Sasa mjinga ni yupi kama ameshawanyoosha kabla ya mabeberu?Mtasubiri sana hayo ya mnyoosho,
Na hata ikitokea anaeumia ni wewe na sio yeye.
Utakekosa huduma ni wewe sasa unafurahia nini?
Ujinga mtupu.
Why watazuia misaadaLabda nikuulize maswali binafsi, una mtoto na Familia ya kulea ? I mean, kwa nini uko dhaifu kiasi hicho ? Je unaweza kuilinda na kuitetea Familia yako kama unayao ? Hauna baba na mama kama wengine ? Hivi mnafikiri Muzungu amakeaa huko muda wote anaiwaza Tanzania ni nani aliwadanganya? Kwa taarifa yenu tu katika nchi ambazo siyo muhimu kwa Muzungu Tanzania ni mojawapo, Muzungu hawezi kupoteza usingizi sababu ya tanzania, his plate is full, acheni ujinga fanyeni kazi, ...
Huyu anatakiwa siku moja asaidiwa kufukuza mbu akimtua sehemu sehemu, kwa nguvu zote! Atajua ni kwa nini si kila tatizo linatatuliwa kwa kutumia nguvuStone ni muumini wa nguvu kutatua tatizo soon atatuma mapolisi wakapige shangazi zao hao mabeberu awatujui kwamba sie ndie mabingwa wa ligi na bifu hapa ni kiwandani
Hakurudisha, alikataa misaada ya masharti.Nyerere alisha wahi kurudisha msaada wa fedha na kukataa misaada mingine kutoka Jumhuri ya Shirikisho la Ujerumani baada ya kupewa sharti la kuvunja uhusiano na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani.
Alishawahi rudisha fedha za misaada pia kutoka Uingereza kesho yake tu baada ya Uingereza kuipa Tanzania mwezi mmoja kufuata masharti yao huku wakitishia kufuta misaada.
Acha hizo. Wakati sisi tunadai uhuru bila vita Kenya walikuwa wanapigana na Uingereza vita ya Mau Mau. Sasa nyakati tofauti kivipi wakati huo vuguvugu la kutumia bunduki kudai uhuru lilikuwa limeota mizizi Afrika yote? Unaweza kusema Kenya lilikuwa koloni na sisi protectorate, lakini bado siku zote Nyerere alisema vita inakuwa last resortHaujui hata kulinganisha na hata unachokiandika siajabu haukielewi, unaelewa Nyerera aliishi na kutawala kipindi gani? Dunia ilkuwaje kipindi hicho, unawezaje kulinganisha changamoto za miaka ya 80 na leo hii ? Isitoshe kwanza ni nini aliyemwaga damu hadi uandike hivyo hivyo ?
Hizo ni conspiracy theory ambazo mara nyingi husemwa na watu ambao wakati huo wala hawakuwa wamezaliwa. Msugiuano wa Tanzania na Uganda ulianza siku nyingi kabla hata hiyo vita kuanza mwaka 1978. Kisa kilikuwa ni urafiki mkubwa kati ya Obote na Nyerere, na Nyerere kumhifadhi Obote na familia yake hapa Tanzania. Kulikuwa na supermarket moja tu Dar enzi hizo, Dar supr market, ambayo ilikuwa ya mama Obote ili kuikimu familia yao. Katika utawala wake, Idd Amin kila mfano wa vita alikuwa akitolea Tanzania. Kuna wakati kabla hata ya vita, alinunua ndege za vita akasema sasa tunaweza kupiga Mwanza kirahisi tu. Akinunua mizinga alikuwa anasema mizinga ina range ya kupiga hadi Dar es Salaam, Tanzania.Nyerere yupi unae mzungumzia?
Nijuavyo Nyerere alibanwa na benki ya dunia kuhusu Sera za Tanzania kwenye uchumi, ndio mpaka akaingizwa kwenye vita na Uganda ili kuikamua nchi kiuchumi, na baada ya hapo nchi ikayumba sana mpaka akalazimika ang'atuke ili kupisha mageuzi (matakwa ya benki ya dunia) ya uchumi kwa bwana ruksa ndio nchi ikaanza kukaa vizuri, kila raisi ana changamoto zake maana wao ni binadamu, kukosea kupo, japokuwa sio Sera za kibepari kuona masikini anafanikiwa, utatumia kila aina ya rasilimali zilizopo kumkandamiza!
