Badala ya kutoa suluhisho ushaanza kulalamika asubuhi na mapema, matatizo haya yanafahamika. Ungetoa suluhisho ungefanya la maana sana.
Huenda kueleza tofauti yetu na wengine ni kulalamika, ila nimeonyesha dosari.
Kugundua tatizo ni njia ya kutibu. Kama wote tungeona dosari, ingekuwa mwanzo wa kutatua.
Ocky. SULUHISHO NI NINI.
1: Kwa upande wa elimu, tungejikita katika elimu ya utengenezaji, technology, ufundi, ugunduzi tangu awali.
2: Serikali ingewekeza seriously kwa walimu wa ufundi hesabu na science kwa ujumla ama kuwaendeleza waliopo, kuwalipa pesa kubwa na mazingira bora ya utumishi.
3: Kuimarisha miundombinu vijijini inayoleta ubaguzi au ugumu kwa shule za porini na mjini kuwa tofauti.
4: Siasa iachwe ijitegemee bila kuingilia taaluma, na utumishi.
5: Kuwekwa sheria Kali kulinda maliasili zetu zisitoroshwe, kama Australia ambapo ni kosa kubwa kukutwa unasafirisha mnyama adimu anayepatikana kwao tu aitwaye Kangaroo. Ajabu kwetu tunasafirisha mpaka twiga.
6: Kuweka utaratibu wa kuwapata kuwashindanisha kwa interview wataalamu mbalimbali ili kuwaajiri na kuwapatia matazamio hata baada ya kuajiriwa wakishindwa watolelewe kazini.
7: Kuwapeleka nje katika nchi bingwa katika ujuzi kadhaa kwa mkataba vijana na watoto wakubwa walio mahiri katika fani za ufundi ili kujifunza, na kurudi kuanzisha viwanda, technology na fani mbalimbali.
Mengine mtajazia.