Mkuu, kisheria mkiishi kama mke na mume na jamii inayowazunguka ikatambua hivyo na mkaishi hivyo kwa zaidi ya miaka miwili basi itatafsirika kuwa nyinyi ni wanandoa sawa na tafsiri watakayokua nayo wale waliofunga ndoa kanisani, msikitini ama bomani.
Sasa hapo mnapata haki na wajibu wooote unaowahusu wanandoa ila mkiamua kila mmoja achukue time ndio kutatokea utofauti kidooogo baina yenu karibu tuishi na wale waliofunga ndoa.
Kwa upande wa wale waliofunga ndoa watapatiwa HATI YA TALAKA na wale waliokua wakiishi under 'presumtion of marriage' yaanisogea tuishi watapatiwa hukumu yao ya HATI YA KUTENGANA.
Na baada ya hapo kama kuna mai iliyochumwa pamoja utaratibu ule ule uliozoeleka wa kugawanya mali kwa wanandoa wanaoachana utatumika kwa pande zote. Hivyo hakuna dhurma yoyote itakayotokea.