Nyerere yupi unae mzungumzia?
Nijuavyo Nyerere alibanwa na benki ya dunia kuhusu Sera za Tanzania kwenye uchumi, ndio mpaka akaingizwa kwenye vita na Uganda ili kuikamua nchi kiuchumi, na baada ya hapo nchi ikayumba sana mpaka akalazimika ang'atuke ili kupisha mageuzi (matakwa ya benki ya dunia) ya uchumi kwa bwana ruksa ndio nchi ikaanza kukaa vizuri, kila raisi ana changamoto zake maana wao ni binadamu, kukosea kupo, japokuwa sio Sera za kibepari kuona masikini anafanikiwa, utatumia kila aina ya rasilimali zilizopo kumkandamiza!
Hizo ni conspiracy theory ambazo mara nyingi husemwa na watu ambao wakati huo wala hawakuwa wamezaliwa. Msugiuano wa Tanzania na Uganda ulianza siku nyingi kabla hata hiyo vita kuanza mwaka 1978. Kisa kilikuwa ni urafiki mkubwa kati ya Obote na Nyerere, na Nyerere kumhifadhi Obote na familia yake hapa Tanzania. Kulikuwa na supermarket moja tu Dar enzi hizo, Dar supr market, ambayo ilikuwa ya mama Obote ili kuikimu familia yao. Katika utawala wake, Idd Amin kila mfano wa vita alikuwa akitolea Tanzania. Kuna wakati kabla hata ya vita, alinunua ndege za vita akasema sasa tunaweza kupiga Mwanza kirahisi tu. Akinunua mizinga alikuwa anasema mizinga ina range ya kupiga hadi Dar es Salaam, Tanzania.
Hata kuna wakati timu ya Taifa ya mpira ilikuwa iende Uganda Nyerere akasema msiende yule kichaa anaweza kuwafunga au hata kuwaua, na hapo ilikuwa kabla ya vita.
Kina Museveni waliokimbilia Tanzania - kabla ya vita, walitaka kuanzisha vita ya msituni dhidi ya Idd Amin Nyerere akawaziua na kusema wasubiri kwanza, Mueveni aende shule badala ya kufikiria vita, na Idd Amin alijua haya yote.
Kwa hiyo vita kati ya Tanzania na Uganda lilikuwa ni suala la lini itatokea, sio msukumo wa nje. Na wala Tanzania ilikuwa haijajiandaa na vita hii. Ndio maana hata vikosi vya JWTZ havikuwa mpakani ndio maana Idd Amin aliiingia nchini kirahisi. Lile daraja la Kagera tulivunja wenyewe, lakini tukasema Idd Amin. Lengo lilikuwa kumfanya Idd Amin asiingie ndani zaidi kwa kuwa hatukuwa tayari kukabiliana nae.
Hata kujibu uvamizi, ilibidi tuanze kutafuta silaha kwanza na tukawa hatuna fedha za kununua cash ndio maana nchi kama Algeria wakatusaidia silaha muhimu baada ya nchi za Magharibi kutukatalia. Samora yeye alikuwa tayari kutupa majeshi yake immediately ili wakati tunajiandaa wao ndio wawe wanapigana frontline, Nyerere akawakatalia. In fact Samora wala hakungoja, tulipovamiwa tu alileta majeshi, wakaabiwa walinde mitaani hapa Dar, wakafundishwa neno moja la kiswahili "kitambulisho?"