Hiki ni kipindi hatari sana na nyie Watanzania mnavyokusanyika na kubanana kwenye huu msiba bila kuchukua tahadhari kisha mnategemea nani aje kujitoa mhanga kisa undugu.
Hao watakuja siku ya kumzika kisha wasepe, masuala ya maisha hayana utani maana uhai unao mmoja tu na hauna mbadala, hiki kirusi kinaondoka na yeyote hata uwe tajiri mwenye hela au rais, kinakubeba tu.
Ingekua huyu kwenye hii picha ndiye anaongoza, nahisi mambo yangekua tofauti maana yeye huwa mjanja sana alishasema za kuambiwa ongeza na zako pia. Ona hapa alivyojilinda wakati wengine wamejianika mazima mazima.