Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Kusiwe na double standards katika utendaji wake. Akumbuke RAIA wote tuna hadhi sawa mbele ya sheria!
Hizo double standard ni yeye anafanya au vyombo husika.. Kama ni yeye anamuoenea mtu Sasa wewe unakuwa unajuaje kama ni kweli kaonewa au katenda kosa kweli.. Kati yako na rais Nani anauwezo wa kupata taarifa nyingi achilia mbali usahihi wa hizo taarifa... Na kama ni yeye anafanya double standard kutokana na KAULI zake je akiamua kuwa km bubu akawa anafanya kazi na haonekani public mara Kwa mara..je utaridhika?
 
Kuheshimu miktaba ya uwekezaji. Hiyo itasaidia sana uwekezaji wa ndani na nje kuongezeka. Uwekezaji utawafanya watanzania wengi wapate ajira. Uwekezaji utasaidia sana mzunguko wa pesa kuongezeka. Mzunguko wa pesa ukiongezeka kutawahakikishia wananchi wa hali ya chini kupata soko kwa shughuli zao wazifanyazo kama vile Mama nitilie, mafundi ujenzi, wapaka rangi, wapakizi wa mizigo, wakulima na wauzaji wa mboga mboga, n.k.

Kwa sasa wawekezaji wengi hawana confidence na Tanzania.
 
Nataka nigundue msingi wa wanaompinga magufuli umelala sehemu Gani? Ni Kwa ajili ya mabishano ya kisiasa? Kama tulivozoea? Au ni Kwa ajili ya kutetea Maslahi ya wengi

Hakuna moja, kuna elfu moja na moja.

Magufuli hataki mjadala, ana hulka ya udikteta, anajiona anajua kila kitu, kasema watu watalimia meno. Kasema wasio na nauli watapiga mbizi.

Anafuga mtu aliyeiba mpaka jina na kufoji vyeti, huku akijinadi anapiga vita waliofoji vyeti.

Hana muelekeo wa kisiasa unaoleweka. Leo anaweza kuvunjia nyumba watu mabondeni bila simile (si mtetezi wa wanyonge) kesho akaachia Wamachinga wafanye biashara bila mipango (anatetea wanyonge bila mpango endelevu).

Magufuli haheshimu uhuru wa bunge, kalipangia bunge jinsi ya kutumia fedha za tafrija bila hata makubaliano na Spika.

Magufuli haheshimu uhuru wa bunge. Kaapisha wabunge wa kuteuliwa wawe mawaziri kabla hawajaapishwa kuwa wabunge.

Magufuli haheshimu uhuru wa mahakama. Kahutubia mahakama na kuzielekeza jinsi ya kufanya kazi wakati mahakama ni mhimili unaojitegemea.

Magufuli hathamini utenganifu wa serikali na kanisa. Anahutubia habari za kisiasa makanisani. Hili linaweza kuleta mtafaruku na mpasuko wa nchi kidini. Nyerere alikuwa anasali St. Peters kila siku akiwa Dar. Mwinyi aliswali sana Msikiti wa Tambaza. Mkapa alisali sana kanisa la St. Immaculata. Kikwete naye pia motto wa Bagamoyo msikiti anaujua. lakini wote hawa hawakuwahi kuhutubia siasa kwenye madhabahu ya dini to my knowledge, ukiondoa maneno machache tu ya shukurani labda.

Huyu Magufuli anatoa hotuba ya siasa kabisa, kanisani!

Magufuli hatahamini utawala wa sharia. Kawaambia Polisi wakiona gari la kawaida linaenda kwenye lane ya mwendokasi, walichukue, walipeleke polisi, watoe matairi, mwenyewe akija kuulizia matairi wamwambie lilikuja hivyo hivyo bila matairi.

Magufuli hana heshima hata kwa mawaziri wake. Anawaruka bila hata uchunguzi. Mke wa Waziri wake wa karibu kaonewa/ wamepishana maneno kidogo na trafiki, jibaba kaingilia issue na kuvunja utaratibu wa mtu kupandishwa cheo polisi.

Magufuli hataki hata kusoma hotuba anazoandikiwa, matokeo yake anasema madudu.

Magufuli anapenda maamuzi ya ghafla na jazba ambayo hayajachekechwa vizuri na mara nyingine yana athari kwa taifa.

Magufuli ana kauli za kijinga kama motto anayebalehe, ona alivyomdhalilisha Mama Kikwet, mke wa bosi wake wa zamani, kwa kumwambia maneno yasiyo staha hadharani.

Magufuli hawezi mijadala ya kisiasa. Ndiyo maana kapiga marufuku mikutano ya siasa ya wapinzani kinyume na katiba.

I could go on and on and on. kwa nini unataka niseme moja tu?

Msingi mkubwa ni kwamba Mgufuli hana uwezo wa kuwa rais.

Mtu kama huyu hafai kuwa kiongozi.
 
