SI KWELI Tohara hupunguza ukubwa wa sehemu za siri za mwanamme

SI KWELI Tohara hupunguza ukubwa wa sehemu za siri za mwanamme

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wataalamu wa afya huelezea umuhimu na faida za kufanyika kwa tendo hili kwa wanaume.

Baadhi ya sehemu wanaume huwa hawatahiriwi kabisa, na wengine wanaotahiri husubiri hadi mtoto afikishe walau miaka 12 ndipo afanyiwe tendo hilo kwa uoga wa kupunguza ukubwa wa viungo hivyo.

B9D7E489-4826-4743-A8E2-CB85C73E2EF3.jpeg

Madai haya yamekuwepo kwa muda mrefu, na majibu sahihi bado hayajatewa. Ni kweli kuwa tohara hupunguza ukubwa wa via vya uzazi vya mwanamme?
 
Tunachokijua
Ni upasuaji mdogo unaofanyika ili kuondoa ngozi ya mbele inayofunika sehemu za siri za mwanamme.

Asili ya utamaduni huu ni imani za kidini, ambazo baadae zilithibitishwa kuwa na faida kiafya. Leo, watu hutahiri kwa sababu za kiafya, au za kidini.

Tohara ifanyike Hospitalini
Mwanamme huzaliwa na ngozi inayofunika uume. Kupitia tohara, ngozi hii huondolewa kwa kufanya upasuaji mdogo usiotumia muda mrefu sana, kati ya dakika 15-30.

Kwa sababu za kiusalama, pamoja na kuhakikisha kuwa tendo hili linafanyika kwa ufanisi mkubwa, ni vizuri kama likifanywa hospitalini.

Tohara kupunguza ukubwa wa uume
Tofauti na jinsi ambavyo watu wengi huamini, tohara haiwezi kudumaza afya ya sehemu za siri za mwanamme hata kama itafanyika kwa mtoto mchanga.

Ukuaji wa viungo vyote vinavyounda mwili wa binadamu huongozwa na mifumo rasmi iliyoshikizwa kwenye vinasaba vya urithi pamoja homoni mbalimbali za mwili.

Msingi wa taarifa hizi hauwezi kuathiriwa kwa kukata ngozi ya mbele inayofunika sehemu hizo.

Kama ambavyo mtu huzaliwa akiwa na asili ya urefu, ufupi, macho makubwa au kipara na asiwe na uwezo wa kuibadili asili hii, vivyo hivyo kwa ukubwa au udogo wa maungo haya muhimu kabisa kwa afya ya uzazi wa mwanamme kwa sababu kinacho ondolewa ni ngozi tu, siyo kichwa wala nyama ya sehemu hizo.

Aidha, Dkt. Godfrey Chale ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi nchini Tanzania akizungumza na JamiiForums amesema kuwa madai haya hayana ukweli.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, miongozo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Kituo cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa (CDC), tohara huwa na faida nyingi kwa afya ya mwanamme mwenyewe, pamoja na mwanamke ambaye atashiriki naye tendo la ndoa.
  1. Tohara hupunguza nafasi ya kupata maambukizi ya mara kwa mara kwenye mfumo wa mkojo hasa kwa watoto wadogo.
  2. Hupunguza nafasi ya kuugua Saratani ya uume pamoja na magonjwa mengine ya zinaa hasa VVU/UKIMWI
  3. Hupunguza uwezekano wa kuugua saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake. Hii ni kutokana na ukweli kuwa mwanamme asiye tahiriwa huwa na uwezekano mkubwa wa kubeba Virusi vya Human papilloma kuliko yule aliyetahiriwa.
  4. Tohara husaidia pia kurahisisha suala la usafi kwa mwanamme.
Tohara inaweza kufanyika muda wowote, kwa watoto wachanga pamoja na watu wazima, hata hivyo uponaji wa haraka huonekana kwa watoto kwa kuwa huwa bado hawajafikia umri wa kuonesha mwitikio wa hisia za kimapenzi hivyo kuufanya uume usimame mara kwa mara kama ilivyo kwa watu wazima.

Katika dini za Kiyahudi, tendo hili la kiimani hufanyika siku ya 8 tangu kuzaliwa kwa mtoto. Kwa ujumla wake, jamii mbalimbali huamua kwa kadri wao wanavyoona inafaa ni lini hasa tohara ifanyike kwa vinaja wao wa kiume.
Binafsi nimetahiriwa lakini kila demu anayebahatika kukutana na mkuyenge wangu lazima aombe poo! Maana unagusa mpaka nje ya cervix
 
Wataalamu wa afya huelezea umuhimu na faida za kufanyika kwa tendo hili kwa wanaume.

Baadhi ya sehemu wanaume huwa hawatahiriwi kabisa, na wengine wanaotahiri husubiri hadi mtoto afikishe walau miaka 12 ndipo afanyiwe tendo hilo kwa uoga wa kupunguza ukubwa wa viungo hivyo.

View attachment 2410644

Madai haya yamekuwepo kwa muda mrefu, na majibu sahihi bado hayajatewa. Ni kweli kuwa tohara hupunguza ukubwa wa via vya uzazi vya mwanamme?
Naunga hoja 100% ...kama kuna anaebisha ajaribu kufanya research atakuja na majibu.
 
Tohara ya utotoni inaathiri ndio ilo alina kupinga nina ushahidi na ilo swala for 100%
Hata mimi na ushahidi ni kweli ina athiri zaidi ya 90% mashine inakua fupi au kimbaumbau/nyembamba kama fimbo au inakua na sifa zote mbili..
 
Kuhusu kuwa kafupi si sahihi coz inayokatwa ni ngozi na si penis yenyewe

Ufupi au urefu unatokana na genetics
Mazingira yanachangia pakubwa tu urefu na ufupi.

Hapa suala ni tunataka kuziendesha sababu zote ziwe upande wetu kadri tunavyoweza ili kupata matokeo tunayoyataka sie.

Observation ya boarding inaonesha waliotahiriwa vichanga zilikuwa hazikui ukilinganisha na waliotahiriwa wamejitambua.
 
Habari yako...
Nimekutana na habari hiyo katika stori za hapa na pale nikiwa na marafiki. Jamaa anasema hataki kumtahiri mwanae mapema maana anachelea mtoto atakuwa akichekwa na wenzake ukubwani kwa kuwa na uume mdogo

Naomba ushahidi wa kitaalamu katika hili au hata uzoefu tu.
 
Ni uongo kua tohara upunguza maumbile ya uume
Tohara haiingiliani na udogo /ukubwa wa uume.zaodi kitaalamu imefanyiwa tafiti na serikali kupitia wizara yetu pendwa ya afya imeauthorize kua tohara ya watoto na watu wazima zifanyika.
 
Back
Top Bottom