Tofauti ya Sunni na Sh’ia ni ipi hasa?

Tofauti ya Sunni na Sh’ia ni ipi hasa?

Katika uislamu hakuna kundi lilotajwa kisheria (Lililotajwa katika Qur-an) kwamba litaitwa Sunni au Sh'ia na kwamba lipi ni sahih na lipi si sahihi., Kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume wetu S.A.W yanatuambia tushikamane na Qur-an na Sunna (Khadithi) za Kiongozi wetu na Mtume wetu S.AW.

Sasa kundi lolote kati ya uliyotaja na usiyoyataja kama watashikamana na hicho nilichokitaja tulichoamrishwa na Mtume wetu S.W.A basi yatakuwa yote ni sawa lakini kama litatokea kundi katika hayo madhehebu wataacha katika hayo hilo kundi tunasema halifai katika uislamu.

Qura-an Suratul Imran Aya 103

وَٱعْتَصِمُوا۟ بِحَبْلِ ٱللَّهِ جَمِيعًۭا وَلَا تَفَرَّقُوا۟ ۚ وَٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَآءًۭ فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِۦٓ إِخْوَٰنًۭا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍۢ مِّنَ ٱلنَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ١٠٣


And hold firmly to the rope of Allah1 and do not be divided. Remember Allah’s favour upon you when you were enemies, then He united your hearts, so you—by His grace—became brothers. And you were at the brink of a fiery pit and He saved you from it. This is how Allah makes His revelations clear to you, so that you may be ˹rightly˺ guided.
Hapo kwenye hadithi ndio kuna utofauti sasa.
 
Shida ilianzia kwenye kifo cha bwana mtume Muhammad (s.a.w) sunni wanakubaliana na wale viongozi waliofatia baada ya kifo cha mtume, kuanzia Abubakar, umar, uthman, kisha ali.. Sasa shia wao wanaona kulifanyanyika uhuni ali alinyimwa uongozi, hivyo wao ni wafuasi wa ali.. Hao wengine wanaona ni wazinguaji(tutumie lugha hii mbovu)
We ndo umemaliza Kila kitu mkuu.Basi tu watu wataleta ubishi usokuwa na maaana.
 
Aya za Qur'an tunajua Allah sw alimtuma jibril kuzipeleka kwa mtume saw,Hadith Allah sw alimtuma malaika gani kwa mtume na kwa nini mtume saw hakuagiza ziandikwe!?...badala yake zimeandikwa miaka 200 baada ya mtume kufariki!?...kwa nini khalifa ummar alizipiga marufuku!?
Mkuu hiyo Quran unayoijua kwamba Allah sw alimtuma jibril kuipeleka kwa Mtume s.w, Aya zake ndizo zilizosema:-
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ (Anajim Aya 4) ...Hayakuwa anayofanya na kusema Mtume S.A.W isipokuwa ni wahyi kutoka Mwenyezi Mungu (Allah)
Ndio maana sisi waislamu ulimwengu mzima tunafanyia kazi maneno na matendo ya Mtume S.A.W (Khadith), tumefata hili agizo kutoka kwenye hiyo Quran ambayo wewe binafsi unakiri kuiamini.

Je unapo mahali Mtume kaagiza Quran iandikwe maana alipokufa ilikuwa bado haijakuwa kwenye mashaf kama ilivyo leo??? na unaikubali vipi ukatae khadithi za Mtume na mienenendo yake kuandikwa?
 
Pia nimepata kusikia mashia wanaakili na uchumi mzuri na wanasaidiana sana kuliko Suni ni kweli.
 
Kwani wenye akili si walisharekebisha wadhani kila mtu lazima apite madrasa.Muelewage humu kuna watu wa namna zote.Na kukosea imo

Sasa inakuaje mtu ujibu ilihali huna ufahamu na hilo jambo??

Hizi mambo zinataka ukae upate darasa na sio blah blah.
 
