Tofauti ya Sunni na Sh’ia ni ipi hasa?

Tofauti ya Sunni na Sh’ia ni ipi hasa?

Asante, kimfumo mtume alipenda kuwapa wajukuu mamlaka sasa yeye kwa shinikizo ya mkewe akataka madaraka.Na kwa kuwa alipaelewa pale vyema akaonelea aanzishe falsafa zake.Uchu wa uongozi sikui madaraka.
Mie sijaona mantiki ya shia kuwwakataa kina Abubakar, walikuwa ni watu wa karibu saana na mtume, lau kama wangekuwa watu wabaya nadhani asingekuwa nao karibu kiasi hicho, kama sikosei abubakari ndio mtu wa kwanza kuupokea uislam nje ya familia ya mtume.
Watu hawa mtume aliwabashiria pepo.. Mtu yupo duniani na tayari inajulikana anaenda peponi.. Si jambo dogo, mtu ambae hafai kwenye uislam isingekuwa hivi.

Mie naona somi hapa, ni kawaida tu kwa watu kutofautiana, hata huku sunni watu wamegawanyika pia, hata huko shia wamegawanyika ndio unawapata mpaka kina agha khan, na ndio maana nabii alitabiri sikku ya kiama kutakuwa na makundi 70+ ila moja tu ndio la peponi.

Madhari mtume hakuwakataa kina abubakar kwenye uhai wake, basi mimi nani niwakatae baada ya umauti wake.. Saydna uthman aliozwa mabinti wawili wa mtume, alikufa mmoja, akamuozesha mwingine, na mwenyewe mtume alisema kama kungekuwepo na binti mwingine angemuozesha pia.

Lakini pia mttume aliacha listi ya wanafiki, ambao wakifa wasiswaliwe na haya majina hakutoa mtume mwenyewe, alipewa na mwenyezi mungu baada ya mtume kwenda kumzika mtu mmoja kumbe ni mnafiki, ndio hapo Mungu akampa majina ya wanafiki..
Kama kweli Abubakar na wenzie hawakuwa wema, basi wwangekuwepo kwenye ile listi.
Swahaba aliyepewa ile listi nimemsahau... Mtume alimwambia hata nikifa, mtu fulani, fulani na fulani msihangaike kwenda kumswalia.
 
Waislamu ninyi hua mnanielewesha vizuri kabisa maswali yangu.

Naomba mnipe tofauti kati ya sunni na sh’ia na mnielezee nini kimesababisha tofauti hizo ziwepo na je hua kuna migongano baina ya hayo makundi mawili?

Tafadhali naomba nielimishwe juu ya hayo masuala adhimu ili nipate kujifunza vyema na nipate uelewa.
Katika uislamu hakuna kundi lilotajwa kisheria (Lililotajwa katika Qur-an) kwamba litaitwa Sunni au Sh'ia na kwamba lipi ni sahih na lipi si sahihi., Kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume wetu S.A.W yanatuambia tushikamane na Qur-an na Sunna (Khadithi) za Kiongozi wetu na Mtume wetu S.AW.

Sasa kundi lolote kati ya uliyotaja na usiyoyataja kama watashikamana na hicho nilichokitaja tulichoamrishwa na Mtume wetu S.W.A basi yatakuwa yote ni sawa lakini kama litatokea kundi katika hayo madhehebu wataacha katika hayo hilo kundi tunasema halifai katika uislamu.

Qura-an Suratul Imran Aya 103

وَٱعْتَصِمُوا۟ بِحَبْلِ ٱللَّهِ جَمِيعًۭا وَلَا تَفَرَّقُوا۟ ۚ وَٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَآءًۭ فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِۦٓ إِخْوَٰنًۭا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍۢ مِّنَ ٱلنَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ١٠٣

And hold firmly to the rope of Allah1 and do not be divided. Remember Allah’s favour upon you when you were enemies, then He united your hearts, so you—by His grace—became brothers. And you were at the brink of a fiery pit and He saved you from it. This is how Allah makes His revelations clear to you, so that you may be ˹rightly˺ guided.
 
