luchelele mzunguko
JF-Expert Member
- Feb 12, 2021
- 1,206
- 1,641
Wakuu mimi ninavyofahamu ni kwamba ndoa ni makubaliano ya mwanaume na mwanamke ya kuwa mume na mke.
Lakini makubaliano haya yawe yamedhibitishwa eidha na watumishi wa Mungu au viongozi wa kimila kwa mujibu wa ndoa za kimila au na Hakimu kwa mujibu wa ndoa za kiserikali zote hizi wakiwepo mashahidi wa pande zote mbili za wale wanao funga ndoa wakiwekeana viapo na mambo mengine kulingana na muktadha husika hukiitimishwa kwa kuvishana pete na kutunukiwa vyeti vya ndoa yaani hati miliki na udhibitisho wa kwamba makubaliano yao yapo sawa kisheria.
Sasa tujadili kwa kueleweshana maana siku hizi vijana wanachukuana tu na kuanza kuishi pamoja almaharufu kama sogea tukae na kuanza kuitana mume na mke, hii si sawa kisheria na ndio imekithiri kwa sasa wasichokijua wanawake ni kwamba siku wamegombana na kuamua kutengana hata kama mwanamke alichangia mwanaume kutengeneza mji atashindwa kupata mgawanyo wa mali kwakuwa hana cheti cha ndoa kinachothibitisha kwamba huyu ni mume wake.
Karibuni tulijadili hili jambo kwa manufaa ya wengi