Mheshimiwa Waziri wa Elimu, naomba kuuliza swali hili na nitaomba ama kupata majibu au kufanyiwa kazi kwa nitakachouliza.
Kwa nini wamiliki wa shule za PRIVATE za Primary wamekuwa wakiwapokea wanafunzi wa darasa la kwanza na kwenda nao mpaka darasa la SITA bila usumbufu wowote lakini wanapoingia darasa la SABA wamekuwa na tabia ya KUWATIMUA wanafunzi ambao wanakuwa hawajafikisha wastani wanaoutaka wamiliki wa shule hizi?
Mtu amelipia ada kubwa kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la SITA, akifika tu darasa la SABA mzazi anaambiwa ampeleke mtoto wake kwenye shule za Serikali.
Kwa nini kuwasumbua wazazi kiasi hiki?
Kwa nini serikali haiwachukulii hatua wamiliki wa shule hizi?
Je, shule za Serikali ni Dampo?
Naomba serikali iandike waraka maalumu kulaani vitendo hivi viovu na kutoa mwongozo na onyo maalumu kuzuia tabia hii.
Mungu ibariki Tanzania, Rais, Mawaziri na Watanzania wote. Ahsante.