Mie sijaona mantiki ya shia kuwwakataa kina Abubakar, walikuwa ni watu wa karibu saana na mtume, lau kama wangekuwa watu wabaya nadhani asingekuwa nao karibu kiasi hicho, kama sikosei abubakari ndio mtu wa kwanza kuupokea uislam nje ya familia ya mtume.
Watu hawa mtume aliwabashiria pepo.. Mtu yupo duniani na tayari inajulikana anaenda peponi.. Si jambo dogo, mtu ambae hafai kwenye uislam isingekuwa hivi.

Mie naona somi hapa, ni kawaida tu kwa watu kutofautiana, hata huku sunni watu wamegawanyika pia, hata huko shia wamegawanyika ndio unawapata mpaka kina agha khan, na ndio maana nabii alitabiri sikku ya kiama kutakuwa na makundi 70+ ila moja tu ndio la peponi.

Madhari mtume hakuwakataa kina abubakar kwenye uhai wake, basi mimi nani niwakatae baada ya umauti wake.. Saydna uthman aliozwa mabinti wawili wa mtume, alikufa mmoja, akamuozesha mwingine, na mwenyewe mtume alisema kama kungekuwepo na binti mwingine angemuozesha pia.



Lakini pia mttume aliacha listi ya wanafiki, ambao wakifa wasiswaliwe na haya majina hakutoa mtume mwenyewe, alipewa na mwenyezi mungu baada ya mtume kwenda kumzika mtu mmoja kumbe ni mnafiki, ndio hapo Mungu akampa majina ya wanafiki..
Kama kweli Abubakar na wenzie hawakuwa wema, basi wwangekuwepo kwenye ile listi.
Swahaba aliyepewa ile listi nimemsahau... Mtume alimwambia hata nikifa, mtu fulani, fulani na fulani msihangaike kwenda kumswalia.
[emoji1787][emoji1787] Kumbe mambo ya nikifa usinizike yalianza zamani sana Duuh.

Bora nimekuwa Mkristo najua thamani ya msamaha.
 
Shida ilianzia kwenye kifo cha bwana mtume Muhammad (s.a.w) sunni wanakubaliana na wale viongozi waliofatia baada ya kifo cha mtume, kuanzia Abubakar, umar, uthman, kisha ali.. Sasa shia wao wanaona kulifanyanyika uhuni ali alinyimwa uongozi, hivyo wao ni wafuasi wa ali.. Hao wengine wanaona ni wazinguaji(tutumie lugha hii mbovu)

Agreed.

Kabla ya Mtume Muhammad (SAW) kufariki, alishawaambia swahaba zake juu ya mtu atakayekua kiongozi baada yake ni Ali(AS).

Lakini mambo yalibadilika baada ya Mtume Muhammad (SAW) kufariki.

Baadhi ya maswahaba walianza mtafaruku mzito sana na tamaa ya kugombania madaraka ilihali walishaachiwa wusia juu ya Ali(AS) ndiye atakuwa kiongozi wa Umma mzima, Lakini walikaidi tena kabla hata ya Mtume Muhammad (SAW) hajazikwa.

“Mimi ni nyumba ya Elimu na Ali(AS) ndiyo mlango wake”- Mtume Muhammad (SAW)

Mtume Muhammad (SAW) aliwahusia maswahaba na watu wengine, wawafuate watu wa nyumba yake(Ahlul Bayt)
 
Kwanza muamini Mungu mmoja tu ambaye hakuzaa wala kuzaliwa ,wala hana mwana wala anayefanana naye,na amini kiwa muhmaad S.a.w ni mtume wake pamoja na mitume kabla yake issa(Yesu),musa,ibrahm mpka adam kuwa hawa ni mitume wa Mungu wametumwa kuufikisha ujembe mmoja wa kuabudiwa mungu mmoja tu na hawajawahi tofautiana.

then tutakupa utafauti murua wa sunn na shea
karibu sana
Issa si Yesu waka Yesu si Issa. Hawana uhusiano wowote
 
Siyo sahihi,
NI BAADA YA KUFARIKI SAYYIDNA ALI BUN ABBI TALIB.

