Nataka nigundue msingi wa wanaompinga magufuli umelala sehemu Gani? Ni Kwa ajili ya mabishano ya kisiasa? Kama tulivozoea? Au ni Kwa ajili ya kutetea Maslahi ya wengi
Hakuna moja, kuna elfu moja na moja.
Magufuli hataki mjadala, ana hulka ya udikteta, anajiona anajua kila kitu, kasema watu watalimia meno. Kasema wasio na nauli watapiga mbizi.
Anafuga mtu aliyeiba mpaka jina na kufoji vyeti, huku akijinadi anapiga vita waliofoji vyeti.
Hana muelekeo wa kisiasa unaoleweka. Leo anaweza kuvunjia nyumba watu mabondeni bila simile (si mtetezi wa wanyonge) kesho akaachia Wamachinga wafanye biashara bila mipango (anatetea wanyonge bila mpango endelevu).
Magufuli haheshimu uhuru wa bunge, kalipangia bunge jinsi ya kutumia fedha za tafrija bila hata makubaliano na Spika.
Magufuli haheshimu uhuru wa bunge. Kaapisha wabunge wa kuteuliwa wawe mawaziri kabla hawajaapishwa kuwa wabunge.
Magufuli haheshimu uhuru wa mahakama. Kahutubia mahakama na kuzielekeza jinsi ya kufanya kazi wakati mahakama ni mhimili unaojitegemea.
Magufuli hathamini utenganifu wa serikali na kanisa. Anahutubia habari za kisiasa makanisani. Hili linaweza kuleta mtafaruku na mpasuko wa nchi kidini. Nyerere alikuwa anasali St. Peters kila siku akiwa Dar. Mwinyi aliswali sana Msikiti wa Tambaza. Mkapa alisali sana kanisa la St. Immaculata. Kikwete naye pia motto wa Bagamoyo msikiti anaujua. lakini wote hawa hawakuwahi kuhutubia siasa kwenye madhabahu ya dini to my knowledge, ukiondoa maneno machache tu ya shukurani labda.
Huyu Magufuli anatoa hotuba ya siasa kabisa, kanisani!
Magufuli hatahamini utawala wa sharia. Kawaambia Polisi wakiona gari la kawaida linaenda kwenye lane ya mwendokasi, walichukue, walipeleke polisi, watoe matairi, mwenyewe akija kuulizia matairi wamwambie lilikuja hivyo hivyo bila matairi.
Magufuli hana heshima hata kwa mawaziri wake. Anawaruka bila hata uchunguzi. Mke wa Waziri wake wa karibu kaonewa/ wamepishana maneno kidogo na trafiki, jibaba kaingilia issue na kuvunja utaratibu wa mtu kupandishwa cheo polisi.
Magufuli hataki hata kusoma hotuba anazoandikiwa, matokeo yake anasema madudu.
Magufuli anapenda maamuzi ya ghafla na jazba ambayo hayajachekechwa vizuri na mara nyingine yana athari kwa taifa.
Magufuli ana kauli za kijinga kama motto anayebalehe, ona alivyomdhalilisha Mama Kikwet, mke wa bosi wake wa zamani, kwa kumwambia maneno yasiyo staha hadharani.
Magufuli hawezi mijadala ya kisiasa. Ndiyo maana kapiga marufuku mikutano ya siasa ya wapinzani kinyume na katiba.
I could go on and on and on. kwa nini unataka niseme moja tu?
Msingi mkubwa ni kwamba Mgufuli hana uwezo wa kuwa rais.
Mtu kama huyu hafai kuwa kiongozi.