Siyo sahihi,
NI BAADA YA KUFARIKI SAYYIDNA ALI BUN ABBI TALIB.

Kundi la kwanza kubwa likamtaka Muawwiyah aendeleze uongozi, wakidai pia mtume alisema utume na uongozi haurithiwi.

Na kundi la pili likataka mjukuu wa mtume aendeleze uongozi through bloodline hasa baada ya maswaaba w4 wakuu wa mtume kufariki wote.
We mbona una matango pori Sana,hii historia umeitoa wapi!?
 
Katika uislamu hakuna kundi lilotajwa kisheria (Lililotajwa katika Qur-an) kwamba litaitwa Sunni au Sh'ia na kwamba lipi ni sahih na lipi si sahihi., Kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume wetu S.A.W yanatuambia tushikamane na Qur-an na Sunna (Khadithi) za Kiongozi wetu na Mtume wetu S.AW.

Sasa kundi lolote kati ya uliyotaja na usiyoyataja kama watashikamana na hicho nilichokitaja tulichoamrishwa na Mtume wetu S.W.A basi yatakuwa yote ni sawa lakini kama litatokea kundi katika hayo madhehebu wataacha katika hayo hilo kundi tunasema halifai katika uislamu.

Qura-an Suratul Imran Aya 103

وَٱعْتَصِمُوا۟ بِحَبْلِ ٱللَّهِ جَمِيعًۭا وَلَا تَفَرَّقُوا۟ ۚ وَٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَآءًۭ فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِۦٓ إِخْوَٰنًۭا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍۢ مِّنَ ٱلنَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ١٠٣

And hold firmly to the rope of Allah1 and do not be divided. Remember Allah’s favour upon you when you were enemies, then He united your hearts, so you—by His grace—became brothers. And you were at the brink of a fiery pit and He saved you from it. This is how Allah makes His revelations clear to you, so that you may be ˹rightly˺ guided.
Kila kundi Lina hadithi zake za mtume,ndiyo maana wengine hatutaki hadithi sababu ni uzushi wa wahuni kuwatoa waislam kwenye Qur'an, Bilal bin rabah alikua mweusi na miongoni mwa wa mwanzo kusilimu,lakini hakuna Hadith toka kwa Bilal bin rabah...
 
Kama PROTESTANTS/ANGLICAN (Anglatère) walivyojichomoa kuupinga utaratibu na mambo ya ROMAN CATHOLICS. Baadaye protestants wakajitokeza LUTHERAN mwasisi akiwa Martin Lutherking (tafakari jina), kuna ORTHODOX (base iko Ussr/Urusi) Wakaendeleza mtifuano na tofauti hadi sasa madhehebu hayaeleweki idadi:
1.....
2.....
3.....
4.....
5.....
6.....
7.....
8.....
9.....
10.….
11.….

Orodha yaweza kuzidi hapo, ila kikubwa nilichokibaliana na wote Islamic&Christian

-Mungu ni mmoja licha ya majina kwa vinasaba vya lugha
-dini zote hazitaji Mungu wa upande wao alikuwa dhebu lipi
-tawasifu za mitume wao zinafanana
-majina kama Nabii Issa/Yesu
-mama wa Issa/Yesu wamekubaliana aliitwa Mariyam/Mariam
-adui wetu ni mmoja Sheikh Twain/shetani
-wote wanahubiri upendo,kusamehe,toba
-wanaamini katika mauti, ufufuo na hukumu
-wamekubaliana uwepo wa pepo na jehanamu

Mengine ni tofauti za kibinadamu kwa maslahi ya kibinadamu

-Wote walianzia na watu wa middle east.
 
TOFAUTI IPO:

Kwa kifupi ulisikia SUNNI maana yake wale WAISLAM wanaojinasibisha na kuihuisha Sunnah yaani MAFUNDISHO YA DINI KAMA ALIVYOYAISHI MTUME WA ALLAH REHEMA NA AMANI ZIWE JUU YAKE....