Kuboresha maslahi ya watumishi wa umma hasa walimu na wauguzi hasa wale wanaofanyia kazi.mazingira magumu ya vijijini. Yaani wanaokubali.kufanya kazi mazingira magumu wanakuwa na maslahi na marupu rupu mazuri kupata wa mjini
FYI: wananchi wengi.Tanzania wanaishi vijijini na maeneo ya mijini wapi Kiasi (sema wanaonekana wengi kwa sababu ya kuishi mahala pamoja kama dar).
 
Nataka nigundue msingi wa wanaompinga magufuli umelala sehemu Gani? Ni Kwa ajili ya mabishano ya kisiasa? Kama tulivozoea? Au ni Kwa ajili ya kutetea Maslahi ya wengi
hili swali lako linaweza kuwa gumu na kuwa na wachangiaji wachache kwa kuwa wengi bado ni kama tunaendeshwa na upepo na hatujui tunataka nini hasa zaidi ya kujipanga kushindana na serikali na sio kutafuta fursa ufanyiwe nini?
mimi binafsi ningependa kodi zishuke kwa wawekezaji wa ndani na hasa kwa wawekezaji wa kati na isiwepo kwa wanaoanza shughuli zao.
kodi zimekuwa nyingi na kwa kiasi fulani zinaumiza hasa milolongo ya kodi. jopo kiukweli si kubwa kama wnavyolipa wafanyakazi.
kingine serikali ifute madeni ya wanafunzi wa bodi ya mikopo na badala yake ifikirie kufanya yafuatayo:-
  1. iweke sheria kuwa kila kampuni iliyosajiliwa iwe na graduate wasiopungua watatu
  2. iweke kima cha chini cha mshahara ambacho kinaweza kukithi kwa kiasi fulani maisha ya mfanyakazi sio 450,000-700,000 ambazo wengi wanalipwa.
  3. mishahara yao iongezeke kila mwaka angalau kwa asilimia kumi (10%)
  4. bodi ya mikopo ichangiwe kutokana na pato linalopatikana kwa PAYE asilimia 20% zichangie bodi hii na bodi ibadilishiwe majukumu yake. hivyo serikali iwe na wajibu wa kuwatafutia waliohitimu kazi na kuhakiksha wanalipwa vizuri badala ya mfumo wa sasa serikali haiwajibiki kuwatafutia kazi na kujua wanalipwaje hivyo kama serikali inataka kusomesha watu wengi wakusanye nyingi kwenye PAYE kwa kuongeza ajira na mishahara.
haya mawili rais unaweza kufanya hata kesho we amua tu
 
1.hataki mijadala.. Mijadala ipi mbona TAASISI nyingi tu zinaendelea na vikao kuhusu masuala yao ya kiutendaji. Mijadala Gani unataka
2.kaiba CHETI, ukiambiwa ulete ushahid unasema Gwajima KASEMA kwanini rais a deal na mambo ya mitandaoni tena mepesi kama haya. Hivi kweli upo serious una amini kaiba CHETI.
3.kuvunjia watu nyumba Unaamini anafanya yeye kabla ya mamlaka husika kufanya uchunguzi na kugundua madhara yatakayokuja.. Embu assume we ni rais na una roho mbaya je kuvunja nyumba za watu unapata faida Gani. Rais ananufaika vipi hapo.. Jamani amkeni ndugu ZANGU serikali ina vyombo vingi wakati mwingine kutimiza majukumu Yake unamuona rais anamkosea mmiliki wa nyumba inayoweza kuingiza maji na kuua watu.
4.fedha zimetumika kufanya jambo Zuri la kuchangia madawati bado tu na Hilo huhitaji kuskia ndugu
5.hivi magufuli kuwaelekeza mahakama kwamba washughulikie kesi haraka nako amekosea? Ila ikumbukwe yeye ni mkuu wa nchi anasimama juu ya mihimili mingine Ila kizuri Anatoa maelekezo ambayo kikatiba yuko sawa
6.ni kosa rais kutoa mwelekeo wa serikali Yake Kanisani.. Na wakati kanisa linakuwa linajua kuwa kutakuwa na ugeni wa mkuu wa nchi. Kosa hapo silioni
7.kumpandisha mtu cheo Utaratib wa nini wakati katiba Inasema kabisa yeye ndio amiri jeshi mkuu.. Mamlaka hiyo yapo chini Yake..
8.hataki kusoma hotuba. Kavunja sheria Kivipi na hayo unaposema madudu HAUPO sawa. Rais ni amiri jeshi HUTAKI aongoze watu Sasa nini maana ya kuwa rais. Mwelekeo wa serikali Yake atautoaje Bila kuongeza maneno anayoyamini
Mimi nasema kwamba magufuli anafanya vizuri Sana Ukitulia na ukijua kuwa tuluchelewa kupiga hatua, hutampinga magufuli.. Pamoja na mapungufu aliyonayo madogo bado anatufaa Sana
 
Akipunguza roho ya visasi, chuki , wivu , majivuno na kujiona mfalme hakika ataleta tumaini walau kidogo kwa wananchi wanyonge..
 
Back
Top Bottom