Kwa pesa ipi? Magufuli alishaanza kukopa kwenye mabenki ya biashara nchini. Halafu Rais SSH kakopa sana mikopo nafuu ya multilateral financial institutions (IDA/WB, ADF/ADB, etc.) ili kuendeleza utekelezaji wa hiyo miradi ambayo hadi sasa bado kabisa kukamilika. SGR yenyewe hata kufika Morogoro tu tabu.
Angekuwa hai wakati huu, hakika watu "wangelimia meno" kama alivyoahidi - very crudely. Mishahara serikalini ingekuwa kama Zaire ya Mobutu, pensheni ndio kabisa, zingefutwa. Pesa za bajeti zingekuwa zinatolewa kishikaji kwa Ujenzi, Majeshi na wateule wachache. It would have been a time of reckoning. Bahati yake na Watanzania kaepushwa na dhahama hiyo.