SHIA ilianza kama VUGUVUGU la kisiasa then baadaye kundi hili likawa na misingi yake ya THEOLOGIA na kwa wasomi wengi wa KIISLAM [JAMUHURIL ULAMAAH] wanaliona kundi hili kuwa sii WAISLAM bali ni kama CULT kwa sababu mafundisho yao mengi yapo kinyume na mafundisho ya Mtume wa Allah Rehema na amani ziwe juu yake.
Je Ahamadiya mkuu wao wanaitikadi nini?
 
Hivi mtume alizaa na kujukuu, kizazi chake bado kipo? Kuna mtu alinambia hawa mnaowaita mashariff ni watu wenye genes za koo ya mtume?
Mtume wanawawe wa kiume walikufa mapema.
Qasim598–601 huyu miaka mi3
Zainab599–629 huyu aliolewa na kuzaa
Ruqayyah601–624 alizaa, mwanae alikaa miaka kama mi5 hivi aliolewa na swahaba bwana uthman khalifa wa 3.
Umm Kulthum603–630 huyu nae aliolewa na bwana uthman baada ya kifo cha dada yake rukiya.
Fatimah605–632 huyu ndio alizaa kina hassan, hussein na muhsin, kisha mabinti zaynab na ummukuluthum
Abd Allah611–615 miaka mi4 akafa
Ibrahim630–632 huyu miaka 2 tu.

Ukitizama hapo juu wanawe wa kiume wote hawakuzaa kuendeleza damu ya mtume, kuna baadhi ya watu wanaamini mtoto wa kike haendelezi kizazi chako, hii ni imani kwa jamii nyingi tu.

Hao wajukuu wa mtume kupitia kwa binti zake aidha walikufa mapema ama waliuwawa kwenye ile vita.. So vizazi vyao sivijui vizuri nadhani ni hussein hivi ndio mwanae aliganikiwa kuwa mpaka imam w 4/5 na akaendeleza kizazi, sina hakika kama kiliendelea ama walikufa bila kuzaliana.

Kuhusu masharifu, neno
Sharif linatokana na Sharaf, lenye maana ya heshima au utukufu. Kwahiyo tunaweza kusema Sharif ina maana ya mheshimiwa kwa tafsiri isiyo rasmi. Kuna usemi wa kiarabu, "Man sharrafa nafsahu fahuwa shareef" wenye maana kuwa anayejiheshimu ataheshimiwa.

Shia walitaka dini irithiwe na hii dini si ya ukoo. Dini ni ya kila mmoja, ili mradi ana vigezo basi anastahiki kuongoza watu...
 
Suruali Ndefu vs Suruali Fupi
Umechemsha. Hii shia ni toleo jipya kabisa Wala hawahusiani na wazee wa vipedo. Hawa Wana mfumo wao tofauti wa ibada na wanamtukuza mfuasi a.k.a swahaba wa mtume aitwaye ALLY. Wote wale wa pedo na wale wa kawaida wanawapinga Hawa , misikiti Yao mingi ilikuwa ya wahindi Sasa hivi ndio wabongo wanachipuka kwa Kasi wakiwameza wazee wa vipedo na wale ndugu zetu wasio na makuu wa bakwata. Asili Yao ni Iran
 
Kila kundi Lina hadithi zake za mtume,ndiyo maana wengine hatutaki hadithi sababu ni uzushi wa wahuni kuwatoa waislam kwenye Qur'an, Bilal bin rabah alikua mweusi na miongoni mwa wa mwanzo kusilimu,lakini hakuna Hadith toka kwa Bilal bin rabah...
Kama ukija kwa matusi na kebehi nitaacha huu mjadala., nilisema nikujibu huenda unahitaji faida kwa suali lako lakini naona unaanza kusema hadithi ni uzushi wa wahuni.,

Ukweli ni kwamba sitaweza kuziweka khadithi za Mtume S.A.W zoote hapa JF na kukufahamisha hii ni sahihi na hii ni uzushi., Isipokuwa ufahamu khadithi zipo vigawanyo vingi ambazo ziko sahihi na dhaifu nk.

