"JIPU LA POOL COLLECTION ACCOUNT BUGANDO HOSPITAL MWANZA"
SIFA YA HII ACCOUNT-NO COST ANALYSIS,FIXED AMOUNT FOR 3DAYS
-NI MAAMUZI YA SERIKALI KWA WANANCHI WAKE.
Kwa mgonjwa anaelazwa anatakiwa atoe 150,000/=cash au kupitia bima ya afya,hii hela hudumu kwa siku 3,na siku ya 4 unaanza kulipia extra charge(40,000/-) kama utaendelea kukaa hospitali, ila hela hii wengi wamechargiwa na kulipia gharama zingine kama vipimo na dawa(ndani ya hizo siku 3)wakiwa ndani ya kifurushi cha matibabu, na mbaya zaidi ikatokea ukakaa cku moja hii hela haina maelezo ya aina ya matibabu umepata na gharama gani umetumia, hivyo ikitokea ulilazwa kwa dharula au kimakosa imekula kwako utajibiwa kirahisi kuwa "HELA IMETOSHA, HUDAIWI"
Kwa Mgonjwa anelazwa na kuhitaji upasuaji unawajibika kulipa 320,000/- vile vile nimekutana na vilio mtu analipa hii pesa na bahati mbaya mtaalam wa upasuaji huo akiwa hayupo,imekwenda na maji,vilio ni vingi kuhusu malipo haya.
Bahati nzuri nimekaa na uongozi wa hospitali mara ya kwanza kunionea huruma, kiongozi aliniandikia nirejeshewe 100,000/-lakini alivyokwenda kumuona mkurugenzi kuidhinisha, wakabatilisha na nikajibiwa kuwa haya ni maagizo ya serikali, nikaomba kama kuna waraka wowote, niliambiwa hapana!kwa mtaji huu serikali itakusanya fedha hata haramu kwa watu wa hali ya chini kwa mfumo wa POOL COLLECTION ACCOUNT.-
Mh.Ummy Mwalimu, na Naibu Mh Kigwangala.,