Kundi la kwanza kubwa likamtaka Muawwiyah aendeleze uongozi, wakidai pia mtume alisema utume na uongozi haurithiwi.

Na kundi la pili likataka mjukuu wa mtume aendeleze uongozi through bloodline hasa baada ya maswaaba w4 wakuu wa mtume kufariki wote.
Kuruani inayosemekana haijaacha kitu, je haikuona umuhimu wa kumtaja au Kuweka muendelezo wa uongozi Hadi watu wakarakana? Au kuruani haikuwepo ila maneno na Hadithi za Warak bin nawfal Kwa mwamedi ndo yalikuwepo?
 
Mkuu hiyo Quran unayoijua kwamba Allah sw alimtuma jibril kuipeleka kwa Mtume s.w, Aya zake ndizo zilizosema:-
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ (Anajim Aya 4) ...Hayakuwa anayofanya na kusema Mtume S.A.W isipokuwa ni wahyi kutoka Mwenyezi Mungu (Allah)
Ndio maana sisi waislamu ulimwengu mzima tunafanyia kazi maneno na matendo ya Mtume S.A.W (Khadith), tumefata hili agizo kutoka kwenye hiyo Quran ambayo wewe binafsi unakiri kuiamini.

Je unapo mahali Mtume kaagiza Quran iandikwe maana alipokufa ilikuwa bado haijakuwa kwenye mashaf kama ilivyo leo??? na unaikubali vipi ukatae khadithi za Mtume na mienenendo yake kuandikwa?
Hapo haimaanishi kila neno,ndiyo maana maswahaba walikua wakimuuliza huu ni wahyi au maoni yako,akisema 'nina njaa naombeni tende wake zangu' huo siyo wahyi
Ama kwa upande wa Qur'an aliacha imeandikwa,na haijalishi story za kiwaki kwamba ilikua haijakusanywa
QUR'AN 25:5
Na wakasema,hivi ni visa vya watu wa kale alivyoviandikisha,anavyosomewa asubuhi na jioni
 
Acha kumfananisha Yesu na Nabii bandia chief
Lakini unakubali kua Yesu alikua anakwenda chooni kukata gogo? (kunya).
Unakubali kua Yesu alikua anakula, tena mitonge mikubwa kinoma?

Kiufupi Yesu na mimi tofauti zetu ni zama tu, za kuishi hapa Duniani.
 
Kama PROTESTANTS/ANGLICAN (Anglatère) walivyojichomoa kuupinga utaratibu na mambo ya ROMAN CATHOLICS. Baadaye protestants wakajitokeza LUTHERAN mwasisi akiwa Martin Lutherking (tafakari jina), kuna ORTHODOX (base iko Ussr/Urusi) Wakaendeleza mtifuano na tofauti hadi sasa madhehebu hayaeleweki idadi:
1.....
2.....
3.....
4.....
5.....
6.....
7.....
8.....
9.....
10.….
11.….

Orodha yaweza kuzidi hapo, ila kikubwa nilichokibaliana na wote Islamic&Christian

-Mungu ni mmoja licha ya majina kwa vinasaba vya lugha
-dini zote hazitaji Mungu wa upande wao alikuwa dhebu lipi
-tawasifu za mitume wao zinafanana
-majina kama Nabii Issa/Yesu
-mama wa Issa/Yesu wamekubaliana aliitwa Mariyam/Mariam
-adui wetu ni mmoja Sheikh Twain/shetani
-wote wanahubiri upendo,kusamehe,toba
-wanaamini katika mauti, ufufuo na hukumu
-wamekubaliana uwepo wa pepo na jehanamu

Mengine ni tofauti za kibinadamu kwa maslahi ya kibinadamu
Ila kwenye ushoga tumetofautiana.
Wakristo wameupokea ushoga, kufikia mpaka kuwapa uchungaji mashoga.

Kwenye uislam shoga haruhusiwi hata kuingia msikitini, tena akigundulika kua ni ndigili ni kumuua tu hakuna jinsi.
 
Back
Top Bottom