Msipende kutazama vitu vidogo vidogo. Hapo Burundi, alipofariki Rais wao, Rais wetu alienda?
Hawa Marais ni binadamu, tunayoyajua kuhusu maisha yao ni machache. Ni wangapi walikuwa wanajua kuwa Hayati Magufuli alikuwa na tatizo la moyo? Kila wakati tulimlaumu kwa kutokusafiri, lakini huenda tatizo lake la afya lilimfanya asiwe huru sana kusafiri. Watu wenye matatizo ya afya ya kudumu, mara nyingi hupata matatizo ya hapa na pale. Yawezekana wewe unapopata msiba, yeye siku hiyo akawa ameamka vibaya kutokana na tatizo lake la afya.
Mseveni ni mtu mzima sana, huwezi kujua ana tatizo gani la afya. Raila alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu, hakuja. Yeye angalao tumajua anasumbuliwa na corona. Kagame, hivi karibuni amepokea chanjo. Wakati mwili ukiendelea kujikinga, unashauriwa ujikinge ili usipate maambukizi wakati chanjo ikiwa bado haijakutengenezea kinga.