Sasa turudi darsa kujua hizo tusome mimi na wewe, ndivyo sharia ilivyotaka tusome na sio kuja hapa na matusi na kusema khadithi ni uzushi wa wahuni.
 
Aya za Qur'an tunajua Allah sw alimtuma jibril kuzipeleka kwa mtume saw,Hadith Allah sw alimtuma malaika gani kwa mtume na kwa nini mtume saw hakuagiza ziandikwe!?...badala yake zimeandikwa miaka 200 baada ya mtume kufariki!?...kwa nini khalifa ummar alizipiga marufuku!?
 
Rudi ukasome tena ndugu, Ali (AS) alimuoa mjukuu wa mtume???

Rudi tena madrasa tena kimbia
Kwani wenye akili si walisharekebisha wadhani kila mtu lazima apite madrasa.Muelewage humu kuna watu wa namna zote.Na kukosea imo
 
An impressive share! 
Thanks, I've just been searching for information about this topic for a long time and yours is the best I have come upon so far.
But, I have more tips that best explain more about the "Nathaniel Bassey Hallelujah Challenge Live 2023"Hallelujah Challenge Live 2023 and how to access them freely and easily I'm happy that I found this in my hunt for something relating to this.
You won't want to miss out.
 
Hivi mtume alizaa na kujukuu, kizazi chake bado kipo? Kuna mtu alinambia hawa mnaowaita mashariff ni watu wenye genes za koo ya mtume?
Mtume alizaa na kujukuu,hao waitwao masharifu hawana nasaba na mtume,na hata wangekuwa nayo haiwasaidii chochote na haiwafanyi wawe wachamungu
 
Hadithi ni hadithi ikishasimuliwa ni hadithi, hata biblilia ina hadithi na ni hadithi.Swala hapa hadithi hizi ni kweli ama uzushi.Ina maana tusipokee mengi ya mtu mzito kama mtume kisa tutaambiwa ni hadithi.MWAGA NONDO.
 
Mtume wanawawe wa kiume walikufa mapema.
Qasim598–601 huyu miaka mi3
Zainab599–629 huyu aliolewa na kuzaa
Ruqayyah601–624 alizaa, mwanae alikaa miaka kama mi5 hivi aliolewa na swahaba bwana uthman khalifa wa 3.
Umm Kulthum603–630 huyu nae aliolewa na bwana uthman baada ya kifo cha dada yake rukiya.
Fatimah605–632 huyu ndio alizaa kina hassan, hussein na muhsin, kisha mabinti zaynab na ummukuluthum
Abd Allah611–615 miaka mi4 akafa
Ibrahim630–632 huyu miaka 2 tu.

Ukitizama hapo juu wanawe wa kiume wote hawakuzaa kuendeleza damu ya mtume, kuna baadhi ya watu wanaamini mtoto wa kike haendelezi kizazi chako, hii ni imani kwa jamii nyingi tu.

Hao wajukuu wa mtume kupitia kwa binti zake aidha walikufa mapema ama waliuwawa kwenye ile vita.. So vizazi vyao sivijui vizuri nadhani ni hussein hivi ndio mwanae aliganikiwa kuwa mpaka imam w 4/5 na akaendeleza kizazi, sina hakika kama kiliendelea ama walikufa bila kuzaliana.

Kuhusu masharifu, neno
Sharif linatokana na Sharaf, lenye maana ya heshima au utukufu. Kwahiyo tunaweza kusema Sharif ina maana ya mheshimiwa kwa tafsiri isiyo rasmi. Kuna usemi wa kiarabu, "Man sharrafa nafsahu fahuwa shareef" wenye maana kuwa anayejiheshimu ataheshimiwa.

Shia walitaka dini irithiwe na hii dini si ya ukoo. Dini ni ya kila mmoja, ili mradi ana vigezo basi anastahiki kuongoza watu...
💕🙏
 
Back
Top Bottom