Kabudi ni mtu mmoja ambae anajua sana sheria, lakini tatizo ni kwamba ni showoff, cocky na pompous. Hiyo inamfanya akose kabisa sifa za diplomacy na kutofaa kabisa kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.Kabudi awe makini sana akienda huko kwa mabberu wanaweza kumkamata kama ndege zetu akashindwa kurudi
Wanasayansi wengi ni wazuri Sana kwenye claiming capacity na sio kwenye reasoning capacity.Thus ni nadra Sana sayansi kutoa kiongozi Bora.Huyu anatakiwa siku moja asaidiwa kufukuza mbu akimtua sehemu sehemu, kwa nguvu zote! Atajua ni kwa nini si kila tatizo linatatuliwa kwa kutumia nguvu
Kweli mkuu. Ndio maana USA mara nyingi maraisi wao wana background ya sheriaWanasayansi wengi ni wazuri Sana kwenye claiming capacity na sio kwenye reasoning capacity.Thus ni nadra Sana sayansi kutoa kiongozi Bora.
Uongozi ni reasoning na sio claiming (kukaza msuli ili kufaulu)
Mkuu unaweza kuwa sawa, lakini mfano ulioutumia wa vita ya Kagera sio sawa na hauna uhalisia!Nyerere yupi unae mzungumzia?
Nijuavyo Nyerere alibanwa na benki ya dunia kuhusu Sera za Tanzania kwenye uchumi, ndio mpaka akaingizwa kwenye vita na Uganda ili kuikamua nchi kiuchumi, na baada ya hapo nchi ikayumba sana mpaka akalazimika ang'atuke ili kupisha mageuzi (matakwa ya benki ya dunia) ya uchumi kwa bwana ruksa ndio nchi ikaanza kukaa vizuri, kila raisi ana changamoto zake maana wao ni binadamu, kukosea kupo, japokuwa sio Sera za kibepari kuona masikini anafanikiwa, utatumia kila aina ya rasilimali zilizopo kumkandamiza!
Sasa kwani mimi nimesemaje juu ya vita Mkuu, maana naona unaunga mkono nilichosema. Hivi umeangalia kuwa hiyo post nilikuwa najibu kauli gani?Mkuu unaweza kuwa sawa, lakini mfano ulioutumia wa vita ya Kagera sio sawa na hauna uhalisia!
Chokochoko za Idd Amini ndizo zilizotusukuma kuingia kwenye vita ile, hata ungelikuwa wewe machukizo ya Idd Amini usingweza kuyavumilia!
Amini alifika mahala anamwambia Nyerere ni beautifull na kwamba angelikuwa mwanamke angemuoa! Wakati wa uvamizi wa kule Kagera kuna ndugu zetu waliuwa kinyama sana, mama mjamzito anachomwa kisu kikavu kikavu na kukata tumbo kutoa mtoto nje alafu wote wakiwa maiti wanatupwa mbe ya mamba!
Tena katika uvamizi ule Amini alishusha bendera yetu na kupandisha ya Uganda huku akijitapa kuwa Nyerere akisema fyoo....atamtandika mpaka Dar es salaam!
Hivi wewe uwe ni kiongozi mwenye roho ya aina gani ya kuvumilia yote hayo huku mamia ya wananchi wako hawana makazi na wengine wameuawa??
Tuache kutungia mifano simple kwa hoja nzito! ....Hatukuwa na viwanda vya kutengeneza silaha za kivita za kukabiliana na Uganda ya Idd Amin ambayo ilikuwa imewekeza sana kwenye kuimarisha majeshi yake, hivyo kuomba msaada nje lilikuwa ni jambo lisiloepukika, vinginevyo waganda wangetusambaratisha na kuchukuwa Tanzania nzima!
"Magufuli aendelee kuwatia njaa mabeberu"Magufuli sio mtu wa kawaida weweeee,acha aendelee kuwatia njaa hao mabeberu,ni mfia nchi yake kikweli kweli,hana unafiki kwa mabebeeu kama viongozi wengine wa kiafrika,usimfananishe na viongozi wengine waoga na vibaraka wa mabeberu,huyu ndio mkombozi wa Africa na si Tz pekee kwa fikra za viongozi wake