makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 31,583
- 92,670
Mie sijaona mantiki ya shia kuwwakataa kina Abubakar, walikuwa ni watu wa karibu saana na mtume, lau kama wangekuwa watu wabaya nadhani asingekuwa nao karibu kiasi hicho, kama sikosei abubakari ndio mtu wa kwanza kuupokea uislam nje ya familia ya mtume.Asante, kimfumo mtume alipenda kuwapa wajukuu mamlaka sasa yeye kwa shinikizo ya mkewe akataka madaraka.Na kwa kuwa alipaelewa pale vyema akaonelea aanzishe falsafa zake.Uchu wa uongozi sikui madaraka.
Watu hawa mtume aliwabashiria pepo.. Mtu yupo duniani na tayari inajulikana anaenda peponi.. Si jambo dogo, mtu ambae hafai kwenye uislam isingekuwa hivi.
Mie naona somi hapa, ni kawaida tu kwa watu kutofautiana, hata huku sunni watu wamegawanyika pia, hata huko shia wamegawanyika ndio unawapata mpaka kina agha khan, na ndio maana nabii alitabiri sikku ya kiama kutakuwa na makundi 70+ ila moja tu ndio la peponi.
Madhari mtume hakuwakataa kina abubakar kwenye uhai wake, basi mimi nani niwakatae baada ya umauti wake.. Saydna uthman aliozwa mabinti wawili wa mtume, alikufa mmoja, akamuozesha mwingine, na mwenyewe mtume alisema kama kungekuwepo na binti mwingine angemuozesha pia.
Lakini pia mttume aliacha listi ya wanafiki, ambao wakifa wasiswaliwe na haya majina hakutoa mtume mwenyewe, alipewa na mwenyezi mungu baada ya mtume kwenda kumzika mtu mmoja kumbe ni mnafiki, ndio hapo Mungu akampa majina ya wanafiki..
Kama kweli Abubakar na wenzie hawakuwa wema, basi wwangekuwepo kwenye ile listi.
Swahaba aliyepewa ile listi nimemsahau... Mtume alimwambia hata nikifa, mtu fulani, fulani na fulani msihangaike kwenda kumswalia.