Jipu kubwa lipo TAZARA.
Kuna wakurugenzi 7 toka uongozi wa Waziri Nundu mpaka sasa wapo. Nundu aliwasimamisha kazi kupisha uchunguzi akaja Mwakyembe kuwarudisha kwa madai ya taratibu zilikiukwa, sasa wameongezeka na kufikia 19.
Mwanzo alikuwepo Ndg Ally Iddy - Head of Commercial, Mr Ayeshi-HHR, Ndg Kasumbai-Marketing Manager, Mrs Masilisi - Finance Manager, Ndg Kamugisha - Ag RGM, Ndg Mabala - Corperate Secretary, Ndg Longino - Head of Passenger, hawa pamoja na hujuma za wizi wa fedha bandalini pia wameshiriki kuuza karakana ya TAZARA likiwa na jengo lenye Standby generator yenye uwezo wa kusambaza umeme karibu wilaya yote ya Temeke. Teknolojia ya mchina!
Mbaya zaidi Serikali iliwaingiza wafanyakazi wa TAZARA keenye payroll ya azina, yaani serikali iliamua kulipa mishahara tangu mwaka jana july kipindi ambacho wafanyakazi wanadai mshahara wa January mpaka June, serikali iliagiza mamlaka ilipe mshahara wa January to June mwaka jana na yenyewe ianze kulipa toka july mpaka June mwaka huu.
Pesa imeliwa japo treni zinatembea za mizigo na abiria nadhani nyinyi baadhi ni mashahidi, hamsikii tena migomo TAZARA lkn toka mwaka jana hakuna hata senti iliyolipwa kwa wafanyakazi hela yote imeliwa na tumeimba sana na hela hii inavyoliwa kweupee.
Tuna uchungu na hela ya serikali, inalipa mishahara ila hii inayozalishwa inaliwa,, jipu lije litumbuliwe