Tofauti na SADC iliyoleta Marais 8, Jumuiya ya Afrika Mashariki amekuja Rais Kenyatta pekee kumuaga Hayati Magufuli

Tofauti na SADC iliyoleta Marais 8, Jumuiya ya Afrika Mashariki amekuja Rais Kenyatta pekee kumuaga Hayati Magufuli

Anayeshikamana na wewe wakati wa shida ndiye rafiki wa kweli.

Kiukweli Jumuiya ya SADC imetushika mkono kiuhakika katika msiba huu mkubwa wa taifa.

Tumeshuhudia Marais kutoka Msumbiji, Afrika Kusini, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Congo nk wakija kumuaga Hayati Magufuli ambaye alikuwa kiongozi mwenzao.

Kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tumemshuhudia Rais Uhuru Kenyatta pekee kati ya Marais 5 wanaounda Jumuiya.

Itoshe tu kusema SADC ndio marafiki wa kweli.
Walimfahamu vizuri sana kwa kuchelewesha Miradi mingi ya Jumuiya ikiwa ni pamoja na SGR, kwa hiyo, kama sisi sote nao wanangoja kwa hamu kuona huyu atakuwaje katika kutoa mchango wake kuendeleza Jumuiya ya Wanachama 7 sasa.
 
Huyo Tall urafiki wake ulikuwa wa kimaslahi tu, japo marehemu alimuweka karibu sana na kuwa marafiki na hata wengine kudai alikuwa akimshauri mengi tu
 
Back
Top Bottom